Muhimu kwa pcb katika selection za chuo

scientist 08

Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
66
Reaction score
40
Katika kuangalia matokeo yenu nimegundua walio pata daraja lakwanza point 3,4,5,6,7 nizaidi ya wanafunzi 500, huku MD muhimbili wanachukua 210 na UDOM 90 jumla 300,ushauri Wangu wanafunzi mliopata 8 na 9 mnapojaza muhimbili jazeni pharmacy, nursing, lab na vyuo vya private kama utaweza Ada yao ,tulieni sana katika kuomba vyuo Mungu atawasaidia tunajua msuli wa pcb unavyotesa
 


Hawatakuelewa kwa sasa hivi, ila baadae watakuelewa
 

Lakini pia si vibaya ku take risk na kujaribu kwa sababu kuna watu wataomba Dental surgery pia hapo, kuna watu wataenda kusoma nje na pia gharama za kuomba si ni elfu 10 tu (it is relatively safe to take a risk at the expense of ten thousands shillings).

NB: Angalizo lako ni la msingi sana.
 
Mimi nitakuwa shahidi yako katika hili

Unajua mimi hili jambo lilinitokea ila NIKAANGUKIA MIKONO SALAMA, namwelewa mtoa mada vizuri mno, ukipiga dv 1.8 unaona ufaulu mkubwa sana ila asee ni wa kawaida mno kulinganisha na nchi nzima
 
Unajua mimi hili jambo lilinitokea ila NIKAANGUKIA MIKONO SALAMA, namwelewa mtoa mada vizuri mno, ukipiga dv 1.8 unaona ufaulu mkubwa sana ila asee ni wa kawaida mno kulinganisha na nchi nzima

Ni kweli ukisemacho, vipi mwenzangu uliangukia wapi (mikono salama ipi) kama hautojali ?
 
Ni kweli ukisemacho, vipi mwenzangu uliangukia wapi (mikono salama ipi) kama hautojali ?

Nilikua napenda kusoma kozi za kompyuta vyuo nilivyokua nataka kusoma ni UDSM TU, selection ikanitoa OUT, nikachaguliwa Ardhi, mood ya kusoma ikakata kabisaa, ikabidi nibadilishe kozi juu kwa juu, ukifika chuo zile point huwa wanazipandisha sa ukitaka kuhama wakataka 8 kwenye masomo mawili tu nikawa nazo nikaingia kupiga BUILDING ECONOMICS,

Sijutii mpaka kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…