Mulugo atoa rushwa kampeni za uchaguzi mufindi

Mulugo atoa rushwa kampeni za uchaguzi mufindi

JUSTIN MPOTWA

Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
16
Reaction score
11
Katika kile kinachoonyesha uwezo mdogo katika ufanyaji wa kampeni na ukosefu wa utashi wa kisheria kwa baadhi ya watendaji wa serikali ya CCM, Mhe. Philip Mulugo, Naibu waziri wa elimu na Mafunzo amekiuka kanuni za maadili ya uchaguzi kwa kutoa rushwa hadharani katika kampeni za udiwani zinazoendelea hapa wilayani Mufindi.

Mulugo alifanya hayo katika Kata ya Mbalamaziwa iliyopo wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, pale alipokuta Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiwa kinafanya kampeni zake katika kijiji cha Mbalamaziwa. Mulugo alikuwa akielekea Mbeya, ambapo akiwa anapita kijijini hapo aliamua kushuka na kuungana na wanaccm waliokuwa wanafanya kampeni.

Mulugo, badala ya kuongelea mambo mbalimbali yanayohusu elimu ambayo nidyo ya muhimu zaidi kwa wakati huu, alijikita katika kumnadi mgombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) bwana Zuberi Nyomolelo ambapo alitoa ahadi kwa wasikilizaji (wananchi), kuwa endapo watamchagua mgombea kupitia tiketi ya CCM, atawapa mifuko ishirini (20) ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari.

Aliahidi kufanya hivyo siku ya kuapishwa mgombea na mifuko hiyo ataikabizi kwa mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini, mhe. Kigola. Kwa mujibu wa sheria ya maadili ya uchaguzi, inasema, hakuna mtu yeyote, kiongozi wa umma anayetakiwa kutoa ahadi yeyote kwa niaba ya mgombea wa chama chochote.

Katika hatua nyingine ya kushangaza zaidi, Mulugo, alitenda kosa jingine kwa kutoa rushwa hadharani fedha taslimu Tsh. 40,000/= kwa timu ya mpira ya kijiji na kuwasisitiza kuwa waichague CCM. Alitoa fedha hiyo akiionyesha hadharani mafungu ya elfu kumi kumi. Hii ni kinyume cha sheria ya maadili ya uchaguzi.

Swali kwa watanzania wapenda Demokrasia na Maendeleo, Je, Kama viongozi wa kiserikali aina ya Mulugo wataendelea kutumia rasilimali za walipa kodi ambao wengi wao ni maskini, je nchi hii tunaipeleka wapi?
 
mbona yupo bungeni hii habari yako ya lini?
waoneeni huruma ccm wapo na hali mbaya kwa kweli
 
Back
Top Bottom