AFYA NA HIFADHI YA JAMII
Hali halisi:
• Ujenzi wa uchumi imara unategemea sana wananchi
wenye afya njema na pia wenye uhakika na matibabu
pindi kunapokuwa na mahitaji.
• Ujenzi wa miundombinu ya afya lazima uendane na
huduma husika. Baada ya miaka hamsini ya Uhuru,
ujenzi wa miundombinu ya afya, mgawanyo wa
wataalamu na upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa
tiba umejikita katika maeneo machache ya nchi, hasa
mijini. Hali hii imepelekea kutokuwepo kwa uwiano
katika upatikanaji na utoaji wa huduma hizi hapa
Tanzania.
Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015
• Wananchi wengi bado wanagharamia huduma za
afya kwa kutoa pesa mfukoni pindi wauguapo.
• Kupanda kwa gharama za matibabu.
• Magonjwa ya kuambukiza kama UKIMWI na
kipindupindu kuendelea kuwa tatizo kubwa na
magonjwa yasiyoambukiza kama saratani na sukari
kushika kasi miaka ya karibuni kunazidisha umaskini kwa
mtu mmoja na Serikali kwa ujumla.
• Serikali kushindwa kugharamia huduma za afya kwa
kiwango tarajiwa kutokana na kutenga bajeti isiyokidhi;
na ubadhilifu wa fedha chache zinazotengwa kwenye
ngazi mbalimbali za utoaji huduma.
• Serikali Kushindwa kuendeleza programu mbalimbali
za afya (mfano mradi wa damu salama) baada ya
wafadhili kumaliza muda wao kunadhorotesha zaidi
huduma za afya, kunakopelekea kutokea kwa vifo
visivyokua vya lazima.
• Serikali kupoteza fedha nyingi kwa kugharamia
matibabu nje ya nchi hasa kwa viongozi na watendaji
wa serikali.
Hifadhi ya Jamii
• Kwa sasa wazee na wote wasiojiweza wamepangiwa
kupata huduma za afya bure ili hali upatikanaji wa tiba
na vifaa tiba katika taasisi za umma ni hafifu.
• Wazee na wasiojiweza wamekuwa wakikusanywa
kwenye nyumba za matunzo (makambi) na kupatiwa
huduma zisizokidhi. Makambi haya yamewafanya
wazee kuishi kifungoni na kuwasababishia upweke,
msongo wa mawazo, kusononeka na hata sonona.
Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015
• Kuwepo kwa mifuko ya bima na hifadhi ya jamii.
• Kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi kwenye sekta ya
afya katika vyuo vikuu na vyuo vya kati kunatoa fursa ya
kupatikana watumishi wengi wa afya.
• Ongezeko la vituo vya afya vinavyoanzishwa na sekta
binafsi, pamoja na taasisi za kidini na zile za kijamii.
• Wazee ni kitovu cha busara cha Taifa wanahitaji matunzo
bora zaidi.
CHADEMA itafanya nini:
• Tutahamasisha idadi zaidi ya Watanzania wajiunge na
bima za afya za malipo nafuu.
• Kuimarisha afya ya msingi pamoja na kinga na kuendeleza
programu mbalimbali za afya baada ya wafadhili
kuondoka.
• Itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa
Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015
afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki
ikiwa ni pamoja na kusomesa kwa gharama ya serikali
wataalam bobezi (Specialists) katika fani mbalimbali za
afya. Pia wataalamu walio mafunzoni kwa vitendo(kama
vile intern doctors, pharmacists, lab scientist, nurses nk)
wanaohudumia wagonjwa katika vituo vilivyoainishwa
watapatiwa posho za kujikimu ili kuwavutia wataalamu
hawa kubaki katika sekta ya afya na kuhakikisha wananchi
wengi wanapata huduma kwa haraka.
• Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuimarisha miundombinu
ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga hospitali za kisasa
na kuboresha mifumo ya rufaa ili kusogeza huduma za
afya karibu na jamii, kuanzisha utalii wa huduma za afya
(medical tourism) na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
• Kurejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea
kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na mishahara,
nyumba za kuishi na usafiri.
• Kuthibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila
kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile
serikali na hospitali za sekta binafsi/kijamii/kidini.
• Kuboresha huduma za afya kwa kurejea na kutunga
sheria za kusimamia taaluma za afya ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kunakuwepo na mafunzo endelevu katika
taaluma hizo.
• Kuharakisha upatikanaji wa dawa za bei nafuu za
magonjwa sugu kama kisukari na serikali kugharamia
magonjwa hatarishi "terminal illnesses' kama saratani na
UKIMWI.
• Kurejea na kuboresha Taasisi za afya kama MSD, NIMR,
TFDA, NHIF ili ziweze kutoa huduma bora na haraka kwa
wananchi.
Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA2015
• Kuhamasisha na kugharamia tafiti za afya hasa
zinazolenga kuimarisha kinga na kupunguza gharama za
huduma za afya.
• Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu
inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi
kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii
zao. Pia kwa wale wenye matatizo ya macho watapatiwa
miwani bure.
• Kuanzisha nyumba mpya na kuboresha nyumba za
matunzo ambazo zinahudumia wasiojiweza ambao
hawana fursa kuishi na jamii zao.
Matokeo tarajiwa
• Wanachi kupata huduma za afya kupitia bima ya afya
na mifuko ya jamii bila malipo kutoka mfukoni mwao pindi
wauguapo.
• Huduma za afya zitatolewa kwa gharama iliyo rafiki kwa
mtumiaji na kwa ubora zaidi.
• Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaojali afya zao ili
kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambuzwa.
• Kupungua kwa tatizo la rasilimali watu katika sekta ya afya
kupitia ongezeko la vituo vya mafunzo na mafunzo kwa
vitendo.
• Watumishi wa afya kufanya kazi kwa ufanisi na hivyo
kuwawezesha kutoa huduma bora zaidi.
• Wazee na wasiojiweza kuishi na jamii zao wakiwa na uwezo
wa kujikimu ki maisha.