Muhongo: Kwa hili kazi ipo.

Ichobela

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
326
156
Jana niliangalia kipindi cha dk 45 ITV,alikuwepo waziri wa nishati mh. Muhongo,kikubwa nilichomfurahia huyu bwana ni kwamba yeye si mwana siasa bali ni mtendaji. Alituhakikishia hakuna mgao wa umeme na kitakwimu km alivyotoa ni kwamba matumizi yetu ni wastan wa Megawati 831 na wana uwezo wa kuzalisha 1400. Maajabu eneo letu la Nyegezi line inayoanzia Nyegezi jeshini kuelekea Buhongwa,kila siku umeme unakatika usiku. Nachelea kusema ni mgao natamani kusema ni aidha hujuma au mambo ya kisiasa. Waziri hebu ufanye kufuatilia,waziri alisema km umeme umekatika ni jukumu la meneja wa sehem husika kuwataarifu wananchi kupitia media. Binafsi sijawahi kusikia taarifa toka kwa meneja TANESCO Mwanza. Huduma ya dharula ukiwapigia ndo utasikia vituko. Ombi langu kwa mtendaji huyu asikae ofcn kusubiria riport, azunguke kuangalia hujuma za wafanyabiashara na wanasiasa kupitia TANESCO.
 
sometime wanakata (collution between wafanya biashara na wafanyakazi wasio waaminifu) umeme ili wauze Generators za kuzalisha umeme majumbani au mafuta yanayotumika kwenye hizo Generators.
 
Back
Top Bottom