Mungu kutoa tamko mwakani

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,070
Reaction score
726
Baada ya muda mrefu MUNGU kukaa kimya na kutotoa adhabu kwa watanzania, MUNGU amekusudia kutoa tamko na onyo kali kwa sababu ya upole wa watanzania uliopitiliza. MUNGU anakusudia kutoa tamko na onyo kali kwa wale wote wanaofumbia macho wizi, ufisadi na rushwa iliyokithiri serikalini. Kwa kuanzia ataanza kutoa adhabu kama mfano kwa wakuu wa ofisi za TAKUKURU, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.

Kwa mjibu wa mtoa habari kutoka mbinguni Bwana MUNGU amepanga kuwatwaa baadhi ya viongozi waandamizi wa taaisisi tajwa ili wakasuburi hukumu zao kwaani MUNGU ameona kundelea kuwapo hapa duniani kutaathiri na kuharibu vizazi vijavyo.

Katika orodha hiyo ndefu ya viongozi wanaotakiwa kupumzishwa na MUNGU huku wakisubiri hukumu zao za mwisho kuna majina ya viongozi wa awamu zote nne za uongozi, lakini inasadikika majina yanayongoza ni kutoka katika awamu ya tatu nay a nne. Lakini cha kushangaza katika orodha hiyo Rais wa awamu zote hawamo. Baadhi ya taasisi na wizara ambazo zina majina mengi ni TRA, WIZARA YA MAMBO YA NDANI, MAHAKAMA, NISHATI NA MADINI NA MIUNDO MBINU NA WIZARA YA MALIASILI NA UTARII.

Inasadikika MUNGU hakupenda kabisa kuona maliasili alizozileta kutunzwa zinaharibiwa kwa kiasi hiki viongozi wakiwa watazamaji tu inasadikika MUNGU anakusudia kusimamisha mvua kwa mwaka mzima ili kutoa fundisho.

Pia mtoa taarifa amesema kuwa hajapenda kuona ukimya wa viongozi wa madhebu mbalimbali ya dini bila kukosoa huku orodha ya majina wakiwa nayo muda mrefu. Inasemakana mashekh na maaskofu wanayo orodha hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka 30 sasa.

Hivyo MUNGU atatoa onyo kali kwa watanzania au kutoa adhabu kali iwapo wataendelea kunyamanza kimya bila kufanya maamzi magumu. Ndugu zangua watanzania hasa mashekh na maaskofu, wachungaji na ustaadhi tunawaomba kutoa kauli zenu ili mtuepushe na adhabu ya MUNGU.
 
Duh, hili dua balaa!Watu wanaweza kukimbia makanisani na misikitini kutubu!
 
Mungu atoe tamko kali kwa samuel 6 pia atoe tamko kali kwa washirika wake.
 
Duh, hili dua balaa!Watu wanaweza kukimbia makanisani na misikitini kutubu!

Huko nako mafisadi wanakalishwa front rows na wanaheshimika kuwa ni waumini waaminifu.....!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…