Wakuu kuna misemo naisikia mara nyingi hususan katika misiba na sielewi hasa maana yake, mwenye uelewa eneo hili naomba anieleweshe. Mfano, mtu anaposema "Tulimpenda zaidi huyu (yaani marehemu) lakini Mungu kampenda zaidi" Hivi Mungu anapenda mauti yatukute wanadamu? Hii kauli huwa inanitatanisha na hasa ninapoambiwa ktk misiba niliyopoteza ndugu zangu.
tukiwa matumboni mwa wazazi wetu, tunaweka ahadi na mungu juu ya vifo vyetu, hivyo tunapokufa ni ahadi tulizoweka zimetimia tu, ndio maana wanasema tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi. na huu ni msemo kuwafariji ndugu wa marehemu.