Muhimu kwa great thinkers!.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimu kwa great thinkers!..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sinapindu, Feb 22, 2011.

 1. sinapindu

  sinapindu Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari za jioni!
  Naomba msamaha iwapo nitakuwa mkosefu katika ufikishaji wa fikra zangu hapa, nimekuwa kimya kwa muda nikisoma mengi hapa na kufanya tafakuri kuangalia mashiko ya hoja katika mijadala mbalimbali lakini hatmae nimegundua katika ung'amuzi wangu kuwa kuna tatizo la kutoichanganua CHANYA.

  Pengine nitakuwa sielewi vema uhali chanya ni upi?au ukoje?katika uhalisia wake, hivyo nitatarajia kuelimishwa na kufahamishwa kwa kina, lakini pengine nanyi mnaelewa vema UCHANYA au mnaelewa vema ndivyo sivyo uchanya ulivyo, hapo hati hii itakuwa somo mintarafu kwenu, Kwa vyovyote viwavyo hali hii inatuhamasisha kukubali kukubaliana kuwa tumekuwa na tofauti za msingi katika kile kinachoweza kutunasibisha wote hapa kuwa tuna uelewa wa mambo na tena tunaelewa kwa ufikiri chanya watanzania wenzangu.

  Naamin pia kuwa tunaifaham kwa hakika hata kama si kichanya kuwa tunayo safari tena iliyo ndefu katika usahihishaji,uboreshaji,uelimishaji,uteteaji na uundaji chanya wa jamii yetu kuanzia ngazi ya chini hadi kileleni, na pia nakosa shaka ya kuwa eti hatutambui ila naamini tunatambua kuwa katika safari hii kuna changamoto kadhaa zinazoikabili jamii yetu kwa sasa.
  Ukweli ni kuwa MAPENZI NI SHINIKIZO LA UPOFU WA MOYO KWA AKILI YA MWANADAMU na TAFAKURI KATIKA AKILI YA MWANADAMU NI UFUNGUO WA MUONGOZO WA FIKRA KATIKA USTAWI WA KILA JAMBO LA MWANADAMU
  Hivyo basi ni vema kwa Wafikiriaji wawe watulivu tena wawe watu wa mijadala mipevu inayotegemea uwezo wa tafakuri katika akili kwa kina na si mianguko ya upofu wa mioyo, hapa akili zinapaswa kuchimba, kuibua, kufukua, kufufua, kuchakatua {ku~process} na kupanga mikakati thabiti ya utatuzi wa matatizo tatizi katika kinachotatiza watatizwaji iwe tumo miongoni mwao au si katika wao.

  Ndugu zangu ukweli utabaki kuwa ukweli kwa muda wote wa maisha ya dunia hii, ukweli wafikiriaji na wajadiliaji mijadala mingi wana tatizo la kuacha kujadili kwa fikra zao na matokeo yake hutumia sehemu ya bongo zao za nyuma kutema kumbukumbu ya nukuu za wenzao waliojituma kufikiri na wakanena kuendana na changamoto za maisha ya mwanadam. Si kosa na sisemi kamwe kuwa ni kosa kunukuu semi za wasemao vema duniani, ila nasema ni vema nasi tunene maneno ya hekima {kama tumejaaliwa hekima na kama hatunayo pole yetu} yatakayonukuliwa na vizazi vingine.

  Tujipe fursa ya kuishi katika ukweli kwa kuwa duniani tunapita,isije ukaja wakati binadamu wajao wakadhani ulipata kutokea muda hapa duniani waliishi wanatheolojia, ambao hawakufikiri na kunena maneno yao ila walikuwa wananukuu BETI, STANZA na AYA katika BIBLIA, MISALE YA BWANA, NYIMBO, KHADITHI ZA MTUME na QUR'AN, pia hapa sisemi kufanya hivyo ni kosa, bali nasema itakuwa tumeviongopea vijukuu vyetu, kwani wangapi ni makasisi, wachungaji, maaskofu na masheikh miongoni mwetu? Hao mbona ni idadi ndogo katika sisi? Tena akheri tungekuwa wafuasi makini wa dini zetu katika matendo, lakini wala maneno tunayoyanukuu hatuyaishi kabisa, sisi tutakanwa mkano wa tofauti ya ule alokanwa mkweli yule YESU wa Mariamu. Yeye ilikuwa mara tatu tena alfajir, pengine kwa kuwa alikuwa mkweli na aliyaishi aliyoyanena huku akinukuu mkweli mwenzake ISAYA, lakini sisi twaweza kukanwa mara mia kenda na kenda tena wakati wa adhuhuri jua linapongeuka kati. Hakika OLE WETU WASOMI WAPOFU!
  Hakika tatizo la wengi ni kutohitaji kujifunza ujenzi wa hoja zenye nguvu au uteteaji wa hoja zao dhaifu lakini zenye ukweli lukuki ,...tatizo hili limekuwa ni kubwa sana kwa wachangiaji au wajadiliaji mijadala katika hashuo hili au matando-pepe karibu yote kuanzia Facebook TZ, JAMII FORUM, Jukwaa huru nk.

  Nimenena haya leo, sikunena jana, haingalipo jana sasa ndio sababu nikanena leo kwa ajili ya kesho, nimethubutu kunena, nimethubutu kujitanabaisha. Hakika nimesema kwa kuwa nimeona niseme ambacho hakijasemwa hapa katika msemo huu. "if something positive has not yet done, we have to be the first to do or act" Kumradhi kwa kutumia lugha ya wageni kwa kuwa ndio jadi ya hao wasiofikiri kufikirisha akili zao, miongoni mwetu, wasije wakadhani siwajali.
  Nimenena wanaofikiri na kupenda kufikiri watafikiri na kuungana nami kufikiri zaidi na kufanya jitihada katika ujenzi wa jamii bora.

  Sina neno jema ila tuuache UKASUKU kwa kuwa tofauti ya kasuku na sisi ni kufikiri na kuamua kwa utashi. Ahsanteni sana karibuni katika tafakuri chanya mkiwa na kumbukumbu kuwa HATA SAA INAYOONGOPEA WAKATI, UPO MUDA HUTAJA WAKATI SAHIHI!


   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  samaraizi basi ili tuweze kusoma kwa furaha....
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mh,asante,ntarudi kusoma kwa mara ya tatu labda nitaelewa zaidi.....:hand:
   
 4. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Duh duh duh....,..,,hao ndio wana-thinka ,akhsante kwa ujumbe
   
 5. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Duh! Nahis unapoint nzito,ila mada umeileta ki unwelcoming. Uchanya na utafakuru wa nadharia halisia ndio nini?
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kaazi kwelikweli!
   
 7. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mkuu una ujumbe mzito sana lakini lugha yako ndo imekuwa ngumu sana kwa members kuupata. Yah nakubaliana sana na wewe kwa sasa critical thinking imeshuka sana nafikiri kuliko kipindi chote cha historia. Kizazi hiki kimekuwa ni cha kunukuu zaidi ya kucreate. Jamii zote tangu za wasomi hata walio chini kabisa tumekuwa ni watu wa kunukuu aliyosema Aristotle, Newton, Karl Marx, Yesu kristo, Martin Luther King JR na wengine wengi walio kwenye historia. Hatuna tena watu wenye kujenga fikra na kutoa hata zipewe heshima na kukubalika kama hawa ma thinker wa enzi hizo. Kila mtazamo unaofanywa sasa na walimwengu ni kurefer aliyesema critical thinker kama akina Gallilei, Nyerere hapa kwetu, JFK, George Washington na wengine na kufanya kama gold standards ambayo inatumika kupimia performance zetu sasa.

  Tunahitaji kutazama upya elimu na mapokeo yetu sasa tangu katika level ya chini kabisa ya makuzi kwenye familia zetu kuona tunajenga vipi watoto wetu kuwa na uwezo wa kutafuta majibu ya challenges za maisha tangu katika level zao na sio ukasuku wa kucopy mapokeo yetu (kuelezwa majibu ya nini cha kufanya). Hii inatakiwa kuenda juu hadi kufikia kwa vyuo vyetu na taasisi mbalimbali hatimaye baada ya kujenga critical thinking ndo mambo yatabadilika na mtazamo wetu hasa wa kujitambua sisi ni nani na our purpose of life itakuja.

  Tutaweza kujenga personal philosophies na kuwa na uwezo wa kuzisimamia kwa nguvu zote. Leo hii mtu yupo tayari kwenda kinyume na taaluma yake kwa vile hana anachokiamini kuwa ni ukweli hata taaluma zetu tumetupa kando kwa kununuliwa na pesa kidogo tu. watu wetu watajua kutafuta solutions za maisha na sio kutafuta shortcuts kama sasa kutegemea rushwa, usanii na kuona watu wanakuwa proud na kufanya mambo kwa ajili ya taifa lao. Ndipo na uzalendo utakuja sio wa kuambiwa na wanasiasa kuweni wazalendo. Uzalendo ni attitude na hii inajengwa tangu utotoni katika makuzi.

  Maadili yote ya nchi yetu yanapotea kwa sababu ya mparanganyiko uliopo wa mapokeo ya elimu ya jamii zetu na pia elimu ya kimagharibi ambayo nayo tunababaisha tu. Hatujengi umahiri katika fani zetu. Msomi wa leo hawezi kuunganisha utaalamu wake kwa upana wake yaani Knowledge, skills na Attitude zinazounda fani yake. Tunakariri kama kasuku na kubeba shahada bila elimu ya kutumia matokeo yake wasomi hawajui hata capacity zao. Hii imesababisha watu wetu kuona cheti ndio elimu na ndio maana sasa watu wanatengeneza vyeti feki kwa vile anatafuta ajira na mwajiri anaangalia cheti sio uwezo wa mtu na tija.

  Leo hii ukiuliza mchango wa wasomi Tz tangu madaktari (PhD holders) hadi chini hutaona tofauti yao katika kuanalyze mambo. Na wote tumekuwa tunakimbilia ajira tu, nani anatengeneza hizo ajira hatujui. Tafuta kati ya wasomi nani ana ubunifu hata kufanya kitu kinachoonyesha critical thinking na ana theory ambazo watu wengine watajifunza hutaona Tz.

  Nilishamuona daktari mmoja pale MNH analumbana na mwanafunzi wa udaktari (MD) kwamba kakosa swali kwenye mtihani wakati alimkaririsha hivyo kwenye physiology akidai nanukuu "Renal physiology is a controversial subject that any concept can be right or wrong" mwisho wa kunukuu, jamaa akaleta kitabu mwalimu huyo alichofundishia kuonyesha reference, yule lecturer akadai Guyton (Mwandishi wa kile kitabu) ana Phd kama mimi so anaweza kuwa wrong pia. So hii inaonyesha jinsi gani tunatakiwa kuumiza vichwa vyetu na kuanza upya kujenga mtazamo wetu. Nikajiuliza kama hiyo concept anafikiri ni wrong na yeye anaamini mwandishi kaandika uongo, kwa nini asifanye research kupata ukweli achallenge na kutoa kitu sahihi ili kirekebishwe na jamaa ya wanaosoma physiology wapate ukweli???

  Hapo ndipo tulipo tunalalamika tu na kuona wenzetu wamekosea lakini hatujifunzi na kurekebisha makosa. Msomi akipewa taasisi ya serikali inakufa hamna ubunifu wakati taasisi binafsi zinafanya kazi na kudumu. Kampuni inaanza kufa moja zingine zinafuata utafikiri wameambiana tuue. Wakati wenzetu ikifa moja ile nyingine inajifunza makosa ili kusurvive. Kulearn tokana na makosa ya wenzie. Mamia ya makampuni na mashirika ya umma (vyama vya ushirika pia) yamekufa wakati hayakuwa na mshindani loh inatia uchungu sana.

  Cha kusikitisha zaidi hakuna efforts zozote za makusudi zinazoonekana angalau kupangwa hata kwa kudanganywa hakuna anayeumiza kichwa kufikiria tumepotoka wapi na kutafuta majibu ya kudumu ila tunatafuta majibu ya emergencies.

  Ndo maana Ngeleja hadi leo tatizo la umeme lina miaka karibu 10 yeye anasema ni dharura!!!

  Nawakilisha!
   
 8. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ahhhhhhh!!! kata vipande vipande basi!! inatia uvivu kusoma!!
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimekupata, ila mmmh, kuna wakati kiswahili nikigumu kuliko kingereza.
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Upo rafiki?? mnasemaje mjengoni hapo??
   
 11. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hashuo Maana yake ni nini?
   
 12. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sinapindu unatisha
   
Loading...