Leo ARUSHA imerejea kama zamani ni mvua kubwa ya barafu imenyesha kama zamani Kila kona ni barafu NA mtiririko WA maji NA barafu.
lakini nimehuzunika uzinduzi wetu WA kampeni za CCM zimekwama NA hii mvua
anyway hawa CHADEMA wanatukimbiza huku jamani
Arusha mtapata sana neema sio mvua tu, yule msukule aliyekuwa anawaletea gundu Mkuu wa Mkoa Magesa Mulugo, sorry Mulongo amehamishwa baada kumshindwa kamanda Godbless Lema.
Amepelekwa Mwanza kupambana na Generali Hezekiah Wenje kule Mwanza.
Nasikia juzi ameripoti kwa kuanza na midharau yake alipokuwa anaongea na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na madiwani akaanza kuwakoromea eti atawafukuza kazi watumishi wote akiwemo Mkurugenzi wa Jiji hilo na Mkuu wa Wilaya kisa ujenzi wa maabara haujakamilika!.
Sifa kwa diwani wa Kata ya Mbugani Mhe. Hassan Kijuu aliyesimama na kumtoa nishai kwa kumuuliza amekuja Mwanza na shilingi ngapi kabla ya kuanza vitisho, jamaa akajaa upepo na kuamuru Mheshimiwa Diwani atoke nje ya ukumbi.
Minong'ono kutoka kwa wana Mwanza ni kwamba Mkuu huyo mpya wa Mwanza hatadumu mkoani humo kutokana na dharau zake zilizotukuka, watu wamekasirika sana kuchangia ujenzi wa maabara lakini yeye amefika na kubeza bila kusema Serikali imechangia shilingi ngapi na huko Arusha alikotoka amekamilisha ujenzi huo au analeta uchuro Mwanza?.
Ninamshauri mheshimiwa huyu kama kweli ni jasiri aiombe serikali yake chenji ya fedha za Escrow zisaidie ujenzi wa maabara badala ya kuwa mkali kama mtu aliyechanganyikiwa kisaikolojia!, Hakika mkosi umeingia Mwanza mvua hazitanyesha tena, hongera A Town kwa kuanza kupata neema ya mvua!!