Mugabe awatuhumu marais wenzie wa Afrika kuhongwa na Morocco

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Rais Mugabe mara tu baada ya kurudi kutoka Addis Ababa, ametoa KEMEO kubwa kwa viongozi wa nchi za Kiafrika waliokubali Morroco kukubaliwa kujiunga na Umoja wa nchi za Kiafrika.

Akizungumza na vyombo vya habari vya kitaifa, rais Mugabe amewalaumu viongozi wenzake akisema, ni kwa sababu WANAPENDA sana hela ya KUPEWA na KUJENGEWA MISIKITI.

Huku akiwalaumu viongozi wenzake ambao aliwataja ni watu WASIOJUA harakati za UKOMBOZI,
wasio na principles/ MISIMAMO na wanayumbishwa na KUHONGWA HONGWA

Rais Mugabe alizidi kusema. Afadhali kama Morocco wangesema WATAIACHIA Saharawi na kuiacha IJITAWALE.
Ila kwa sasa hizo ndoto zimekwisha.
Hata hivyo rais Mugabe alisema TUTAEDELEA KUPAMBANA hadi Saharawi IWE HURU
Chanzo:The Herald Zimbabwe

..hii ni baada ya viongozi kadhaa kukubali Morocco kurudishiwa uanachama wake wa AU.

..Rais Mugabe ameshutumu kwamba viongozi waliokubaliana na uamuzi huo wamefanya hivyo kutokana na ushawishi wa FEDHA toka Morocco.

..Tanzania ni moja ya nchi zilizobariki uamuzi wa kuirudisha Morocco AU.

..Mugabe amelaumu kwamba Morocco imerudishwa ndani ya AU bila kulazimika kubadili msimamo wake kuhusu kuikalia kimabavu Sahara Magharibi.

..Msumbiji, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zimbabwe, na Algeria, ni kati ya nchi zilizopinga uamuzi wa kuirudisha Morocco ktk AU.

..kupata habari zaidi soma hapa chini:
Mugabe lashes out at African leaders for Morocco return to AU

Mugabe amesikika akilia na maraisi wenzie wa Africa kwa kuirudisha Morocco uanachama wa AU ambao hata hivyo walijivua wenyewe kupinga kuingizwa uanachama mahasimu wao wanaotaka kujitenga chini ya POLISARIO........

Tumeahidiwa viwanja vya mpira na makorokoro mengine na mfalme wa MOROCCO kwa Mugabe huo ni ufisadi...................kama ni kweli sasa hivi zoezi la kupasua majipu na huku tunahongwa limekaaje?

Kesho morocco wasipotekeleza ahadi zao kama Muammari Kadaffi ambaye alituahidi kutusaidia kujenga nyumba kwa waathirika wa mafuriko kule KILOSA akaishia na serikali yake..................tutakaa wapi na hiyo aibu.................kura imeenda huku tunatuhumiwa ufisadi.................ipo kazi!
 
Waziri kivuli wa mambo ya nje alipaswa kuhoji kama wanatujengea uwanja, msikit na fursa ya kutua Rabat moja kwa moja, sisi kama taifa tumewapa nini?

Ni makosa kutarajia handouts kutoka Moroco kana kwamba wao ndo wameendelea sana. Kama South Africa wameshindwa kutusaidia, then hakuna wa kutusaidia.
 
..hii ni baada ya viongozi kadhaa kukubali Morocco kurudishiwa uanachama wake wa AU.

..Rais Mugabe ameshutumu kwamba viongozi waliokubaliana na uamuzi huo wamefanya hivyo kutokana na ushawishi wa FEDHA toka Morocco.

..Tanzania ni moja ya nchi zilizobariki uamuzi wa kuirudisha Morocco AU.

..Mugabe amelaumu kwamba Morocco imerudishwa ndani ya AU bila kulazimika kubadili msimamo wake kuhusu kuikalia kimabavu Sahara Magharibi.

..Msumbiji, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zimbabwe, na Algeria, ni kati ya nchi zilizopinga uamuzi wa kuirudisha Morocco ktk AU.

..kupata habari zaidi soma hapa chini:
Mugabe lashes out at African leaders for Morocco return to AU
 
Nimesema jambo hili Jana kwenye uzi mmoja wa "mpenzi" mmoja wa CCM Na Serikali ya Chama hicho kuwa AU sio wamoja kabisa.Na kinachoonekana kuwa eti Ni wamoja Ni dhambi(mkakati) wao tu wa kuwabagua Wazungu linapokuja suala la ICC.Kama Mgabe amesema baadhi ya nchi zimehongwa ili kubadili misimamo yao bila shaka hata lile la ICC Kuna "mpunga" umepita kwa baadhi ya nchi toka nchi zinazoendesha jambo hili. Basi Waafrika Na tuache ujinga.
 
Mugabe mwanangu anazaliwa mpk amemaliza form four swali la rais wa Zimbabwe ni nani bado kijana ana jibu moja!..hiki kichwa ni kotapini kuingia kwa nyundo kutoka kwa nyundo!
 
..madai aliyoyatoa Mzee Mugabe ni mazito.

..na yako specific. anasema wazi kabisa Maraisi wenzake wamepewa hiki na kile.
 
Back
Top Bottom