Muhimbili: Wagonjwa wa figo waelezea Matatizo wanayokumbana nayo. Waomba Waziri Ummy awasaidie

CHANGAMOTO TUNAZO PITIA WAGONJWA WA FIGO MUHIMBILI.

Ndugu Mheshimiwa waziri zifuatazo ni changamoto tunazo pitia Kama wagonjwa wa figo.

1. Gharama za kuchuja damu (dialysis) ziko juu sana kwa watu wanaolipa cash hata kufikia kupotezea wenzetu wengi walio shindwa kulipia hivyo tunaomba mtupuguzie ikiwezekana mtutafutie donors ili tuweze kufanya bure Kama vile wa athirika wa madawa wanavyo lipiwa.

2. Kume kuwa na gharama kuongezeka Mara kwa Mara kwenye sindano ya EPO kuongeza damu mwanzo ilikuwa 4000 ila kwa Sasa iko juu 16,000 kwa sindano moja tunaomba ishuke.

3.Swala la kupata msamaha ustawi wa jamii kwa Sasa limekuwa halipo kabisa kinyume na muongozo wa msamaha wa ustawi wa jamii kwani wengi kwa Sasa hatuna uwezo wa kulipia na familia zimesha tu choka kutusaidia na tunashi kwa kusaidiwa na rafiki nao wamesha tuchoka.

4. Huduma tunazo pewa na ma nesi nazo ni changamoto lugha zao sio nzuri kwa wagonjwa ....

5. Swala la parking lime kuwa changamoto tuna lazimishwa kulipia wakati pesa tu ya matibabu kuipata inakuwa shida tunaomba magari yote ya wagonjwa yaingie free na kutoka bila kulipia kwa kuwahatuna uwezo. Wagonjwa wa Figo wanaenda Muhimbili saa tatu Usiku na kutoka saa moja asubuhi. Halafu Maegesho unalipishwa 1,000 kila saa tena usiku. Masaa nane ya kukaaa Muhimbili unalipia Maegesho 8000 hadi 10,000 saa nyingine. Tunaomba Wagonjwa wasilipishwe maegesho.

6.Mheshimiwa waziri tunaomba kama msamaha unatolewa kiwango Cha cash kiwe kimoja siyo wengine wanalipa elfu 30, wengine laki na themanini wengine elfu sabuni inatutengenezea mazingira ya kuhisi wanapokea rushwa maana wengine wananyinwa msamaha

Muhimbili Mbu ni wengi, kwanini wasipulizie dawa? Tunakesha na mbu kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.
Nimetokwa na machozi.
Mungu awaponye.
 
Mkiambiwa muache kumeza MADAWA YA AJABU AJABU HAMTAKI, atiii ooohhhh tunafuata utaalamu wa afyaa!

Baadaye buuum, mafigo yamefelii. Unaanza Kutoa ushuzi kama kuku.

Bado tena mnakunywa soda na machipsi ya ajabu ajabu. Hamtaki kula magimbi ati ni ushamba!

Ati ujanja ni kunywa cocacola na kufungiwa madripu ya kutibu figo!
 
Nilipoona kwa kunywa maji mengi sanaa kama lita tano kwa siku pamoja na dawa fulani ya maji nachanganya na maji nikiwa nayatoa kwa njia ya mkojo na maumivu yalikuwa makali sana kadri mawe yanavyoshuka chini ,,Hali hii ya mawe imenipata mara tatu kwa interval ya miaka 2-3 ilaa kwa sasa natumia sana malimao haijarudi tena kwa miaka kama 4 hivi

Hongera sana mkuu!...itabidi uwe mwalimu na balozi kwa wengine...Mungu akupe moyo wakusaidia wengine wenye shida kama hiyo na wanateseka vitandani!...
 
CHANGAMOTO TUNAZO PITIA WAGONJWA WA FIGO MUHIMBILI.

Ndugu Mheshimiwa waziri zifuatazo ni changamoto tunazo pitia Kama wagonjwa wa figo.

1. Gharama za kuchuja damu (dialysis) ziko juu sana kwa watu wanaolipa cash hata kufikia kupotezea wenzetu wengi walio shindwa kulipia hivyo tunaomba mtupuguzie ikiwezekana mtutafutie donors ili tuweze kufanya bure Kama vile wa athirika wa madawa wanavyo lipiwa.

2. Kume kuwa na gharama kuongezeka Mara kwa Mara kwenye sindano ya EPO kuongeza damu mwanzo ilikuwa 4000 ila kwa Sasa iko juu 16,000 kwa sindano moja tunaomba ishuke.

3.Swala la kupata msamaha ustawi wa jamii kwa Sasa limekuwa halipo kabisa kinyume na muongozo wa msamaha wa ustawi wa jamii kwani wengi kwa Sasa hatuna uwezo wa kulipia na familia zimesha tu choka kutusaidia na tunashi kwa kusaidiwa na rafiki nao wamesha tuchoka.

4. Huduma tunazo pewa na ma nesi nazo ni changamoto lugha zao sio nzuri kwa wagonjwa ....

5. Swala la parking lime kuwa changamoto tuna lazimishwa kulipia wakati pesa tu ya matibabu kuipata inakuwa shida tunaomba magari yote ya wagonjwa yaingie free na kutoka bila kulipia kwa kuwahatuna uwezo. Wagonjwa wa Figo wanaenda Muhimbili saa tatu Usiku na kutoka saa moja asubuhi. Halafu Maegesho unalipishwa 1,000 kila saa tena usiku. Masaa nane ya kukaaa Muhimbili unalipia Maegesho 8000 hadi 10,000 saa nyingine. Tunaomba Wagonjwa wasilipishwe maegesho.

6.Mheshimiwa waziri tunaomba kama msamaha unatolewa kiwango Cha cash kiwe kimoja siyo wengine wanalipa elfu 30, wengine laki na themanini wengine elfu sabuni inatutengenezea mazingira ya kuhisi wanapokea rushwa maana wengine wananyinwa msamaha

Muhimbili Mbu ni wengi, kwanini wasipulizie dawa? Tunakesha na mbu kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.
Poleni sana Wapendwa wetu kwa hizo changamoto.
 
Apple cider vinegar unaweka kijiko kimoja kwenye glass ya maji ya vuguvugu, unakunywa asubuhi na jioni. Unaweza search YouTube kidney stones - DK Berg.
Hunywi tu mkuu.
Kuna muda, namna yake ya kunywa na kukaa mikao ya hayo mawe kitoka
 
Watu wengi hawanywi maji wanakunywa soda pombe na vinywaji vingine! Kunyweni maji kwa wingi hii tunaita water therapy kunyweni maji usingoje kusikia kiu maana kusikia kiu ni kwamba umeshaishiwa maji mwili tayari!
Dialysis sio nzuri haijawahi kuwa nzuri hata kidogo, ni mateso makubwa sana kukaa kwenye mashine hiyo ni basi tu kwa sababu ni tiba lakini inaumiza mnoo!! 😌😌😌
 
Back
Top Bottom