Naomba msaada,
Wanaume na kama nakosea mnisamehe, mimi ni mwanamke nimeolewa ila mume wangu ni kama mke wangu yaani mimi ni mume wake, amekuwa na tabia hizi hajishughulishi na familia yake yaani mke na watoto hivyo namlisha namvika namfanyia kila kitu na nisipofanya ana mdomo atanitukana kweli.
Kwa sababu amenifanya kuwa mme wake hawezi kunipiga analalamika hadi analia, yeye anafanya kazi anapata hela ila akipata hela anazitoa zote kanisani sadaka, hana muda hata na tendo la ndoa analala anaomba sebuleni usiku kucha anaomba utajiri.
Wakati huo Mungu akimbariki kampa kitu anaenda kutoa vyote kanisani ananitegemea mimi kwa kila kitu kula, kujenga, kusomesha, majukumu yote ya ndani kinachoniumiza mimi hela anapata, akipata anagawa zote amekuwa na utaratibu wa kutembea hana hata senti tano mifukoni yaani akikapata anakimbia mbio akaitoe akishaitoa ndio anatulia.
Hali hiyo imenifanya nimuone ni mke wangu na sio mme wangu, binafsi tangu amenioa mwaka wa 5 amewahi kunipa matumizi mara 2. Nimechoka sana na hali hii sisi ni wa kristo sio vizuri kuachana tutamkosea Mungu ila natamani nijiachie na kibuzi naogopa kumkosea Mungu.
Naombeni mnishauri jamani niko hoi.