Naomba niulize kati ya Katibu Mkuu na Mwenyekiti nani mwenye cheo kikubwa?
Mwenyekiti anawakumbatia hao mafisadi, yeye Katibu mkuu atafanya nini?
Mimi binafsi naona hizi ni kauli za CCM za mfa maji.
Tunataka kuona Mwenyekiti akiwa clean bila biasness yoyote halafu asafishe nyumba yake.
Ni Mwenyekiti tu ndiye anayeweza kupunguza utitiri wa viongozi mafisadi ndani ya CCM.
Halafu hao wanaotajwa mafisadi mbona wote wameshinda kwa kishindo katika majimbo yao ya uchaguzi isipokuwa Mramba ambaye aliwatukana Warombo?
Ni vizuri kujua kuwa Watanzania siku hizi wanaangalia utendaji kazi wa mwakilishi wao bungeni na nche ya bunge!!!