Mufindi tumeumizwa vya kutosha sasa yatosha

mr culture

Senior Member
Mar 23, 2019
111
230
Inayoonekana kwenye picha ni barabara ya wilaya ya Mufindi yenye majimbo mawili yanayo wakilishwa na wabunge wa chama tawala Kusini na Kaskazini toka mfumo wa vyama vingi kuingia nchini CCM ndio imetawala majimbo yote na kuongoza halmashauri na ni majimbo yenye mchango mkubwa sana kwa taifa letu.

Ikumbukwe wilaya ya mufindi imekuwa ikiongoza kwenye ukusanyaji wa mapato ukiachana na Ilala ya Dar,Pamoja na mchango huo wananchi wa wilaya hii wamekuwa wakiteseka kwa muda wote. Leo ni siku ya nane barabara haipitiki,wananchi wanateseka kweli kweli hivi hawa wananchi waliikosea nini CCM!

Na ni hawa wanojinasibu kwenye majimbo ya upinzani eti mkitaka maendeleo chagueni CCM haya ndio maendeleo mnayoyaleta kweli? Barabara hakuna,maji hakuna kodi mnakusanya kwanini hamrudishi fadhira?

Lugola,Mgimwa(MP) nadhani mtakuwepo kwenye jukwaa hili timizeni wajibu wenu tafadhari.

IMG-20190515-WA0022.jpeg
 
ni mbovu mkuu,mvua ikinyesha kidogo ndio hali kama unavyoiona hakuna usafiri unaopitika ikumbukwe huku kuna viwanda vya kutosha vya chai na karatasi na uzalishaji mkubwa wa miti lakini hakuna kinachofanyika
Haipitiki nini sababu mkuu?
 
ni mbovu mkuu,mvua ikinyesha kidogo ndio hali kama unavyoiona hakuna usafiri unaopitika ikumbukwe huku kuna viwanda vya kutosha vya chai na karatasi na uzalishaji mkubwa wa miti lakini hakuna kinachofanyika
Dah!
Hukumu ya mahakama kuu muitumie vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom