Muhimbili- hii haijatulia kabisa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili- hii haijatulia kabisa!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Mar 20, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita nimekuwa nikimsindikiza Bi. Mkubwa Muhimbili kwa ajili ya kuonana na Daktari. Kiutaratibu, ukishafika unasubiri kusikia jina lako likiitwa toka kwenye lundo la mafaili yaliyopo. Kwakuwa huwa hawana uhakika ni wagonjwa wangapi watahudhuria kliniki siku husika, basi wanalazimika kutoka na mafaili yote na hivyo kufanya shughuli mzima ya kusubiria jina lako kuwa frustrating. Aidha, ukishasikia jina lako, unasubiri tena kusikia jina lako kwa mara ya pili ili ndipo ukapange foleni kwa ajili ya kulipia Sh. 5,000/=. Binafsi, nimeenda pale kiasi cha mara tano mfululizo, lakini mara zote tumekuwa tukitumia zaidi ya saa moja kwa zoezi hili pekee! Ukishatoka hapa, ndipo unaenda kwenye foleni nyingine ya kuonana na Daktari ambako nako utatumia zaidi ya saa moja! Swali langu kwa uongozi wa Muhimbili, je hali hii haiwezi kutafutiwa dawa?! Je, hamuwezi kutumia cheap technolgy zilizopo ili kupunguza hali hii?! Binafsi, nahisi hakuna sababu yoyote ya msingi ya kumfanya mgonjwa akae kwenye foleni ya kusibiria kuitwa faili lake. Kwa mtizamo wangu, nahisi matumizi ya M-PESA yanaweza kuondoa tatizo hili. How? This is how i see.
  Cash Department inaweza kuwa na namba maalumu kwa ajili ya wagonjwa wanaotarajia kuja kuonana na Daktari. Kwanza, pawe na database itakayokuwa na taarifa zote muhimu za wagonjwa wanaokuja Clinic. Kwa vile kila mgonjwa anafahamu tarehe yake ya kuja, basi ashauriwe kutuma hiyo Sh.5,000/= kwa M-PESA siku moja kabla ya muda aliopangiwa. Hii maana yake ni kwamba saa sita kabla ya wagonjwa kufika, tayari kitengo husika kitakuwa kinafahamu ni wagonjwa wangapi watakuja (with very minimal deviation).
  Ili mradi hamna chochote mgonjwa anachoulizwa kwenye dirisha la malipo, then sioni ulazima wowote wa kupitia sehemu hii. Therefore, kwavile malipo yatakuwa yameshafanywa in advance kwa M-PESA, then itakuwa ni wajibu wa watumishi wanaohusika na mafaili kuchambua yale mafaili ambayo yameshalipiwa na kuyapeleka Cash section, may be six hours kabla ya muda ambao wagonjwa wamepangiwa kuja. Cashiers watafanya kazi zao kama wanavyofanya wanapokuwa face to face na mgonjwa. BUT, even more important, Cashier mmoja tu ataweza kuifanya kazi hii tena kwa ufanisi mkubwa kabisa tofauti na sasa ambapo hutumika 3 to 4 Cashiers tena wanaofanya kazi under pressure! Finally, Cashier ataambatanisha stakabadhi zote (including kopi anayopewa mgonjwa as a receipt) kwenye faili la mgonjwa tayari kwa kupelekwa kwa Daktari. Wagonjwa watapata stakabadhi zao za malipo huko huko yalikoenda mafaili yao (kwa Daktari) badala ya kupoteza zaidi ya saa nzima kusubiria kusikia akiitwa jina ili akalipie Sh. 5,000/=! Hii maana yake ni kwamba, mgonjwa akishafika, ataenda moja kwa moja kwenye foleni ya kuonana na Daktari. Jambo hili vilevile litasaidia kufahamu in advance ni wagonjwa wangapi watakuja kuonana na Daktari na hivyo kufahamu mapema ni Madaktari wangapi watahitajika siku husika.
  Similary, kwa kawaida mgonjwa akishatoka kwa Daktari anaenda kupanga foleni nyingine ya kusubiri dawa. Akishachukua dawa anaenda kwenye foleni nyingine ya kusubiri kupangiwa tarehe nyingine ya kuja kuonana na Daktari!!!!! Foleni hii ya mwisho nayo haina maana yoyote kwavile haihitaji face to face contact na mgonjwa! Na sizani kama section hii (ambyo ipo inside the same roof na Cashiers) inatumia taarifa zozote kutoka kwa Daktari ili kumpangia mgonjwa tarehe. Kama hivyo ndivyo, basi foleni hii nayo haina maana kwavile mara baada ya Cashier kumaliza kazi zake, anaweza kusogeza faili la mgonjwa kwa mpanga tarehe na mgonjwa kupangiwa tarehe kabla ya faili kupelekwa kwa Daktari. Jambo hili likifanyika, litapunguza foleni ambazo ni frustrating kutoka sehemu 4 hadi 2- I guess this can be big improvement.
  Namshukuru mungu, kwa uweza, baraka na rehema zake ameninusuru na maradhi hivyo sina uzoefu na section zingine za hapo Muhimbili. But i think, weakness za aina hii zipo kwenye vitengo vingine vile vile ambazo naamini nako zinaweza kurekebishika na ku-improve overall services.
  MIND: Mgonjwa nae ni mteja ingawaje si busara kumwambia KARIBU TENA baada ya kumuhudumia! Don’t forget, country development MUST be chained among all institutions!
   
Loading...