Muhimbili: Wagonjwa wa figo waelezea Matatizo wanayokumbana nayo. Waomba Waziri Ummy awasaidie

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
CHANGAMOTO TUNAZO PITIA WAGONJWA WA FIGO MUHIMBILI.

Ndugu Mheshimiwa waziri zifuatazo ni changamoto tunazo pitia Kama wagonjwa wa figo.

1. Gharama za kuchuja damu (dialysis) ziko juu sana kwa watu wanaolipa cash hata kufikia kupotezea wenzetu wengi walio shindwa kulipia hivyo tunaomba mtupuguzie ikiwezekana mtutafutie donors ili tuweze kufanya bure Kama vile wa athirika wa madawa wanavyo lipiwa.

2. Kume kuwa na gharama kuongezeka Mara kwa Mara kwenye sindano ya EPO kuongeza damu mwanzo ilikuwa 4000 ila kwa Sasa iko juu 16,000 kwa sindano moja tunaomba ishuke.

3.Swala la kupata msamaha ustawi wa jamii kwa Sasa limekuwa halipo kabisa kinyume na muongozo wa msamaha wa ustawi wa jamii kwani wengi kwa Sasa hatuna uwezo wa kulipia na familia zimesha tu choka kutusaidia na tunashi kwa kusaidiwa na rafiki nao wamesha tuchoka.

4. Huduma tunazo pewa na ma nesi nazo ni changamoto lugha zao sio nzuri kwa wagonjwa ....

5. Swala la parking lime kuwa changamoto tuna lazimishwa kulipia wakati pesa tu ya matibabu kuipata inakuwa shida tunaomba magari yote ya wagonjwa yaingie free na kutoka bila kulipia kwa kuwahatuna uwezo. Wagonjwa wa Figo wanaenda Muhimbili saa tatu Usiku na kutoka saa moja asubuhi. Halafu Maegesho unalipishwa 1,000 kila saa tena usiku. Masaa nane ya kukaaa Muhimbili unalipia Maegesho 8000 hadi 10,000 saa nyingine. Tunaomba Wagonjwa wasilipishwe maegesho.

6.Mheshimiwa waziri tunaomba kama msamaha unatolewa kiwango Cha cash kiwe kimoja siyo wengine wanalipa elfu 30, wengine laki na themanini wengine elfu sabuni inatutengenezea mazingira ya kuhisi wanapokea rushwa maana wengine wananyinwa msamaha

Muhimbili Mbu ni wengi, kwanini wasipulizie dawa? Tunakesha na mbu kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

Majibu ya Uongozi wa Muhimbili - Prof. Janabi akieleza Jinsi Serikali inavyochangia utoaji huduma za Figo
 
Dah aisee vile nimepata shida ya mawe kwenye figo mara tatu naogopa sanaa siku figo zifaili nikawekwe kwenye hizo mashine kwa masaa yote hayo
Uliponaje mkuu,mi nilitumiaga dawa ya kuweka kwenye maji yalikuwa ynatoka kwa njia ya mkojo
 
Nilipoona kwa kunywa maji mengi sanaa kama lita tano kwa siku pamoja na dawa fulani ya maji nachanganya na maji nikiwa nayatoa kwa njia ya mkojo na maumivu yalikuwa makali sana kadri mawe yanavyoshuka chini ,,Hali hii ya mawe imenipata mara tatu kwa interval ya miaka 2-3 ilaa kwa sasa natumia sana malimao haijarudi tena kwa miaka kama 4 hivi
 
Daaah! Mh.Waziri,afanyie kazi masuala hayo,aonyeshe kujali.Wagonjwa wa figo wanapitia hali ngumu sana,hasa kwenye gharama za uchujaji damu,kama alivyotanabaisha mleta mada.Donors wakipatikana,itakua vema.
Daaaah! pole kwa waathirika.
 
Nikisikia mtu anafanyiwa dialysis huwa naogopa sana kuna jirani yangu alikuwa akienda mwenyewe muhimbili kufanyia dialysis anarudi ,lakini kuna siku kama kawaida yake alienda akaishia huko huko watu wanamsubilia arudi kumpe ndo kapotea R.I.P
 
Nilipoona kwa kunywa maji mengi sanaa kama lita tano kwa siku pamoja na dawa fulani ya maji nachanganya na maji nikiwa nayatoa kwa njia ya mkojo na maumivu yalikuwa makali sana kadri mawe yanavyoshuka chini ,,Hali hii ya mawe imenipata mara tatu kwa interval ya miaka 2-3 ilaa kwa sasa natumia sana malimao haijarudi tena kwa miaka kama 4 hivi
Na matunda ya apple pia yanasaidia
 
Nyama choma pia na chumvi unapokula nyama ndo vilivyonisababishia mawe vile nilikuwa napenda sana chumvi
Daaah! inaogopesha sana,ndomaana ukimsikiliza Dr.Janabi,unaweza ukaona unakosea kila unachofanya.Kutunza afya ni kazi sana,ila ikipata hitilafu,ni kazi zaidi,na ndo unalazimika kuilinda kwa masharti magumu.Tuwe tunawadadisi watumishi wa kada za afya,kila tuendapo kwenye vituo vya kutolea huduma zao,hii yaweza ikatufanya tukapata taarifa zinazoweza kutusaidia kuepukana na yanayoweza kuepukika.
 
Nilipoona kwa kunywa maji mengi sanaa kama lita tano kwa siku pamoja na dawa fulani ya maji nachanganya na maji nikiwa nayatoa kwa njia ya mkojo na maumivu yalikuwa makali sana kadri mawe yanavyoshuka chini ,,Hali hii ya mawe imenipata mara tatu kwa interval ya miaka 2-3 ilaa kwa sasa natumia sana malimao haijarudi tena kwa miaka kama 4 hivi
Malimao yanasaidia pia au?
 
Yaani inaogopesha sana,nikimuona mtu anaayefanyiwa dilysis,inaniwazishaga sana.Sasa hivi unakuta hadi kuna watoto chini ya miaka 18,wanafanyiwa dialysis,yaani nikiwaangaoiaga,nawasikitiaga sana,maana hata muda wa kwenda shule anakosa,anabaki ni yeye na tiba husika.Kwakweli Mungu atusaidie.
Nikisikia mtu anafanyiwa dialysis huwa naogopa sana kuna jirani yangu alikuwa akienda mwenyewe muhimbili kufanyia dialysis anarudi ,lakini kuna siku kama kawaida yake alienda akaishia huko huko watu wanamsubilia arudi kumpe ndo kapotea R.I.P
 
CHANGAMOTO TUNAZO PITIA WAGONJWA WA FIGO MUHIMBILI.

Ndugu Mheshimiwa waziri zifuatazo ni changamoto tunazo pitia Kama wagonjwa wa figo.

1. Gharama za kuchuja damu (dialysis) ziko juu sana kwa watu wanaolipa cash hata kufikia kupotezea wenzetu wengi walio shindwa kulipia hivyo tunaomba mtupuguzie ikiwezekana mtutafutie donors ili tuweze kufanya bure Kama vile wa athirika wa madawa wanavyo lipiwa.

2. Kume kuwa na gharama kuongezeka Mara kwa Mara kwenye sindano ya EPO kuongeza damu mwanzo ilikuwa 4000 ila kwa Sasa iko juu 16,000 kwa sindano moja tunaomba ishuke.

3.Swala la kupata msamaha ustawi wa jamii kwa Sasa limekuwa halipo kabisa kinyume na muongozo wa msamaha wa ustawi wa jamii kwani wengi kwa Sasa hatuna uwezo wa kulipia na familia zimesha tu choka kutusaidia na tunashi kwa kusaidiwa na rafiki nao wamesha tuchoka.

4. Huduma tunazo pewa na ma nesi nazo ni changamoto lugha zao sio nzuri kwa wagonjwa ....

5. Swala la parking lime kuwa changamoto tuna lazimishwa kulipia wakati pesa tu ya matibabu kuipata inakuwa shida tunaomba magari yote ya wagonjwa yaingie free na kutoka bila kulipia kwa kuwahatuna uwezo. Wagonjwa wa Figo wanaenda Muhimbili saa tatu Usiku na kutoka saa moja asubuhi. Halafu Maegesho unalipishwa 1,000 kila saa tena usiku. Masaa nane ya kukaaa Muhimbili unalipia Maegesho 8000 hadi 10,000 saa nyingine. Tunaomba Wagonjwa wasilipishwe maegesho.

6.Mheshimiwa waziri tunaomba kama msamaha unatolewa kiwango Cha cash kiwe kimoja siyo wengine wanalipa elfu 30, wengine laki na themanini wengine elfu sabuni inatutengenezea mazingira ya kuhisi wanapokea rushwa maana wengine wananyinwa msamaha

Muhimbili Mbu ni wengi, kwanini wasipulizie dawa? Tunakesha na mbu kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.
Si juzi tu hata wiki haijaisha hapohapo Muhimbili wametoka kuwasifia madaktari bingwa kuwa wamekuwa mkombozi wa figo na sasa shida hiyo imebakia ni historia!?
 
Kama serikali kupitia wahisani wake inatoa ahueni kwa vidonge vya ARV na waathirika, kwa nini isifanye the same kwa wagonjwa wa figo ???
 
Back
Top Bottom