Mungu niondolee hulka ya kuwaamini wanasiasa

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,662
Kama kuna kosa nililifanya na bahati mbaya likaota mizizi moyoni mwangu ni suala la kuwaamini wanasiasa hususani wa nchini kwangu.

Mara ya kwanza nilimuamini sana Lowassa nikaamini ndiye mwanasiasa pekee jasiri na mwenye kutuvusha katika Tanzania yenye kila hitaji. Akatuacha CCM akaenda UKAWA na huko nikajipa moyo kuwa atakuwa rais na kwa vile hana visasi Serikali yake huenda ikachukua viongozi wa kutoka CCM ili mradi tu Tanzania isonge mbele.

Nikamuamini Dr. Slaa nikizingatia ashawahi kuwa Padri!!

Nikamuamini Zitto na yeye akaniacha njia panda, nikamuani Mnyika na wiki jana nikamsikiliza Kubenea YouTube akiwahakikishia hawezi kujiunga na watu waliomumwangia Tindikali.

Duh kweli ndo sababu wanaume sasa wanaoa midoli huenda nao wamevurugwa na wanasiasa
 
Wanasiasa sio Miungu watu ni hawa hawa watu tunoishi nao kila siku.

Yaani wewe uyafanyao yanafanania na wayafanyao. Usimwamini mtu mpe asilimia kadhaa za kulifanya jambo ila sio kumwamini kwa kila kitu.
 
Malaika waliowahi kumuona Mungu walishawahi kuasi na wakamgeuka, sembuse wanasiasa wa nchi masikini ??? Nchi huanza kuwa na adabu pale tu ambapo wananchi wanaamua kushika hatamu na kuwafundisha watawala kwamba nchi ni ya nani. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao uko duniani kote na hata Mzee Nyerere aliwahi hata kuusema namnukuu "Nitawaona watanzania kuwa ni wapumbavu sana kama hawataisi Serikali inayotawala kwa maslahi ya familia chache"

Ufaransa, Uingereza, Urusi, Uchina, Japan na kwengineko walipata maendeleo makubwa baada ya kuamua kuwanyang'anya hatma yao watawala wao. Kiufupi mkuu Ng'wanapagi hakuna taifa ambao limewahi kuamka na kukuta mwanasiasa amewewakea mezani mkate, siagi na maziwa. Kama hilo taifa lipo nitajie hapa nilione. Wanasiasa na vyombo vya dola huwa na adabu pale tu wanapojua kwamba nchi siyo mali yao.

Lakini kwa akili za kuwategemea wanasiasa utaendela kuwa masikini sana utaendelea kuvunjika moyo tu.
Chukueni hatua na muamue leo hii........Ngumu kumeza lakini hii ndiyo dawa pekee!
 
Imani imeondoka kabisa. Sasa hakuna siasa kuna maslahi.
Mbaya zaidi hawana uchungu wowote na watu waliowasimamia kupata hayo madaraka na hadi kufikia kununulika. Bora wangekuwa wanawarudishia hata fadhila kidogo wanachama wao waliowafikisha hapo kwa pesa wanayopokea
 
Imani imeondoka kabisa. Sasa hakuna siasa kuna maslahi.
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, watanzania mnategemea sana kufanyiwa vitu na wanasiasa ndiyo maana hamuwezi kufika mbali hata siku moja (Hebu badilisheni haya mawazo ya kizamani)
Tanzania: ujinga, unafiki, uchawi na umbea ndo tunayoyaweza
Msisingizie Uchawi hapa, sisi tumekuwa wajinga sana kujiaminisha kwamba tunaweza kukombolewa na kikundi cha wanasiasa. Hicho kikundi kikiwageuka ndiyo mnaanza kupoteza matumaini kama hivi; hebu jioneni mnavyolalamika utafikiri hao wanasiasa ni miungu wenu.
 
Wanasiasa sio Miungu watu ni hawa hawa watu tunoishi nao kila siku.

Yaani wewe uyafanyao yanafanania na wayafanyao. Usimwamini mtu mpe asilimia kadhaa za kulifanya jambo ila sio kumwamini kwa kila kitu.

Atleast some breath of fresh air,
Hili nimelisema sana wengi huwa hawanielewi,
Waendelee kumsubiria MASIHA atakayekuja kuwaokoa.
 
Na ulivyokuwa mjinga wenzako wanakula ruzuku kwa jina lako halafu wanakwambia mtukane Raisi wetu Magufuli, Halima Mdee umemwona ndani ya Dreamliner yetu? Lkn anakwambia wewe usipande!
 
Maendeleo ya nchi hii hayawezi kuletwa kwa imani za kumwamini kiongozi(kakikundi ka watu) atayaleta. tena ukikafuatilia mienendo yake..unastaajabu

Hili limekuwa linaisumbua jamii yetu ndiyo maana tumekuwa warahisi kwa kuendeshwa na cheap propagandas..

Viongozi washalijua hili wanatupindua pindua kama chipsi kwenye Karai.
 
Lakini ujue kuwa Kenya hata Zimbabwe watatuacha mbali sana. Kinachoendelea huko ni woga wa watawala kuongoza wakiwepo wapinzani. Bila upinzani imara nchi yetu itayumba.
 
Malaika waliowahi kumuona Mungu walishawahi kuasi na wakamgeuka, sembuse wanasiasa wa nchi masikini ??? Nchi huanza kuwa na adabu pale tu ambapo wananchi wanaamua kushika hatamu na kuwafundisha watawala kwamba nchi ni ya nani. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao uko duniani kote na hata Mzee Nyerere aliwahi hata kuusema namnukuu "Nitawaona watanzania kuwa ni wapumbavu sana kama hawataisi Serikali inayotawala kwa maslahi ya familia chache"

Ufaransa, Uingereza, Urusi, Uchina, Japan na kwengineko walipata maendeleo makubwa baada ya kuamua kuwanyang'anya hatma yao watawala wao. Kiufupi mkuu Ng'wanapagi hakuna taifa ambao limewahi kuamka na kukuta mwanasiasa amewewakea mezani mkate, siagi na maziwa. Kama hilo taifa lipo nitajie hapa nilione. Wanasiasa na vyombo vya dola huwa na adabu pale tu wanapojua kwamba nchi siyo mali yao.

Lakini kwa akili za kuwategemea wanasiasa utaendela kuwa masikini sana utaendelea kuvunjika moyo tu.
Chukueni hatua na muamue leo hii........Ngumu kumeza lakini hii ndiyo dawa pekee!
Hapa tuna maswali ya kujiuliza kiongozi.

Ni kwanini Jamii yetu imeshindwa hili?

Je, ni historia ya kisiasa jamii iliyopitia toka tunapata Uhuru au ni mifumo iliyopo!

lakini hii mifumo inawekwa na nani kama sio sisi wananchi kupitia miongoni mwetu tunaowapa mamlaka ya kutuongoza?
 
Na ulivyokuwa mjinga wenzako wanakula ruzuku kwa jina lako halafu wanakwambia mtukane Raisi wetu Magufuli, Halima Mdee umemwona ndani ya Dreamliner yetu? Lkn anakwambia wewe usipande!
Sio ruzuku tu hata huyo Magufuli anakula Ruzuku sema yake imepewa jina lingine.

hapa mada ni kuweka imani kwa kiongozi usilete usiasa usiasa.. Magufuli ni mwanasiasa, lowasa ni mwanasiasa, Mbatia ni mwanasiasa mtoa mada aliyetaka tuwajadili hapa.
 
Maendeleo ya nchi hii hayawezi kuletwa kwa imani za kumwamini kiongozi(kakikundi ka watu) atayaleta. tena ukikafuatilia mienendo yake..unastaajabu

Hili limekuwa linaisumbua jamii yetu ndiyo maana tumekuwa warahisi kwa kuendeshwa na cheap propagandas..

Viongozi washalijua hili wanatupindua pindua kama chipsi kwenye Karai.
Mwanadamu mwenye FREE WILL huwezi kumtegemea wala kumwamini linapokuja swala la maslahi, pesa, madaraka au nguvu. Kanuni ninayoishi nayo mpaka leo ni hii: "Kila mwanasiasa ni adui yangu, na ataacha kuwa adui yangu pale tu ambapo amerudi uraiani kama mimi. Mtu mwenye uwezo wa kutoa uhai wako na kumiliki dola hawezi kuwa rafiki yako hata siku moja"
 
Sio ruzuku tu hata huyo Magufuli anakula Ruzuku sema yake imepewa jina lingine.

hapa mada ni kuweka imani kwa kiongozi usilete usiasa usiasa.. Magufuli ni mwanasiasa, lowasa ni mwanasiasa, Mbatia ni mwanasiasa mtoa mada aliyetaka tuwajadili hapa.

Usimlinganishe Raisi wetu na ujinga!
 
Lakini ujue kuwa Kenya hata Zimbabwe watatuacha mbali sana. Kinachoendelea huko ni woga wa watawala kuongoza wakiwepo wapinzani. Bila upinzani imara nchi yetu itayumba.
Kwangu nchi sio lazima iwe na chama cha upinzani kikubwa chenye nguvu.

ninatoa mifano...kuna nchi hazina mfumo mpana na wenye nguvu wa upinzania lakini ni nchi zilizo piga hatua katika maendeleo ya jamii.

Ng'wanapagi wewe si unaijua Botswana? kuna upinzani wowote wenye nguvu?

kikubwa nchi iwe na wanachi wenye fikra pevu na maono mapana juu ya nchi yao. ikishakuwa hivi hata Mwanasiasa akifanya jambo baya anahofia sauti ya jamii.
 
Na ulivyokuwa mjinga wenzako wanakula ruzuku kwa jina lako halafu wanakwambia mtukane Raisi wetu Magufuli, Halima Mdee umemwona ndani ya Dreamliner yetu? Lkn anakwambia wewe usipande!
Wewe shoger usiniletee ukuku wa CCM na CHADEMA hapa. Nimekuwa mapumziko nyumbani kijijini,nimekuta wananchi wanapeleka mpunga dukani kubadirishana na mafuta ya kula na kupaka sababu ya maisha magumu ambayo hayajawahi kuwepo kabla harafu kenge wachache wanakwambia wanaunga mkono juhudi za mtu kuwapatia maisha bora Watanzania. Nimefika Kakola, nimefika Bugarama nilichokishuhudia ni watu wanajichukulia nyumba bure za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi baada ya kukosa wanunuzi na wakaamua kuondoka kwenda makwao
 
Back
Top Bottom