Kibona
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 1,023
- 652
Serikali ya marekani na raia wa marekani ni vitu viwili tofauti, inapokuja kwenye maswala ya nchi hakuna mambo ya utu bali ni maslahi tuu
Pamoja na marekani kuwa na maslahi binafsi, lakini hata ile democratic stability waliyonayo ukilinganisha na China, ni bora Marekani maamuzi yako decentralized kidogo walau kuna usalama. Lakini China siyo nchi ya kupewa nafasi kabisa maana kitakachotokea duniani Mungu peke yake ndo anajua.
Kwanza tutarajie tu kuwa china itasambaratika siku yoyote ile maana inakwenda against nature haiamini katika uhuru wa kutoa maoni, haiamini katika haki za binadamu, pamoja na mafanikio makubwa ya kiuchumi lakini wachina wengi hawajui kinachoendelea duniani. Serikali imedhibiti habari za nje, ni CCTV 9 tu inayotoa habari ambazo pamoja na kuchujwa sana lakini walau zina sura ya kimataifa hata hivyo wachina hawatumii CCTV 9 kwa sababu karibu 95% ya wachina hawajui kiingereza. Chanel zingine zaidi ya 30 ambazo nazo ziko chini ya CCTV zinatangaza kwa kichina lakini hizo ukiziangalia hata kama hujui kichina utagundua kuwa zimekaa kipropaganda kama ilivyokuwa kwa vyombo vya habari enzi za Nyerere. Ni kuwasifu viongozi wa kisiasa, na kuonesha jinsi china ilivyoonewa na mataifa makubwa, hata mgogoro wa tibet watu nje ya china wana habari nyingi sahihi kuliko wachina wenyewe.
Kwahiyo kinachotokea Arabuni sasa kitatokea china pia japo sio siku za karibuni. Itachukua mda mrefu wachina kutambua haki zao lakini siku wakitambua basi yanayotokea Arabuni yatatokea. Na yakitokea basi Marekani ikae sawa kwasababu kama Marekani itaanza kurusha mpira kama inavyorusha huko Syria, Yemen na Bahrain kwasababu za kimaslahi basi mauaji yatakayotokea hayajapata kutokea maana ile sio serikali.
Sasa nchi kama hiyo haiwezi kuvaa viatu vya Marekani duniani labda kama tunataniana. Tunaweza kuwa tunachukizwa na jinsi ambavyo Marekani inashughulikia baadhi ya matatizo kwa kuzingatia maslahi zaidi. Lakini dunia kuongozwa na Marekani ya sasa ni salama zaidi kuliko kuongozwa na china ya sasa, labda china ifanye mabadiliko makubwa ya kiuongozi.