Mungu tusaidie Watanzania tusio na hatia! Basi laendelea kuchafua hali ya hewa, Lauwa!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
WanaJF! Usiposiba ufa utajenga ukuta! Ni msemo ulikwisha nenwa kitambo na sasa inajidhihisha nyakati hii wakati Ndg,jamaa na hata marafiki wanavyozidi kutoweka kwa ajali ya barabarani. Basi la Sumry leo limeangukana na kuuwa watu wawili hapo hapo mkoani Mbeya na kujeruhi zaidi ya watu 20. MUNGU tusaidie!
 
Sumry tena???...inaonekana kuna tatizo la kiutawala ndani ya Sumri, kwa kumukumbu zangu hii itakuwa ajali ya nne kama siyo ya tano katika mwaka huu
 
Ajali ni tatizo ambalo hamna anayelifanyia kazi Tanzania, limeachiwa hawa wajinga wa Polisi sijui tutakufa hadi lini ndipo serikali iwe serious na swala la usalama barabarani
 
Roho za watanzania zinaendelea kuteketea barabarani.Ajali za barabarani zinauwa kuliko ukimwi au Malaria.Sio lazima tumwajiri waziri mashuhuri wa Kenya hon'ble John Michuki ili kuleta heshima barabarani.

Sheria za usalama barabarani na Usafiri zinahitaji kusiamiwa ipasavyo na kuwajibishana kulingana na kanuni na sheria.

Natoa pole kwa ndugu jama na marafiki waliofiawa,Mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu pema peponi na kuwapa faraja ndugu jama na marafiki.Majeruhi poleni sana na balaa hili,mwenyezi Mungu awajalie nafuu

Kwa kweli inaumiza sana kuona watanzania wenzetu wanavyopata vilema na kupoteza maisha kwa sababu ya uzembe au mapungufu katika usiamizi wa sheria za usalama na usafiri
 
RIP-iwapendwa na poleni jamaa na ndugu wa marehemu. Mungu awafariji. Ila Tanzania uongozi ni kuchunga matumbo yao tu-traffik wanatafuta makosa madogo ili wale lakni usalama wa barabarani imekuwa tatizo kubwa sana kwa wananchi.Tuna uchungu sana
 
kafara imetolewa. inaonyesha mmiliki wa hiyo kampuni alikuwa na deni kubwa la damu sasa ndo yuko mbioni kukamilisha zoezi. This is in another side of our physical world. Devil and his people are very busy working. If you believe in God, before travelling, you should first pry, if you can touch the bus its good, Dont let nobody understand what you are doing.
 
Ajali zinaua, zinaacha wayu wengi waliopoteza viungo. Kwani hata la kudhibiti ajali tunahitaji wawekezaji?
 
Wafiwa poleni sana .Na Marehemu wapumzike kwa amani .Je ni nani anamiliki haya ma Bus ? Kama ni Mbunge wa CCM au kama ni Ma CCM basi suluhu hapa hakuna .Poleni sisi watanzania.
 
Wafiwa poleni sana .Na Marehemu wapumzike kwa amani .Je ni nani anamiliki haya ma Bus ? Kama ni Mbunge wa CCM au kama ni Ma CCM basi suluhu hapa hakuna .Poleni sisi watanzania.
Mkuu! Mmliki wa mabasi haya ya Sumry nasikia ni Fisadi mmoja wa Sumbawanga mjini na ameshawahi kuwa mbunge kwa tiketi ya chama cha magamba kbl ya uchaguzi wa october mwaka jana na cjui mpk leo ndiyo mbunge cjajui ila ana asili ya shombeshombe na bila shaka tuna haja tukiwa kama abiria haina haja ya kupanda haya mabasi ya kampuni hii.
 
Chakushangaza ajali hizi tunajulishwa hapa jf but vyombo vya habari haviandiki wala kutangaza ajali za sumry je kunanini?rip all.
 
WanaJF! Usiposiba ufa utajenga ukuta! Ni msemo ulikwisha nenwa kitambo na sasa inajidhihisha nyakati hii wakati Ndg,jamaa na hata marafiki wanavyozidi kutoweka kwa ajali ya barabarani. Basi la Sumry leo limeangukana na kuuwa watu wawili hapo hapo mkoani Mbeya na kujeruhi zaidi ya watu 20. MUNGU tusaidie!
Asante mungu mpnzi wangu kaponb ktk ajali hiyo,japo anadai kapata maumivu ya mguu.Poleni kwa waliopoteza ndug na jamaa.Ajali imetokea Ileje,gari yenyewe haijamaliza hata mwezi kupiga trip zake huko
 
Tafadhali sali kwanza kabla ya kusafiri. ukweli ni kwamba hii ni kazi ya shetani tu na wala si mipango ya Mungu. Haya mambo ya kishirikina yapo kila mahali duniani hata Ulaya na America pia. Kaa na YESU vizuri atakulinda salama salmini. AMEN
 
Wanapenda league hawaziwezi,nashangaa kuna mabasi yanakwenda kasi kuliko hata hiyo sumry lakini siyasikii kupata ajali!,madereva wao hawako makini.Kuhusu umiliki wa kampuni,nijuavyo mimi,sumry ni za bwana Abdallah sumry aliyekuwa mbunge wa huko Rukwa(jimbo silijui).Lakini kuna yale mengine nissan-UD(luxury) za malaysia inasemekana ni za yule kiranja mkuu wa mawaziri wote!
 
Chakushangaza ajali hizi tunajulishwa hapa jf but vyombo vya habari haviandiki wala kutangaza ajali za sumry je kunanini?rip all.
Best! Hakuna hata chombo moja hata cha hbr kimetangaza hbr hii. Mi cjui 2naelekea wapi na hw viongozi wabovu 2liowekewa madarakani.
 
Back
Top Bottom