NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,023
- 2,492
Naamini hamjambo.
Wale tusiopenda habari ndefu tuendelee na mambo mengine kwani karama ya kufupisha haijanipitia bado ila naitaka.
Leo nilikuwa nikiperuzi gazeti la kila siku la THE CITIZEN linaloandikwa kwa kingereza. Kichwa kimoja cha habari na picha yake vikanivuta. Ilikuwa ni picha ina mwanamke mrembo aliyevalia suti na nyuma yake kulikuwa na wanaume kadhaa wakimuangalia. Kichwa cha habari kilisema "My life as a male escort". kwa kuangalia picha na neno escort ninalolijua mimi kutokana na "umilisi" mdogo wa kingereza nikafikiri ni habari ya wanawake na wanaume katika siasa.
Nilipoanza kuisoma nikagundua nilikuwa nimepotea kabisa. Makala ilimuhusu kijana Andrew aliyekuja jijini dar miaka 6 iliyopita kutafuta maisha baada ya kuacha shule na kwenda kusaka madini mererani kwa miaka miwili bila mafanikio na kisha kuamua kuja Dar es salaam.
Alipofika Dar es salaam alishauriwa na mwenyeji wake ajiingize kwenye biashara ya kupaka wanawake rangi eneo la mwenge kwani ingeweza kumsaidia kupata mtaji wa biashara kwa haraka. Alikubali kazi hiyo kwa shingo upande, na akaanza mafunzo ambapo alimudu vizuri. Alishauriwa namna ya kujiweka vizuri kimuonekano na kumasaji miguu vizuri kwa uangalifu ili kuvutia wateja na kufurahisha wateja.
Muda si muda akajikuta katika wakati mgumu. Baadhi ya wateja wake walianza kumtongoza na kuahidiwa fedha. Mwanzoni alipata shida lakini alipofikiria mahitaji mengi ya maisha ya kila siku aliamua kukubali akajiingiza rasmi katika shughuli ya kuwauzia wanawake ngono.
Huduma yake ya ngono ilikuwa kwa haraka kwani alikuwa akipata "oda" nyingi toka kwa wateja wapya na wa zamani. Mambo yalikuwa mazuri zaidi pale huduma yake na namba yake ya simu ilipowekwa kwenye blogu ya wakubwa ambayo jina lake halikutajwa.
Biashara hiyo ilimpatia fedha nyingi na ameweza kufungua maduka mawili ya viatu, moja dar na moja arusha. Kumiliki kwake maduka haya mawili kumeamsha hamu yake ya kuwa na hela zaidi kwa hiyo hutumia fursa ya kuwa na maduka hayo ya viatu pamoja na vitu vingine kupata wanawake "wanawake wanapokuja hapa huwa nafanya juu chini kuwavutia kwa kuoneka mtanashati na mwenye kujiamini. Hivi vinawavutia na kufanya iwe rahisi kuwafanya wawe wateja wangu wa huduma nyingine - ya ngono.
Alivyoanza
Anakumbuka mteja wake mmoja alikuwa akimdadisi sana kuhusu maisha yake. Huyu mteja alifanikiwa kumfanya rafiki na wakapeana namba za simu na kuna wakati mteja alikuwa akimpgia na kumtaka akamfanyie huduma ya pedikyua nyumbani. Mara mteja akaanza kumlipa zaidi ya ujira wake.
Badala ya 10,000 akawa anampa 30,000. Siku moja yule mteja akaamua kufunguka na kumwambia kuwa anampenda na kuwa mumewe hamridhishi kwani yuko busy na biashara. Andrew akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake ambapo alishauriwa akubali. akakubali na siku ya kwanza alipewa 150,000. Andrew anasema wakati ule ilikuwa ni hela nyingi sana. Mimi naoina hata sasa ni hela nyingi, kwa hiyo labda sasa hivi anapata nyingi zaidi.
Kwa nini wanawake huchepuka?
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa wanawake walioolewa wanaotumia mtandao wa mahusiano wa AshleyMadison ambao hulenga wanandoa wanaotaka kuchepuka, wanawake wanaochepuka si tu wale wenye matatizo kwenye ndoa zao. Wengi husingizia matatizo ya ndoa wakishagundulika. Nisiongelee sana hili. Tuendelee na ujasiriamali wa Andrew.
Andrew ambaye ameoa anasema kazi si rahisi. Alikutana na mkewe miaka miwili kabla ya kuamua kuanza ujasiriamali wa ngono. Mara nyingi tu hulazimika kusema uongo kwa mkewe hasa pale anapopata wateja wa nje ya dar au wale wa dar wanapomtaka wakafanyie mbali na dar. Anashukuru kuwa na duka arusha kwani humrahisishia kumdanganya mkewe na mkewe humpa baraka zote kwani anajua umuhimu wa biashara yao ya viatu.
Alipoulizwa anafanyaje pale moyo wa mteja unapomdondokea Andrew alisema ni ngumu sana kwani hujikuta akilazimika kuvunja mawasiliano na wateja wa aina hiyo, hali ambayo huathiri biashara kwa kiasi fulani. "Mimi ni mwanandoa na ninampenda mke wangu.
Najua ni vigumu kujihusisha na mwanamke mwingine bila kuwa na hisia juu yake lakini nimejifunza kushughulikia changamoto zinazoendana na hali kama hiyo. Kwa mujibu wa Andrew kuna vijana wengi tu ambao hutoa huduma kama yake kwa siri sana huku wakiendesha maisha yao mengine kama kawaida.
Wateja wengi wa Andrew ni wanawake wanandoa wenye kipato kikubwa wenye umri wa miaka 30-40 na wanawake wa umri huo huo ambao hawajaolewa na hawapendi mahusiano ya kudumu. Andrew anaongeza kuwa usiri ni jambo la muhimu kuliko yote katika biashara hii.
Tofauti na biashara ya ngono inayofanywa na wanawake, ufanisi katika biashara hii kwa wanaume hautegemei tu uwezo wa "kupiga sarakasi" bali uwezo wa kusikiliza na kuonyesha mahaba. "wanawake hawapendi ngono tu bali pia na mazungumzo", hivyo unahitajika uwezo wa kusikiliza hadithi zao na kuzielewa ili kuweza kujua mahitaji yake.
Source: THE CITIZENS
Inawezekana hakuna jipya ila ndo hivyo, mimi nimepigwa na butwaa, na bado nina mshangao ndo maana nikajikuta naandika hapa.