Muhimu kwa mustakabali wa afya yako

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
ENERGY.jpg
ENERGY.jpg


Azam company ni kampuni inayorisha Watanzania na nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara. Mzee wetu huyu amekuwa msaada mkubwa kwa

Watanzania na nchi jirani zinazotuzunguka kupitia huduma mbali mbali anazotoa kuanzia usafiri wa majini, vyakula hata vinywaji. Sitasita kumpongeza
mzee wetu kwa huduma zako na Mungu atakulipa kwa ili.

Kilichonifanya nikujadili hapa mzee ni hiki kinywaji chako kipya , Watanzania wamekipokea na wanakitumia sana kifupi kinauzika huu ndio ukweli.Na mimi kama miongoni mwa wateja wake nikajaribu kukionja kutaka kujua kina ladha gani kinywaji hiki? Kinywaji hiki kinaitwa

# ENERGY
# DRINK .Baada ya kufungua na kuonja kwa mara ya kwanza kilinishinda kurudia fundo la pili nikajua labda huenda ni gesi ngoja nikiache kwa muda
kidogo, lakini hata baada ya kukirudia tena bado kilinishinda.

Nikajikuta navutiwa kusoma kimeungwa kwa kutumia viungio gani(ingredients) hiki nilichokiona ndicho kilichonifanya niandike haya , malengo sio kuharibu biashara yako la ni kuwajuza Watanzania ambao wengi wetu lugha iliyotumika hapa ni changamoto kuijua , lakini pia wengi wetu huwa hatuna utamaduni wa kusoma hivi vibandiko kabla ya kutumia .

NI NINI NILICHOKIONA NA KIKANISTUA?? HIKI HAPA !!
1.INGREDIENTS(VIUNGIO)

Water sugar, Carbondioxide,Citric acid,(E330),Taurine, Acidity Regulator Sodiumcitrates E331,Colour plain , Caramel E150a, ‪#‎CAFFEINE ,Inositol,Preservative Potassium Sorbate E 202,Flavouring,Niacin,Pantothenic Acid, Vitamin B6, B12.

Baada ya kuandikwa hivi viungia ukiangalia katika chupa hii kilichofatiwa ni muda wa matumizi na mahali kinapozalishwa. Lakini bado sikupata mantiki kwanini kimekuwa kikali mno kwanini!!!! GHAFRA katika kudadisi zaidi ndipo chini ya maandishi hayo nikakuta maandishi mengine mapya tena yamewekwa juu ya wino#MWEKUNDU# kuashiria TAHADHALI bila kuandikwa neno lenyewe la TAHADHALI Maandishi haya yameandikwa katika lugha ya KINGEREZA yanasomeka hivi:

"High caffeine content(31.5mg/m100)Taurine(0.0 3%).Do not Drink More than 2battles per Day, Not suitable for persons Sensitive to Caffeine, Children, Pregnant, Breast feeding women and Avoiding Drinking before sleeping"

# TAFSIRI YA # MANENO HAYA KWA TUSIOJUA!! Ina kiasi kikubwa cha CAFFEINE, Usinywe zaidi ya chupa 2 kwa siku, Haifai kwa watu wenye matatizo na CAFFEINE, haifai kwa watoto, wajawazito, wana mama wanaonyonyesha na mwisho Usitumie muda mfupi kabla ya kwenda kulala kinywaji hiki. Kwanini usinywe muda mfupi kabla ujakwenda kulala ?

Kiwango cha 31.5mg/ml100 za caffeine ni nyingi kwa matumizi ya kawaida hivyo kuna hatari ya blood pressure kushuka na ukiwa usingizini na hatimaye ukapoteza maisha hivyo ni hatari kunywa wakati unakwenda kulala, inaathiri ubongo pia. kwa watoto na hata watu wazima. kwa wajawazito, kwa wanaonyonyesha.

Sasa Mzee wangu Baresa ni watanzania wangapi wanatumia kinywaji hiki pasipo kujua? kuna wajawazito watoto, wazee wote wanakibugia tu hawajui kinachoendelea katika kinywaji hiki mzee. Hakuna kinywaji ambacho ni CARBONATED kisichokuwa na CAFFEINE hii inajulikana lakini mzee HIKI KIWANGO CHA (31.5mg/100m)

ULICHOWEKA HUMU NI KIKUBWA MNO Sina hakika lakini inawezekana KIKAPITA hata kiwango cha kwenye HEINKEN . CAFFEINE DRINK Kuna baadhi yanchi kama UFARANSA, MAREKANI, HISPANIA, UINGEREZA WAMEPIGA MARUFUKU Kutokana naathari zake hasa KATIKA UBONGO.
Hakuna shaka Mzee baada ya muda mfupi wa matumizi ya kinywaji hiki WATANZANIA WENGI.

HASA kina mama na watoto na hata wanaume watapata matatizo haya , MFUMO WA UBONGO kuathirika hili halina shaka , VIDONDA vya tumbo, kwa wana mama wajawazito wanaobugia pia watazaa watoto wenye matatizo hasa AKILI kutokana na Ubongo kuathiliwa, wanaonyonyesha pia, MZEE kama ujumbe huu utakufikia naomba TUONDOLEE JANGA ILI Maana haya matatizo
tuliyonayo YANATUSHINDA .

Watanzania wengi wataumia SIKU CHACHE ZIJAZO na hazipo mbali.
 
Yani nimemtoa thamani yote azam baada ya kutoa hiko kinywaji tena kwa jero jero bora hata angeuza buku mbili wangenunua watu wazima lkn jero!?tutegemee taifa la machizi lijalo manake mtoto aende dukan anunue hiko kinywaji kuna mwenye dukan gani akaacha hela kwasababu ya kumuonea huruma mtoto alieenda kununua?! Nashkuru kwa kuleta uzi huuu sana tena sio udini mnk mm ni muislamu tena ahlusunna salafiyyah
 
Kimsingi ili kinywaji(beverages) kiitwe energy drink zinahitaji kua na stimulants drugs haswa caffeine kwa wingi.

Umeongelea azam tu je hivo vingine kama redbull, monster energy nk. Vinafaa kwa matumizi? Na viwango vyao vya caffeine ni kiasi gani labda tufanye comparison?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom