Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Wiki jana nilifika Muhimbili kwa mambo ya kijamii na nikawa na hamu ya kuangalia nguvu ya Rais ilivyoleta changes. Ni kweli kuna watu wanaonyesha mabadiliko ktk utendaji kazi wao, lakini kwa upande wa madaktari walio wengi, mambo bado kabisa!!
Kama alivyosema rais, sasa nimejionea wazi kwamba kuna mashine za tiba zilizoharibiwa kwa makusudi ili ile inayomilikiwa na daktari wa hapo muhimbili itengeneze biashara. Tena wanakuelekeza kwa furaha kabisa kwamba kuna mashine sehemu ..
Madaktari wa Muhimbili ni majipu. Hawaonekani kazini na hawana haraka kwa wagonjwa. Ni aibu kwamba mgonjwa bado anaweza kusubiri wodini kwa wiki nzima bila kumuona daktari. Tatizo siyo uhaba wa madaktari. Madaktari ni wengi Muhimbili lakini wanahangaika na kazi za binafsi mitaani. Ile syndrome ya kudeka haijawatoka.
Naomba nitoe pendekezo kwa waziri muhusika. Kwanza watumishi wa sekta ya afya waboreshewe maslahi yao kwa haraka. Hakuna haja ya utafiti mambo yanajulikana maana haiwezekani nesi mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 20, aishie kupata mshahara wa milioni moja na nusu tu! Haya ni matusi ktk taaluma.
Pili, wafanye Madaktari wajitambue kwamba ni waajiliwa wa Wizara. Baada ya hapo, waelewe kwamba wanaweza kufanyakazi mkoa wowote nchini. Tatu, asiyekuwa na muda wa kazi ya serikali ashauliwe kuacha kazi ili aendelee na kazi za binafsi. Baadaya hapo, Mh. Waziri hamisha madaktari hawa waende mikoa mingine. Tatizo lao ni kwamba hawaoni umuhimu wa kufika hospitali kabla ya kuhudhulia kwenye dispensari zao. Njia pekee ya hawa watu kuachana na dispensari zao ni kuwaondoa mkoani dar es salaam. Atakayeona hana sababu ya kuondoka, arudishe ajila yetu. Hakuna sababu ya kubemebeleza mtu ambaye hana huduma kwa wananchi.