Hapana, multpartism iko sehemu nyingi na pia colonialism, sio kwamba ilitokea Africa peke, tusichukulie vitabia vya viongozi wetu wa kiafrica amboa ni selfishness, uchu wa madaraka, ukatili, ukabila, unafiki, uroho mbaya ziwe visingizio ku chukia wazungu na mulitpartism, Malaysia Indonesia India Singapore S.Korea wana mulitpartism mbona wanaeendelea vizuri......tatizo la Africa wrong selection of our leaders. Tunapendelea tu watoto wa maskini with poor economic and political background...... Wana lack international exposure to see how democracy oparates in other developed countries imagine you have atop leader who can't admire even to go abroad to emulate and learn leadership skills, anaona kutumia million10 ninyingi bcz ov poverty background at home.
Kweli kabisa wazungu wanasingiziwa mengi ili madhalimu waendelee kufanya udhalimu.
Kabla ya Wazungu kuja Wangoni hawakuweza hata kuoana na Wamatumbi.
Wachaga wa Kibosho hawakuweza hata kujenga nyumba yenye mlango eneo la Wachaga wa Machame.
Kabla ya Kuja hao wanaosema kwamba wametugawa ili watutawale Haikuwa rahisi Chifu wa Wazanaki kutawala Makabila 125 yaliyopo Eneo lenye ukubwa wa Tanganyika au Tanzania.
Hizi zilikua in kauli na propaganda za wapigania Uhuru ili kuwaunganisha waafrika kudai Uhuru lakini Afrika iligawanywa na wakoloni ili wao wenyewe wasiingie kwenye vita ya kuvamia makoloni na kuingia kwenye migogoro. Ni busara na maarifa yao yaliwapelekea kuligawa bara la Afrika.
Watu wenye akili wakiokota pesa njiani wanagombana kidogo na kisha wanakaa na kuona namna bora ya kugawana.
Lakini wapumbavu wanapookota pesa njiani wanagombana mpaka wanaichana chana.
Wanaotetea mfumo wa chama kimoja watuambie kwamba waliupata wapi huo mfumo kama sio kwenye vitabu na mawazo ya hao hao wazungu. Na ukweli ni kwamba vyama vile vilivyokua na uchungu kamili na Uhuru ,utu na haki ya mwafrika havikupewa nafasi kabisa wakati wa mkoloni na viongozi wake wengi walinyongwa.
Wazungu wameleta vitu vingi vizuri ila wajinga ndio wanaovitumia vibaya kwa tamaa zao.
Hivi kwa akili ya kawaida Makabila 125 na dini zaidi ya tano tofauti utawapaje mfalme wa kudumu toka ukoo mmoja kama sio kutaka kuigawa nchi vipande vipande na kupata vinchi 125.
Ulaya ina vinchi vidogo kama vitongoji kwa sababu kila koo na kabila lilitaka kujitawala na kupinga kutawaliwa na ufalme mwingine kwa mabavu.
Wakajifunza kuwa suluhisho la kujenga umoja na kuaminiana ni Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi.
Hata ukiangalia Marekani bila kuwa na demokrasia pangekua na vurugu kubwa sana mana Viongozi wangepatikana kibabe na wengi wao wangetokea kwa wale wenye asili ya Uingereza . Sasa je ,black American wangekua watazamaji tu au wangeamua kutafuta jimbo lao na kujitenga?
America imekua moja kwa sababu ya Demokrasia .
Afrika haiwezi kuungana kwa sababu ya Fikra nyingi za watawala ni za kidikteta kwa hiyo kila mmoja anauchu wa madaraka.
Matokeo yake wanarushia lawama nchi za magharibi.
Leo hii Afrika ingekua ni Taifa moja lenye nguvu endapo tungekua na mfumo wa kweli wa kidemokrasia mana kila mtu angekua anaamini katika haki na usawa na Uhuru .
Watawala wangekua wanajishusha na kukubali kuwa watumishi wa watu. Lakini Figisu kwenye chaguzi zinapelekea waafrika watumie nguvu kuzuia wenzao kugombea na wakigombea wanaporwa ushindi na sasa tunaona waafrika kwa waafrika wanatumia nguvu kubwa kuwazuia waafrika wenzao hata kugombea nafasi za uongozi wa chini kama udiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Hapa utamlaumu vipi Mzungu? Yani Ndugu yako unamzuia kukaa mezani na kula chakula halafu we we unayefanya dhulma unamsingizia jirani.
Kama kweli Afrika tunapenda mfumo wa kiimla wa chama kimoja basi tuwaelimishe wananchi waelewe uzuri na ubaya wa chama kimoja kisha tuwape nafasi ya kutoa maoni yao juu ya kufuta vyama vingi ili tutawaliwe na chama kimoja. Hakika kwa kiwango cha uelewa wa Waafrika kilipofikia kwa sasa hakuna MTU anayependa mfumo wa chama kimoja kwa hiyari labda kwa kutumia nguvu kubwa ya kuwamaliza wale wanaotaka Mfumo wa vyama vingi unaotoa fursa ya kuibua vipaji na watawala wenye ushawishi zaidi kuongoza.
Wale Leo wanaopenda chama kimoja ni kwa sababu tu chama chao kinatawala lakini kikitoka madarakani hata kesho hao hao hawataki kusikia habari ya mfumo wa chama kimoja . Hapo ndipo utagundua kuwa hakuna binadamu anayependa mfumo wa chama kimoja na tabia zake za kikaburu.