Cha msingi ni kama Wazimbabwe wenyewe wameridhika na hali hiyo hakuna neno. Umri wake na kikundi kidogo cha opposition visitufanye tumwangalie vibaya huyu mzee. Na hii yote kwasababu tumejawa na demokrasia ya magharibi inayoweka vibaraka kwenye nchi zetu za kiafrika na kuruhusu unyonyaji wa rasilimali zetu.
Huyo mzee sio mnafiki, anajitahiio kadri ya uwezo wake kuitendea mema nchi yake ingawa vikwazo vya magharibi vimembana na kuzorotesha uchumi wa nchi yake. Tuwaachie wazimbabwe wenyewe ndio wenye maamuzi juu ya nchi yao