GE2025 Muinja Maingu: Nimeridhika Na Uteuzi, Nitabaki CCM

GE2025 Muinja Maingu: Nimeridhika Na Uteuzi, Nitabaki CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
654
Reaction score
1,598
Mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Muinja Maingu, amesema ameridhishwa na mchakato wa uteuzi uliofanywa na chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, akibainisha kuwa ataendelea kubaki ndani ya CCM na kuunga mkono maamuzi ya chama.
WhatsApp Image 2025-07-29 at 20.13.08_78f25e13.jpg
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa orodha ya walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali, Muinja amesema kuwa ingawa hakuwa miongoni mwa waliopitishwa, anaamini mchakato huo ulikuwa wa haki na wa wazi.

“Nimeridhika na mchakato wa uteuzi. CCM ni chama changu na nitabaki ndani ya chama kuendelea kukitumikia kwa nafasi yoyote nitakayopangiwa. Maamuzi ya chama nayaheshimu,” alisema @maingu7.

Ameongeza kuwa mshikamano, uvumilivu na utii kwa maamuzi ya chama ni misingi muhimu kwa kila mwanachama wa kweli, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Chanzo: Matukio
 
Back
Top Bottom