Mume mwenye busara

Mume mwenye busara

Denis1729

Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
36
Reaction score
112
Mwanaume mmoja alimuoa msichana aliyekua ni mrembo kweli, Katika kuishi kwao katika maisha ya ndoa, mwanamke alipatwa na ugonjwa wa ngozi. Taratibu akaanza kupoteza uzuri wake, Ikatokea siku moja mume akasafiri kwenda kufanya kazi sehemu na wakati akirudi akapata ajali mbaya ya gari iliyopelekea awe kipofu.

Hata hivyo maisha yao yaliendelea kama kawaida mume akiwa haoni na mke akiwa na ugonjwa mbaya wa ngozi.

Siku zilizidi kwenda na ule ugonjwa wa ngozi ukazidi kumshambulia vibaya yule mke, ila mumewe aliendelea kumpenda na maisha ya kupendana yalitamalaki ndani ya mji wao. Ilifika siku yule mwanamke alifariki, kifo cha mkewe kilimhuzunisha sana bwana yule. Walifanya mazishi na baada ya mazishi bwana yule akataka kuhama kabisa mji ule.

Ndugu wa bwana yule wakamwambia, umefiwa na mkeo ni nani sasa atakua akikuongoza njia na hali hii wewe huoni? Bwana yule akawajibu, mimi siyo kipofu, muda wote huo nilikuwa nikiigiza, kwa sababu mke wangu angejua nauona ubaya wake uliosababishwa na kuharibika kwa ngozi yake ingemuumiza zaidi na kujiona hana thamani tena kwangu.

Hivyo nilijifanya kipofu ili niitunze furaha yake, alikua ni mke mzuri kweli kwangu.

FUNZO.
Japo kisa hiki ni cha kufikirika (fictional)
ila ni vema tujifunze kwamba bora tujifanye vipofu na kupotezea madhaifu ya wapenzi wetu ili tujenge mahusiano ya furaha. Haijalishi ni mara ngapi meno yanang'ata ulimi wako, ila bado ulimi na meno vipo pamoja mdomoni mwako.

Huo ndiyo moyo wa KUSAMEHE.
Ingawa macho hayaonani ila yote yanaona vitu kwa pamoja, yanafumba na kufumbua pamoja na kulia pamoja. Hiyo ni spirit ya UMOJA. Mungu atujalie tuwe na spirit ya kusamehe na ya Umoja. Peke yangu naweza 'kusema' ila pamoja tunaweza kuongea. Peke yangu naweza kufurahia ila kwa pamoja tunaweza tukasheherekea'
Huo ndiyo uzuri wa mahusiano mema,
sisi si kitu bila ya mmoja wetu. Wembe ni mkali lakini haukati mti, na shoka ina nguvu lakini huwezi kunyolea nywele.

Kila mmoja wetu ni wa muhimu kutokana na upekee wake, acha dharau, muheshimu mtu vyovyote awavyo, Tuvumiliane.
 
kikubwa na kufocus sana kwa mtu hata watu muhimu dunia hii ina mabillion ya watu hata vitu hatuwezi kuridhika kwa kutafuta kizuri zaida ila tunatakiwa kupata kilicho bora kwenu then tuishi nacho na kuvumilia matatizo zote .


ukweli uvumilivu ndo kila kitu kwani ndo maisha halisi
 
Watoto wazuri hadithi hii inatufundisha nini??
 
Back
Top Bottom