Habari za kazi wana MMU,
Leo nimesikitishwa na wanawake wawili hapa kazini wanao gombea mwanamme mmoja,kwanza ilikua wanafanya siri
Mpaka ikawa kila mmoja anamjua mwenzie sasa yakaanza mashindano ya kugawa zawadi kwa mwanamme,Ghaliyah
Kanunua set bed room set Wafaa akanunua Sofa set imekwenda mpaka Ghaliyah kwao mambo safi kamnunulia bwana
BMW X5 mpya Wafaa hana jeuri hiyo,gari bwana kapewa kama siku 10sasa leo asubuhi kwenye mkutano ndio tiffu
likaanza bwana anavutwa huku mara anavutwa na yule Wafaa akawa anamtukana mwenzie "Mie sio wewe mpaka
Nihonge gari ndio nitakiwe kaa ukijua mwanamke mapenzi"
Ghaliyah akacheka kwa dharau sana akajibu" Muhonge vya thamani mwanamme uone kama atachomoa kwako"
Nikashanga sana wanavyojibizana kisa mwanamme,na yule bwana anacheka yani Wafaa karoa anakigari kama changu
cha mwaka 47 huko, uzuri huyu bwana tunaheshimiana sana nikamuita kumwambia alivyofanya sio sawa
Akanambia wote wanajigonga nasipendi kumuudhi hata mmoja katika wao na nilishawambia wanajua bwana karibuni anawacha kazi na hakuna hata mmoja anaejua.
swali langu waungwana ivi wanawake wengine inakuwaje wanakua na ujinga kama huu? kwani wanaume hakuna?
Ahh babu weee,wako wanao stahili kupewa lakini sio kama mwanamme huyu mwanamme suruali alojibweteka mpaka sofa anunuliwe kwa lipiHebu watake radhi...mbona wanaume kutwa kucha kuwanunulia viwanja,vigari kama si amagari,kuwajengea nyumba...wakati hata wazazi wetu vijijini hawana hata unga robo kibaba.....mla naye huliwa...lo.
Wallah sipendi tabia za wanaume wengine kuhongwa hongwa ovyo na hata ajui kama iko siku vitamtokea puani...
Ahh babu weee,wako wanao stahili kupewa lakini sio kama mwanamme huyu mwanamme suruali alojibweteka mpaka sofa anunuliwe kwa lipi
asojikaza.....
Loh.. Dume zima linajichekesha tuu kuhongwa gari na sofa set hata aibu halina...Kama ni kaka yangu namzaba vibao... Mwanaume hasifiwi kwa kuhongwa bana...!
Kwani we Shufaa mzanziberi? nimevutiwa na lafidhi yako.................btw wanatoshana mwayego almuradi wanapagaishwa enough kumhonga huyo bwana gari siye ni nani kuwaingilia?
Shufaa mzanziberi ndo yupi huyo?
I'm just following the trend The Boss.................maana nimeona Ghaliyah mara Wafaa so nimeguess huyu lazima atakuwa anaitwa Shufaa or something like that..................lol
Hivi unajua Shufaa ndio Apple?
we mzanibari nini?
waitwa nani?Twaibaa? lol