Mukwala Vs Ateba

Mukwala Vs Ateba

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
773
Reaction score
2,587
Kuna hawa strikers wa Simba , Simba Ina mastriker watatu ambao kwenye pecking order ateba ni namba moja , mukwala Namba mbili na mashaka namba tatu, kwa upande wangu sijawahi muelewa kabisa ateba , nafasi anazopata na kuzibadili kuwa magoli naona haviendani kabisa, pia uwezo wa kusimama kwenye nafasi haifurahishi , tofauti na mukwala anapata game chache na nafasi chache lakin anafunga na hata uwezo wake wa kukaa kwenye nafasi ni mkubwa sana kiasi kwamba namini Simba wangepata winga na viungo wazuri angetisha, wewe kwako yupi Bora hata yanga ruksa kusema chochote hata matusi sawa tu
 
Wote wawilu, hawana ubora wa kucheza timu kubwa kama simba, japo kwangu mukwala ni bora zaidi, ila anapaswa aboreshe kiwango, kuwa na ubora kucheza simba
 
Kwanini Mukwala alikuwa anapata game chache na dkk chache?
 
Mukwala alikuwa na goli nne. Akatuliaaa akajafunga la tano muhimu vs Mashujaa dkk za jioni sana. Akatuliaaa akaja akampiga hattrick vs Coastal union yakawa Nane. Ndio watu wakatoka msituni kuwa Mukwala noma KWA Ateba. Ingawaje wote huwezi kuwategemea kufanya makubwa ila Magoli ya chapu ya Mukwala yametoa watu msituni na yamewababaisha
 
Mukwala vs Ateba ni sawa na Kagere vs Bocco.

Kagere alikua ni mtu wa kutumia nafasi chache kama Mukwala kufunga goli ila Bocco hadi akose nafasi 3 au 4 ndiyo afunge kama Ateba
 
Wote wana mapungufu makubwa. Binafsi Ateba ni mzuri kwa fitness, kuweza kuhold mali nk ila mzito kufanya maamuzi. Mukwala hatulii eneo lake stahiki, anazurura sana to the extent kuna timu mpira unafika eneo lake yeye kama central striker yeye hayupo eneo hilo wakati huo, pia ana papara mno.
Simba inabidi watulie sana kwenye selection ya nani wa kubaki msimu ujao otherwise yatakuwa yale ya Baleke, Phiri kuondoka wakati mmoja
 
Simba inabidi watulie sana kwenye selection ya nani wa kubaki msimu ujao otherwise yatakuwa yale ya Baleke, Phiri kuondoka wakati mmoja
Hii hoja umetisha Sana.

Tatizo Simba ni kujazana upepo, Mugalu ilikuwa hivi hivi kisha ikaja ya Moses Phiri na Jean Baleke.

Waamue kubaki na anayefundishika.
 
Game ya AL MASRY , huwezi sana mlaamu ATEBA.. angalia ni clear pass alipewa...,,,,,?
labda cha kulaumu ni kutofanyika kwa tactics sub mapema ....
Kocha unapoona PLAN A inafeli , gundua tatizo haraka ..kama mpinzani ameshambana KIBU D + ATEBA , change formation and style....
Mwite MPANZU elekeza cha kufanya
 
Alichofanya Jana ateba ni kile kile kitu kuwa huyu hatufai , anapoteza sana nafasi anakera
Uchawi upo. Unamuona mtu hata kukuambia hawezi amenenepa na ana kitambi, Bado unamchezezsha dakika 80, ambaye Yuko fiti unamchezezsha dakika 10. Ni mjinga tu ambaye hataamin kua huu sio uchawi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom