Muhimbili university Diploma 2019/2020

Muhimbili university Diploma 2019/2020

Kama unaangalia future yako ya ajira na kujiendeleza kimasomo nenda Muhimbili na kama unataka uishie mtaani kwenye viji-dispensary vya akina Ngowi na Macha huku ukiwa na Diploma yako ya Clinical Officer basi nenda Lugalo, Naomba nikuelimishe kwa kifupi sana, Ukiwa na diploma ya Nursing ukienda nje Kenya, Namibia, South Africa, Malaysia etc utapata kazi lakini hiyo diploma ya Clinical officer mwisho wake ni Zanzibar na hapo sasa amua kusuka au kunyoa!
Asante mkuu..! Kwa ushauri mzuri
 
Nimechaguliwa Diploma in Nursing And Midwifery chuo cha MUHIMBILI SCHOOL OF MIDWIFERY na OR-TAMISEMI kwenye selection za kidato cha tano, vyuo vya Afya na ufundi 2019/2020. Lakini mimi kwenye selform tulizojaza shuleni niliomba Clinical Medicine LUGALO na Medical Laboratory Sciences Singida College of Health and technology, Nataka kuhama hiyo Nursing niende hizo kozi niliokuwa nimeomba hapo awali, lakini kuna ndugu, jamaa na marafiki wanasihi niende tu hapo Muhimbili Nursing. Natunguliza shukrani naombeni ushauri wakuu wazoefu
Wakiume utasomaje nesi mzee baba
Nyie Ndiyo mnajiita Dr nesi huku kazini
Nenda CO au Lab
Asante broo ndio maana nikaomba ushauri kabla ya maamuzi
Mawazo ya kuwa nursing ni kazi ya wanawake yamesha pitwa na wakati. Ukisoma kwa bidii nursing inakufikisha mbali. Siku hizi kuna hata degree za nursing na nimekutana na manesi ambao wamefika mbali wengine wakiwa wahadhiri vyuo vikuu pamoja na vyuo vya Tiba wakiwafundisha hao madakitari wanafunzi.
Kuna wengi wanaokwenda nchi kama America au Uingereza jiulize wanafanya kazi gani zinazolipa- ni nursing.
Mwaka jana au juzi niliona tangazo la nchi ya UK ikitafuta nurses kutoka Africa. Hivyo ni wewe mwenyewe na malengo yako. NURSING INALIPA.
 
Kwani C.O hawezi kujiendeleza?anaweza soma C.O akimaliza akasoma MD na watu wengi wamepita hiyo njia. Unasema kuishia mtaani kwenye vidispensari ndugu umeongea usiyoyajua...nenda kwenye vituo vya afya ma C.O wapo wa kutosha.Kwa miaka 3 serikali kwa upande wa afya imeajiri watu wengi wenye diploma kwahiyo acha kupotosha
Kama unaangalia future yako ya ajira na kujiendeleza kimasomo nenda Muhimbili na kama unataka uishie mtaani kwenye viji-dispensary vya akina Ngowi na Macha huku ukiwa na Diploma yako ya Clinical Officer basi nenda Lugalo, Naomba nikuelimishe kwa kifupi sana, Ukiwa na diploma ya Nursing ukienda nje Kenya, Namibia, South Africa, Malaysia etc utapata kazi lakini hiyo diploma ya Clinical officer mwisho wake ni Zanzibar na hapo sasa amua kusuka au kunyoa!
 
Mtoa maalda chaguo ni lako uende Muhimbili au Lugalo kila mtu nadhani ametoa yake kila kozi ya afya ina faida yake ni wewe tu kuangalia kipi kitakutoa.
 
Kwani C.O hawezi kujiendeleza?anaweza soma C.O akimaliza akasoma MD na watu wengi wamepita hiyo njia. Unasema kuishia mtaani kwenye vidispensari ndugu umeongea usiyoyajua...nenda kwenye vituo vya afya ma C.O wapo wa kutosha.Kwa miaka 3 serikali kwa upande wa afya imeajiri watu wengi wenye diploma kwahiyo acha kupotosha

Hii ni ajabu ya Kipofu kumwonyesha njia mwenye macho
 
Mimi nataka Clinical Officer hapo LUGALO lakini wadau wananishauri niende muhimbili tu. Kwasababu pote nmepata naombeni ushauri nifanye maamuzi sahihi
Nenda Clinical Officer.
Kibongo bongo, Clinical Officer ana sifa/heshima kuliko Nursing...ingawa wote wana Diploma na mshahara ni sawa.

Nenda Clinical Officer.
 
Huu ushauri ataukumbuka
Clinical officer ana kaOfisi chake saafi. Hata akiwa Mwanaume au mwanamke saafi.
Nesi sasa...Full kutumwa tumwa.

Kama kuna kuchagua machaguo mawili achague hiyo Clinical officer.

Kama kuna chaguo moja tu la Nesi, haina shida kwa kuwa hamna jinsi.
 
Huyo anababaishwa na jina Muhimbili sisi ndo tupo huku kwenye hiyo kada hulali njaa ukiwa C.O
Clinical officer ana kaOfisi chake saafi. Hata akiwa Mwanaume au mwanamke saafi.
Nesi sasa...Full kutumwa tumwa.

Kama kuna kuchagua machaguo mawili achague hiyo Clinical officer.

Kama kuna chaguo moja tu la Nesi, haina shida kwa kuwa hamna jinsi.
 
Mtoa maalda chaguo ni lako uende Muhimbili au Lugalo kila mtu nadhani ametoa yake kila kozi ya afya ina faida yake ni wewe tu kuangalia kipi kitakutoa.
Asante broo angu Mimi acha niingie Nursing hapo Muhimbili wengi wanasema iko poa sana, halafu jambo kubwa sijui hiki chuo lini wanafungua maana sijapata joining instruction hata hawaleti.
 
Vyuo vyote vilivyopo under Nacte wanafungua tarehe 7 ila kwa Muhimbili sifahamu ngoja nitafute kisha nitakujuza
Asante broo angu Mimi acha niingie Nursing hapo Muhimbili wengi wanasema iko poa sana, halafu jambo kubwa sijui hiki chuo lini wanafungua maana sijapata joining instruction hata hawaleti.
 
Sawa mkuu lakini muhimbili kwan ipo under nini
Muhas ipo Under TCU.
Vyuo vikuu vyote ( Vyenye majina ya UNIVERSITY) vipo Under TCU.

Mitihani yao inatungwa na kusahihishwa na walimu wao.

Vyuo vilivyo chini ya NACTE, mitihani ya mwisho inatoka NACTE.
 
Uamuzi wako ni sahihi sana, binafsi sipendi kozi ya uuguzi kwasababu zangu binafsi lakini kama wewe umeipenda nakuhakikishia utafurahia zaidi kuliko hiyo kozi ya Utabibu wanayokushauri.
Pia kwa Muhimbili Institute (chuo ulichopangiwa) utakula bata tu kwa hiyo kozi, hawana mambo mengi, zaidi utapigika na practice hapo hospitali ya taifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom