Emoj
JF-Expert Member
- Oct 9, 2015
- 839
- 1,304
Baadhi ya wanaume ni shida tupu yaani unaweza ua mtu hivihivi maana ni afadhali kufungwa jela hata miaka mia kuliko kuvumilia kumuona bado anaishi.
Yamemkuta mdada family friend wetu, huyu dada namfahamu toka tukiwa wadogo kweli ana tabia nzuri mpole na mambo mengi ni msomi na ana kazi yake nzuri tu.
Kwenye mapenzi wakapendana na mkaka dreva tax wakaoana miaka sita sasa na wamejaliwa watoto wawili, baada ya kuoana kwa vile mdada alikuwa na kazi nzuri anafanya airport akamununulia mkaka gari ili aachane na kumfanyia mtu mwingine kazi aendeshe gari lao na pia mdada akafungua grocery msimamizi mkuu mume wake, mwanaume kawa royal maisha mazuri.
Hivi karibuni ndoa yao ikaanza kuyumba ndo bibie kanishirikisha kwamba anahisi mumewe anatoka kimapenzi na house girl wake maana house girl siku hizi hamueshimu kama zamani, mi nikamwambia usiwaze vibaya labda housegirl ana mambo yake tu si unajua tena hawa ni wakuwabembeleza na ukizingatia una mtoto mdogo na akaniambia pia hela ya grocery hajui zinaenda wapi kila akimuuliza mumewe vipi anadai biashara hakuna ila vitu vinaisha, akimuuliza mbona sasa vitu vinapungua na unasema hujauza wakati hapa center nzuri ya biashara anamjibu nimekunywa mimi grocery mwaka tu mtaji mwanaume kaufirisi ikabidi wafunge.
Hee! Jana bibie si kawafumania kweli housegirl na mume, jamani mdada wa watu kachoka ni kulia tu halafu mume wake anamwambia ndo hivyo fanya chochote utachoamua kufanya!Nyumba waliokuwa wanaishi ya kupanga alipangishiwa mdada kazini so wanaishi hapo na mume ili awe karibu na kazi ndo mdada kumwambia mume aondoke atoe kila kilicho chake asepe maana hapo kwake, mume katoa vitu vyake huwezi amini si mwanaume kaondoka na mfanyakazi wakaenda mtaa wa pili kupangisha na mfanyakazi.
Mdada ananiomba ushauri nimesikia kutetemeka haivumiliki kumuacha kuona huyo mwanaume wakiishi pamoja na mfanyakazi wanaume mnataka nini? Kwanini mnasababishia wanawake matatizo jamani tena mama watoto wako hadi kufikia hatua ya kumdharau kiasi cha kutembea na mfanyakazi wa ndani kwake kabisa, si bora basi ungetafuta mwanamke huko nje, hata kama mwanamke ana kosa ila ni vyema angemwambia au basi afadhali mara mia angetoka kutembea na mwanamke mwingine huko nje basi na sio housemaid wake.
Na kwa huyu dada kusema labda mdada kamuachia housegirl amuhudumie mumewe hapana,huyu dada namjua anajituma sana na ni mtu anayepinga sana housegirl kumuhudumia mume.Wanaume nini kinawasumbua? Kwanini kama unajua ukiingia kwenye ndoa huwezi kutulia usiache kabisa kuoa.