Mufti wa Tanzania atangaza rasmi kufunguliwa kwa Madrasa za Wanafunzi wenye umri mkubwa

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi, ametangaza kufunguliwa rasmi kuanzia jana kwa madrasa, zilizofungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona (Covid 19).

Sheikh Zuberi, alitoa kauli hiyo jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu katika msikiti wa Gadafi mara baada ya swala ya Ijumaa.

Alisema kuwa madrasa zote zilizofungwa zifunguliwe na kuanza kutoa huduma kama ilivyo kuwa awali, lakini kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya.

“Lakini katika hili madrasa zitakazorudi na kuanza kutoa huduma ni zile pekee zenye wanafunzi ambao umri wao kidogo ni mkubwa na wanaojitambua, wale wadogo kabisa zitaendelea kufungwa mpaka hapo tena tutakapo toa tamko jingine,” alisema Mufti Zuberi.

Kadhalika, alisema kuwa madrasa zitakazofunguliwa kuanza kazi zinatakiwa kuchukua tahadhari zote ambazo zinaelekezwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Lazima katika madrasa hizi kuzingatia maagizo ya wataalam kama vile kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni na hili sisi kama Waislamu hatutashindwa kwa kuwa Muislamu na kunawa ni jambo la kila siku,” alisema.

Alipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kufanikisha kupitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Maoni yangu

Wanajukwaa hapa namuona shekhe mkuu wa Tanzania, shekhe Zuberi UTV ameruhusu kuanza kwa madrasa nchini.

Masomo haya yalisimamishwa na Waziri Mkuu march 17mwaka huu na hapo awali tuliambiwa wenye mamlaka ya kutangaza shugli zote zilizo simama kurejerea ni rais,waziri mkuu ,waziri wa afya au msemaji wa serkali sasa hii jeuri ya shekhe zuberi ameitoa wapi.

Madrasa Watoto hujazana sana kuliko hata shule za msingi maana hawa hukaa chini tena kwa makundi wakisoma kwa sauti hii inamaana kama kuna mwenye korona hakuna wa kutoka salama

USSR
 
Pale kwa mtoro walijifanya kufunga msikiti wakaambiwa na mkuu mwenyewe msikiti wenyewe mnaufunga utafikiri mliujenga, siku iliyofuata tu mbiombio wakaufungua.

Corona tulishafanya mpk pate after pate kuifurahia maana ilishaisha bongo,acha madogo wakapate ilim.
 
Wanajukwaa hapa namuona shekhe mkuu wa Tanzania, shekhe zuberi UTV ameruhusu kuanza kwa madrasa nchini.

Masomo haya yalisimamishwa na waziri mkuu march 17mwaka huu na hapo awali tuliambiwa wenye mamlaka ya kutangaza shugli zote zilizo simama kurejerea ni rais,waziri mkuu ,waziri wa afya au msemaji wa serkali sasa hii jeuri ya shekhe zuberi ameitoa wapi.

Madrasa watoto hujazana sana kuliko hata shule za msingi maana hawa hukaa chini tena kwa makundi wakisoma kwa sauti hii inamaana kama kuna mwenye korona hakuna wa kutoka salama

USSR
Tulia wewe, Usitupangie cha kufanya
 
Hii ndio Tanzania 🇹🇿 ...BAKWATA NI KITENGO NDANI YA JUMUIYA YA WAZEE WA KISARAWE ... hii ndio BONGO
 
Si mnatangazia dunia kuwa mmeitokomeza corona? Mchecheto wa nini MATAGA?
 
Wanajukwaa hapa namuona shekhe mkuu wa Tanzania, shekhe zuberi UTV ameruhusu kuanza kwa madrasa nchini.

Masomo haya yalisimamishwa na waziri mkuu march 17mwaka huu na hapo awali tuliambiwa wenye mamlaka ya kutangaza shugli zote zilizo simama kurejerea ni rais,waziri mkuu ,waziri wa afya au msemaji wa serkali sasa hii jeuri ya shekhe zuberi ameitoa wapi.

Madrasa watoto hujazana sana kuliko hata shule za msingi maana hawa hukaa chini tena kwa makundi wakisoma kwa sauti hii inamaana kama kuna mwenye korona hakuna wa kutoka salama

USSR
Kunywa bia mkuu utulie
 
Shida so sheikh mkuu

Shida wazazi wanaokubali watoto wao waende ilhali wanajua kuna corona.....
 
Wameshindwa kupukutika huku mtaani tunakosondekwa kwny madaladala sembuse darasani? Ni muda muafaka sasa na shule za awali zifunguliwe make imethibitika vijimafua vya corona havina madhara kwa binadamu
 
MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi, ametangaza kufunguliwa rasmi kuanzia jana kwa madrasa, zilizofungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona (Covid 19).

Sheikh Zuberi, alitoa kauli hiyo jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu katika msikiti wa Gadafi mara baada ya swala ya Ijumaa.

Alisema kuwa madrasa zote zilizofungwa zifunguliwe na kuanza kutoa huduma kama ilivyo kuwa awali, lakini kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya.

“Lakini katika hili madrasa zitakazorudi na kuanza kutoa huduma ni zile pekee zenye wanafunzi ambao umri wao kidogo ni mkubwa na wanaojitambua, wale wadogo kabisa zitaendelea kufungwa mpaka hapo tena tutakapo toa tamko jingine,” alisema Mufti Zuberi.

Kadhalika, alisema kuwa madrasa zitakazofunguliwa kuanza kazi zinatakiwa kuchukua tahadhari zote ambazo zinaelekezwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Lazima katika madrasa hizi kuzingatia maagizo ya wataalam kama vile kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni na hili sisi kama Waislamu hatutashindwa kwa kuwa Muislamu na kunawa ni jambo la kila siku,” alisema.

Alipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kufanikisha kupitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21.
 
Madrasa Watoto hujazana sana kuliko hata shule za msingi maana hawa hukaa chini tena kwa makundi wakisoma kwa sauti hii inamaana kama kuna mwenye korona hakuna wa kutoka salama
SIKU NYINGINE UKITAKA KUTOA MAONI AU CHALENJI YOYOTE, KWANZA SOMA VIZURI ULICHOKIPOST KABLA HUJAKURUPUKA.

ANGALIA PARAGRAPH HII KWANZA...
"“Lakini katika hili madrasa zitakazorudi na kuanza kutoa huduma ni zile pekee zenye wanafunzi ambao umri wao kidogo ni mkubwa na wanaojitambua"

PITIA KWANZA MANENO YAKO NA MANENO HAYO KISHA TOA MAONI UPYA.
 
Back
Top Bottom