mume na mke

sakapal

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,804
1,424
Je kutokana na uchunguzi wangu niko sawa juu ya hii? naombeni maoni yenu pia,

Mwanaume ambaye yuko insecure juu ya mke wake katika maeneo yote yaani kuanzia kitandani hadi kimaongezi na utashi atakuwa hivi,
-Anamtukana mke wake na kumtamkia maneno ya kumuudhi kwa kosa dogo tuu, kosa lake yeye mwenyewe mwanaume, kosa lililofanyika zamani na kuchukulia ndo ulivo wew mwanamke.
-Hajiamini kama amefanikiwa kuwa na mke mzuri na anammiliki hadi watu wa nje wamwambie, kitu kizuri akiambiwa na mkewe hakikubali hadi aambiwe na mtu wa nje.
-Akifanya kosa na likionekana live-kubambwa au kufumwa akifanya uovu huwa mpole kama choroko na huomba msamaha kama mtoto na kuahidi kutorudia tena na kesho akirudia hilo kosa usithubutu kumkumbusha kwasababu utakula makofi hadi usahau jina lako
-Anatumia kilevi kupata confidense ya kujieleza na anajihisi hasikilizwi na kuishia kutishia nikijua unamahusiano nje utakoma
-Hujibu dry au short kwa story anazopigiwa na mkewe hata za kuchekesha ili kuvunja ukimya na mwisho huyageuza maongezi kuwa ugomvi na mwisho hasira na kurushiana maneno machafu na mwisho kununiana

Wanaume hawa huwa kero kwa wake zao wazuri na mwisho wa yoote mke hutafuta stress release nje itakayo mchekesha, itakayomfanya akijirembe asifiwe umependeza, hata zawadi ya pipi tu hutosha kumteka mwanamke wa namna hii
mwnamke huyu huwa amejeruhiwa tayari na akipata mtu anayemjali kwa kumsikiliza na kuongea na e kwa upole hulala na kuwaza muda wote maongezi mapya na kukunja ndita kwa mume wake.

Angalizo mwanaume wa jinsi hii tunzamke wako akipata wanaomjali nje hatakusikiliza tena na hatakuwa anaogopa kuvunja ndoa.
-Wanawake wengi wa dhahama ya ndoa kama hii hujaribu kwa nguvu zao zote kujenga hiyo ndoa isibomoke pamoja na kero zote wanazopata ila ogopa A FED UP WOMEN!!
 
Kumbe walevi wote huwa hawan confidence.....inawagusa wengi tu, ati eeeh?

sio wote ila baadhi yao hukosa kujiamini hasa kwa wake zao hii ni mbaya sana na inawakosesha amani sana
 
Hivi kwani women hawana Integrity ama ubinaadamu kwamba wasiposifiwa ndani ya ndoa huenda kuundress kwa any man who praises her?

Kwa kweli I hate kupigwa mkwara kwamba nikiharibu kidogo tu mke c wangu.
 
nilifikiri ungeandika za wote wanaume kwa wanawake kumbe umependelea upande mmoja..okaay
 
Ukiona mambo hayo yanaanza kutokea ndani ya nyumba ujue mapenzi yashakufa hapo.. Bora huyo mke achukue chake mapema, kuliko kusubi ageuzwe punching bag.
 
Hivi kwani women hawana Integrity ama ubinaadamu kwamba wasiposifiwa ndani ya ndoa huenda kuundress kwa any man who praises her?

Kwa kweli I hate kupigwa mkwara kwamba nikiharibu kidogo tu mke c wangu.

hehehehee ndo umhandle kwa heshima na taadhima ili usipigwe mkwara..lol!
 
Hivi kwani women hawana Integrity ama ubinaadamu kwamba wasiposifiwa ndani ya ndoa huenda kuundress kwa any man who praises her?

Kwa kweli I hate kupigwa mkwara kwamba nikiharibu kidogo tu mke c wangu.

hii ni nature ya wanawake kama wanavyoeleweka kwamba ni ua au pambo la nyumba shurti kulisifia au kulitambua kama lipo
 
nilifikiri ungeandika za wote wanaume kwa wanawake kumbe umependelea upande mmoja..okaay

kwasababu mm ni mwanamke na nimeziona hasa kwa ukaribu za wanaume zipo ila nimesita kuziweka nikiwapa nafasi wachangiaji waziweke
 
Sijaelewa unaposema 'mwanaume ambaye yuko insecure' unamaanisha nini?..
Ukifunguka kuhusu hilo..pengine itakuwa rahisi kutitirika..
 
Sijaelewa unaposema 'mwanaume ambaye yuko insecure' unamaanisha nini?..
Ukifunguka kuhusu hilo..pengine itakuwa rahisi kutitirika..

namaanisha hajiamini kwenye jambo analofanya au analomiliki....
 
Kama ulimaanisha mwanaume ambaye hajiamini kwa mkewe..mimi nadhani kwanza tungeangalia 'kwanini wanaume wanajenga hiyo 'inferiority complex' kuliko kuangalia matokeo ya hiyo kitu..kwangu mie nadhani cha muhimu kwanza ni kujitahidi kuzuia hiyo inferiority na kujaribu kuizuia..Binafsi naweza kushauri yafuatayo:
1.Jitahidi kumpenda mtu mnaye'fitiana'..kielimu, kiuchumi na kimtazamo.
2.Jitahidini kuheshimiana hata katika mambo yaliyo madogo.
3.Msiishi kwa kuigiza..i.e jamii inanionaje??
 
am telling u nimeiona hii kwa wifi yangu mmoja kwa kaka yangu, yaani bro anamsema vibaya sometimes hata kwenye gari bila hata kusubiri wafike chumbani na kuyaongea after all ni ishu ndogo tuu. One day wifi alisahau kitu home wakaenda wote hadi site kufika kule analaumu wifi akawa mpole akaomba msamaha yaishe ni bahati mbaya jamani alisema hadi ikawa kero, haya sku ingine wifi alikuwa anaendesha akatoka kwenye line kidogo nje ya barabar loh alovosemwa utasema sio mkewe.
mi ninachojua mkiwa wapenz pamoja na hasira kunanjia ya kumkosoa au kumweleza mwenzio kwamba hiki ulichofanya sicho ila kwa style hii hv nnavoseam wameshaachana sku nyingi wifi kala tym yake kaka anahaaha na watoto kulea kakonda ile mbaya ila A FED UP WOMAN IS LIKE A GUN
 
Ndio maana nasema lazima tujifunze kitu hapa..nini kimepelekea bro wako kuwa hivyo???
Kwa sababu yote unayoeleza ni matokeo ya 'inferiority'..je nini tunaeza kufanya ili kuepuka?
Hili ndio nataka tujadili!!
 
sakapal unakunywa soda gani? Oops! Unakunywa kinywaji gani? Ingekuwa mtihani ningekupa "A". Nitafute nitimize ahadi!
 
Last edited by a moderator:
hii ni nature ya wanawake kama wanavyoeleweka kwamba ni ua au pambo la nyumba shurti kulisifia au kulitambua kama lipo

Yeah But the last time I checked a woman is also a human being capable of making intuitive deductions. Ana sehemu kubwa ya kuhakikisha ndoa yake inakuwa ya furaha pia sio kukimbilia uzinzi na kuto'earn' mistakes zake kisha kusingizia hakuwa anasifiwa na mmewe.
 
Ndio maana nasema lazima tujifunze kitu hapa..nini kimepelekea bro wako kuwa hivyo???
Kwa sababu yote unayoeleza ni matokeo ya 'inferiority'..je nini tunaeza kufanya ili kuepuka?
Hili ndio nataka tujadili!!

Mkuu nadhani sakapal hakumalizia vizuri utafiti wake, otherwise angegundua kuwa wanaume wengi wasiojiamini wanasababishiwa na wake/wapenzi wao. Usikute hata bro wake naye alisababishiwa na mkewe!
 
Mwanaume siku zote hapendi kuoneka mwenye makosa au kuonekana yuko chini,hata kama kosa amefanya yeye hutaka kuligeuza na kuwa la mwanamke,lakini ,mengine huchagizwa zaidi na tabia ya mtu binafsi pamoja na mazingira aliyokulia nayo.
 
Wanaume hawa huwa kero kwa wake zao wazuri na mwisho wa yoote mke hutafuta stress release nje itakayo mchekesha, itakayomfanya akijirembe asifiwe umependeza, hata zawadi ya pipi tu hutosha kumteka mwanamke wa namna hii

sakapal naomba kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa hapo kwa red. Manake sinaga mazoea ya kumsifia mwandani wangu. Si kwamba siwezi kufanya hivyo, ila ni kwamba sijuagi mashiko yake, hivyo huwa na-ignore tu!
 
sakapal ungefafanua kwa mfano halisi ingekuwa haki zaidi, ila kwa hivyo ulivoiacha imekaa kiujumla-jumla hivyo hivyo inapoteza uhalisia sababu sio wote wanaokunywa pombe wanafanya hizo tabia za kishamba...

Ila yote kwa yote huyo mwanaume unayemaanisha hajafaulu kwenye mtihani wa The Boss kwa huyo mtu kuitwa Mwanaume.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom