Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA)

Ndio maana Tundu Lisu kasema tujitoe huko kwanza,ndio tuanze "harakati" za kudai "mapanki" yetu ya dhahabu.Kama hatutakuwa tumejitoa,basi hao "mababeru" lazima watuadabishe,sbb tutakuwa tumevunja mikataba ambayo sisi wenyewe,kwa utashi na akili zetu timamu,tuliikubali na kuanguka saini.

Tukishamaliza huko,tuje tujitoe kwenye hizi "Bilateral Treaties" ambazo tuliingia kwa "mbwembwe" na USA,Canada na UK.Tukimaliza hapo,tuje kwenye bunge letu na tupeleke mswaada kwa hati ya dharura ili kufanya marekesbisho ya sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997 na sheria ya Misamaha ya Kodi za madini ya 1998 na ile Sheria ya Madini ya 2010 iliyoletwa Bungeni sbb ya "Buzwagi Saga-2007"

Vinginevyo,tutabaki kupiga kelele na kujazana upepo tu.
 
barafu Umeongea yote kwa Ufupi kabisa.

Acha wengine waendelee kushabikia sifa za "kisanii". Tunahangaikia tulipoangukia instead ya tulipojikwalia. (Kwenye Sheria zetu na Mikataba ya 4%) hii Sanaa ya " mchanga" ni sehemu ndogo mno ya ujambazi unaofanyika katika sekta za nishati, Madini na gase. (Wabunge wakutoka vyama mbadala wamelipigia kelele sana jambo hilo).
 
Yaani mikataba hii ingesainiwa kipindi cha mwinyi au kikwete sijui waislam tungezificha wapi sura zetu kwenye mfungo huu..haya sasa imesainiwa 1998 na mtakatifu akiwa hai..tumebaki kulalamikia na kuugulia tumboni!..
 
Hizi mali hata zikiachwa sisi tutazipeleka wapi? Mikataba ilisainiwa Mwl Nyerere akiwa hai.
Sasa kama ni hivyo kwa nini wapinzani amekuwa mkiilalamikia? Magufuli amejaribu tayari mmeanza kumchamba
 
Kwanza kabisa msitegemee muwekezaji yoyote kujakuwekeza iwapo tutajitoa MIGA.Kila muwekezaji anataka awe na uhakika fedha anazowekeza hasa kwenye hizi nchi za dunia ya tatu zinakuwa salama
MIGA siyo tatizo, watu wanapotosha tu.MIGA wanachoangalia ni makubaliano yenu na muwekezaji yamefuatwa ama hayakufuatwa.MIGA hawakutuambia tufute kodi zote kwa wawekezaji wa migodi na tuchukue 4% tu kwenye mirabaha,hayo wangeulizwa wale wabunge wapiga meza waliwaza nini kupitisha sheria hiyo.
 
MIGA na ICSID wote ni watoto wa World Bank ;

Amendment ya PPP act imefanikisha kujiondoa kwenye hicho kitanzi ; wapinzani wanasema tutapoteza investors.

Lisu alipokuwa anatuambia tujitoe MIGA na wapinzani wakashangilia ndio tulikua tuongeze Investor's?

Upinzani wa ajabu sana huu.
 
Lissu alimanisha kwakuwa mmeamua kutumia ubabe basi mijitoe kwanza vinginevyo mtashitakiwa.

Swali:
Sio nyinyi mliombeza na kumuita msaliti?

Leo hatujashitakiwa?

Hamna akili nyinyi watu.
 
Sasa mkuu anatakiwa ashughulikie jambo hili kwa akili zaidi. Dalili zinaonyesha maamuzi ya rsisi hayakuongozwa na ushauri wa wataalamu! Very sad!
Kwani Lissu si mtaalam? Shida ni siasa nyepesi zinazofanywa awamu hii huku zikiongozwa na uchu wa madaraka wa kiwango cha lami
 
Lissu alimanisha kwakuwa mmeamua kutumia ubabe basi mijitoe kwanza vinginevyo mtashitakiwa.

Swali:
Sio nyinyi mliombeza na kumuita msaliti?

Leo hatujashitakiwa?

Hamna akili nyinyi watu.
Kinachozungumzwa hapa ni hasara za kujiondoa ICSID ambayo inafanana na MIGA ambayo mlipendekeza tujitoe.

Kubadili msimamo kwa Upinzani ni jambo la kawaida.
 
Back
Top Bottom