Mungu awabariki wana wa Meru ya Mashariki.

democratic

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
1,642
295
Mmeonyesha kuwa kinyume na nguvu na ghiliba zote za mafisadi wa nchi hii,mmetukumbusha kuwa jukumu la kuilinda hii nchi ni letu sote,mkaendelea kutuonyeha kuwa utawala wa nchi hii uko kwa wananchi wenyewe na sio genge dogo la watu waliokwisha lewa pesa walizowaibia watu maskini na wavuja jasho wa nchi hii.

Wana meru ya mashariki,historia ya nchi hii itawaacha huru siku zote,angalau leo mmewafuta machozi watu wote wanaoonewa na kukandamizwa na utawala huu wa ccm,ninayadedicate haya maamuzi yenu ya leo,kwanza kwa Baba wa taifa hili Mwalimu Julius K.Nyerere ambaye pamoja na juhudi zake zote za kuwafunda viongozi lukuki ndani ya ccm juu ya uzalendo wa taifa hili,wengi leo hii wameyakana mafunzo yake.Ushindi huu uende pia kwa Chacha Wangwe,Regia Mtema na wale wote ambao wametangulia mbele za haki wakiwa wametuachia mapambano haya ya kuleta usawa katika taifa hili.

Mungu awabariki sana my bravos wana meru ya mashariki,sasa mlijenge jimbo lenu chini ya mbunge mliyemchagua nyinyi wenyewe baada ya kuzifumbia macho hila zote za pesa za mafisadi wa nchi hii.Hakika the freedom is coming tomorrow.Viva wana meru ya mashariki,viva Chadema, viva Tanzania.

Akhsanteni sana,
Ni mimi mwanahaki mwenzenu,Nawasalimu.
 
Ukombozi uliokusudiwa na wazee wa kimeru walipomtuma kirilo uno mwaka 1955 kudai ardhi zilizoporwa na walowezi umefika leo. Viva arumeru viva tanzania
 
Back
Top Bottom