Mume kufukuzwa kazi kumenifundisha kuchepuka, sasa nimekuwa sugu

LoraJigger17

Member
Feb 2, 2017
94
78
Bhandugu salaam!

Nina yangu ya moyoni wapendwa wacheni niyatoe nipate kupumua! Mimi nimeolewa tangu mwaka 2008, tuna watoto wawili na mume wangu.

Lakini tangu mwaka jana February mume wangu alipata matatizo kazini kazi ikawa imeisha, na mimi ni mama tu wa nyumbani, huwa saa nyingine nafanya vibiashara vidogo vidogo kwa msimu tena.

Mwezi huu wa February tunatimiza mwaka mume pasipo kuwa na kazi, watoto wanasoma private school sababu alikuwa na kazi nzuri, yuko na elimu nzuri, akipata kazi huwa inakuwa ya maana.

Sasa mwenzenu maisha yalinishinda, ilifikia point mwanaume anashinda ndani tu hatuna chochote cha kula na watoto, nikaona hakuna namna wacha niokoe jahazi kama mama. Kuna jamaa alikua ananimendea tangu kitambo sana nilikua sina mpango sababu mume alikua akinipa kila nilichotaka.

Sasa kwa wakati huu na shida hizi ikabidi nimkubalie. Tukaenda mji wa mbali tukapima afya, tukazindua mahusiano, mapenzi yakaanza pole pole, jamaani mpaka sasa tuna miezi nane katika kuchepuka (nae ana mke na watoto wawili).

Naomba niseme hivi; NILICHELEWA KUCHEPUKA NA HUYU BWANA, maana mambo anayonipa sijawahi kupata. Mpaka sasa yeye ndio kanipa pesa nimelipa kodi ya nyumba, kanipa ada za wanangu, ananipa matumizi ya nyumbani, maisha safi, stress zote kwiiishhhhaaaa niko na tabasamu masaa yote.

Tumesisitizana kila mmoja aheshimu ndoa yake, nimemsisitiza sana asibadili mwenendo wake mbele ya mke wake na familia yake. Nami nimejiapiza kumuheshimu mume wangu mpaka mwisho, tunafanya kwa usiri mkubwa sana lakini kila mmoja wetu anapata raha ile mbaya.

Akinipa appointment sifanyagi ajizi, sibakishi kitu, nampa hasa hadi inapata moto, nikirudi home kimyaa! Sasa huyu mume wangu anachonishangaza ni kwamba akitaka kutoka ananiomba nauli, nami nampa yoyote nilonayo, misosi napika tunakula, watoto wameenda shule kama kawaida, hata hajashangaa wala haulizi hela natoa wapi wala nini, hapo ndio simuelewi!

Eti jamani nisaidieni atakuwa anawaza nini?
 
Kwa hiyo unatuaminisha mwanamke ameumbwa hawezi kufanya kazi za kuzalisha tofauti na kuugawa mwili wake eeh! !?

Umenipa maswali mengi saana wewe mama. Pole wanao. Kuna wanawake single mom's hawajawahi kugawa uroda kama kitega uchumi na familia zao zinasoma na zinakula vizuri
 
Umetumia njia ya SHETANI kujikimu kimaisha,hata uhangaike vipi MUNGU asingekuacheni,tena pale unapofikia kuchoka kabisa ndo wakati wa MUNGU kukupa faraja,ulipochoka hukupiga moyo konde ili muumba akunasueni,sikuombei mabaya ila nasikitika kukuweka wazi kwamba,SHETANI atakuvuruga kiasi ambacho hutaacha kuona kila aina ya rangi za hukumu.ni swala la muda tu.
 
Bhandugu Salaam!!
Nina yangu ya moyoni wapendwa wacheni niyatoe nipate kupumua!
Mimi nimeolewa tangu mwaka 2008, tuna watoto wawili na mume wangu.

Lakini tangu mwaka jana February mume wangu alipata matatizo kazini kazi ikawa imeisha, na mie ni mama tu wa nyumbani, huwa saa nyingine nafanya vibiashara vidogo vidogo kwa msimu tena. Mwezi huu wa February tunatimiza mwaka pasi mume kuwa na kazi, watoto wanasoma private school sababu alikuwa na kazi nzuri, yuko na elimu nzuri, akipata kazi huwa inakuwa ya maana.

Sasa mwenzenu maisha yalinishinda, ilifikia point mwanaume anashinda ndani tu hatuna chochote cha kula na watoto, nikaona hakuna namna wacha niokoe jahazi kama mama. Kuna jamaa alikua ananimendea tangu kitambo sana nilikua sina mpango sababu mume alikua akinipa kila nilichotaka.

Sasa kwa wakati huu na shida hizi ikabidi nimkubalie. Tukaenda mji wa mbali tukapima afya, tukazindua mahusiano, mapenzi yakaanza pole pole, jamaani mpaka sasa tuna miezi nane ktk kuchepuka (nae ana mke na watoto wawili).

Naomba niseme hivi; NILICHELEWA KUCHEPUKA NA HUYU BWANA, maana mambo anayonipa sijawahi kupata!
Mpaka sasa yeye ndio kanipa pesa nimelipa kodi ya nyumba, kanipa ada za wanangu, ananipa matumizi ya nyumbani, maisha saafii...stress zote kwiiishhhhaaaa niko na tabasamu masaa yote.

Tumesisitizana kila mmoja aheshimu ndoa yake, nimemsisitiza sana asibadili mwenendo wake mbele ya mke wake na familia yake. Nami nimejiapiza kumuheshimu mume wangu mpaka mwisho, tunafanya kwa usiri mkubwa sana lakini kila mmoja wetu anapata raha ile mbaya!

Akinipa appointment sifanyagi ajizi, sibakishi kitu, nampa hasa hadi inapata moto, nikirudi home kimyaa! Sasa huyu mume wangu anachonishangaza ni kwamba akitaka kutoka ananiomba nauli, nami nampa yoyote nilonayo, misosi napika tunakula, watoto wameenda shule kama kawaida, hata hajashangaa wala haulizi hela natoa wapi wala nini, hapo ndio simuelewi! Eti jamani nisaidieni atakuwa anawaza nini?!!

Na yy very soon atakutana na boss ambae alikuwa anampenda siku nyingi, na atampa kazi mzuri na yy atakuwa anachepuka kama ww
 
Dunia hii...Dunia hii.

Kutokana na hali ya maisha ukaamua kumsaliti Mumeo kwa Makusudi na kuhalalisha ZINAA.

Na kwajinsi unavyomsifia huyo unayezini naye na kumwona bora kuliko mumeo ni wazi kabisa wewe ni Muhuni mzoefu.

Ipo siku Mungu atamuinua tena mumeo kiuchumi sana na si bure akayajua hayo yote unayomfanyia, atakuacha yeye na mchepuko ukakuacha pia.

Utakuja kuwakosa wote.

Acha hiyo dhambi unayoifanya dada yangu.

Usijisifie Usaliti na Uzinzi.
 
Ana elimu nzuri na alikua na kazi nzuri???
Watoto wanasoma private schools??? Hayo yote yananipa picha kua alikua na salary nzuri pia. Swali n kwamba hakua na miradi mingne ya kumuuingizia kipato inje ya salary????

ANYWAYS.....Kuna uwezakano mkubwa kua anafaham vyote vinavyoendelea hapo, na ndo maana kaamua kukaa kimya coz hana chakufanya kwa ss. Lkn mambo yake yakishakua mazur tena ujue yako ww yatakua juu ta mawe..kua makini!
 
Back
Top Bottom