Mufindi na umaskini wa kutupwa

Mufindi na umaskini wa kutupwa

wadabali

Member
Joined
Jan 20, 2013
Posts
9
Reaction score
1
Awali ya yote namshukuru mungu kwa kunijalia afya njema na kunipa fursa ya kupata elimu ambayo bila shaka ninalo deni kwa wananchi wa Mufindi,mimi nimezaliwa kijiji cha kihanga,wilaya mufindi,mkoa wa Iringa leo nitagusia kwa ufupi mambo matatu ambayo yapo mufindi lakini bado watu wake ni maskini.

(1)SHAMBA LA MSITU WA SAOHILL
(2)SHAMBA LA CHAI UNILIVER
(3)KIWANDA CHA KARATASI MGOLOLO(MPM)

Bila woga nataja hadharani kuwa ufisadi uliokidhiri ktk shughuli hizo muhimu hazijaweza kuwanufaisha wananchi wa maeneo husika kutokana na vingozi wakubwa na wilaya kuingia mikataba ya kifisadi na kujimilikisha rasilimali kwa njia isiyo halali mfano WAZIRI LUKUVI MB(ISIMANI) anamiliki kitalu cha miti kupitia kiwanda cha ustas karibu na kiwanda cha nguzo za umeme ambacho kinamilikiwa na MERAB KIIJIJI CHA KIHANGA.

Mkuu wa wilaya EVARISTI KALALU ana kibali kupasua mbao isivyo halali,pia amejimilikisha ardhi kimabavu ktk kijiji cha Mapanda.
Kiwanda cha Mgololo limekuwa shamba la bibi na amemiliki MNORWAY miaka(90),wafanyakazi hawajalipwa stahiki zoa tangu kubinafsishwa kiwanda miaka zaidi ya kumi na mbili sasa.

Mashamba ya chai balaa tupu mshaharaTsh 3000@siku mabadiliko ni sasa
 
Ndio wajue faida ya kuchagua CCM.......Kidumu Chama Cha Mapinduzi Mufindi........
 
Ni thread nzuri ingawa kuonesha kuwa haturidhiki na viongozi waliopo ni kuwatupilia mbali na kuchagua viongozi wazalendo,sisi wanamufindi ni wakujilaumu kwani tuliwahi kumchagua mbunge mmoja na aliongoza miaka 40 bila jipya la kujivunia.
 
kamwene mnyalukolo, naungana na ww 110% , mngai na serikari yake ndipo alipo tufikisha na sisim yao kaka sisi wengine tupo mbali ila tunaunga na wewe kutafuta tiba ya ugonjwa huu wa ufisadi wilayani kwetu. Dawa ni kuing'oa ccm na takataka zake zote kwa mkoa wairinga.
 
Naanza kuamini kua, upo uhusiano wa karibu sana wa UJINGA na kuichagua ccm, maeneo mengi yenye umasiki wa kutisha pamoja na ujinga ndiko huko huko ccm hua wanapata ushindi wa kishindo! Naelewa pia kua kwanini magamba huchukia sana wanapoona CDM inatoa elimu ya uraia kwa wananchi, mleta uzi, pamoja na kukuonea huruma wewe na wakazi wenzio, nenda zaidi, waelimishe hao wana Mufindi kua, "Kuna uhusiano mkubwa na wa karibu kati ya kura yao wakati wa uchaguzi na maisha wanayoishi"
 
yaani kiukweli mleta uzi nakuunga mkono asilimia zote!
...hivi m4c huko haijawahi pita?
Coz bado kuna tatizo kubwa la elim kwa hao wananchi!
 
Back
Top Bottom