Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,547
- 47,200
Kwakweli nimeguswa swana na namna ndugu zetu wanavyokua treated nje ya nchi na especially matukio mawili ya hivi karibuni nchini Msumbiji na Malawi.
Katika nchi ambazo zipo very lenient kwa maswala ya uhamiaji na hasa Raia wa kigeni nadhani tunaongoza kwa afrika.
Binafsi nimeshihudia in a number at times Raia wa kigeni akiwa na Sauti hata kushinda mwenyeji. Unakuta baadhi ya wenyeji wananyenyekea wageni kuliko hata ndugu zao wa kitanzania.
Kwa muda mrefu Tanzania imekua kimbilio la wahamiaji kutoka nchi mbali mbali za ukanda huu wa afrika mashariki, kati na kusini kutokana na mazingira mazuri yenye kujali utu wa mtu.
Kinachotokea sasa ni muendelezo wa aina mpya ya siasa za kidunia za kila Taifa kuanza kujali maslahi yake. Ilianza kwa Uingereza kujitoa EU, Ikafuata na siasa za Trump za kuweka Marekani kwanza, hali inayotoa tafsiri kwamba kila nchi inahitaji kujali Raia wake kwanza kuliko raia wengine.
Ingawa Watanzania tumekua na utaratibu wa ukarimu kwa wenzetu, lakini hali kwa sasa imebadilika, na kila nchi sasa inazidi kuimarisha sera zake za uhamiaji ili kulinda raia wake.
Ongezeko la watu pamoja na uchache wa rasilimali ambazo zinazidi kupungua ukilinganisha na miaka ya nyuma, inaweza kuwa sababu ya kuanza kutumika kwa sera hii kwa sasa.
Ni wazi kwamba hata sisi watanzania, inatubidi kubadilika na kuachana na unyonge wa kutetemekea wageni kwa kuzidisha makali ya sheria za uhamiaji ili kumlinda mtanzania na kufaidika kwa rasilimali zake.
Hakuna haja ya kuajiri Raia wa kigeni kwa maelfu kufanya kazi ambazo hata Raia wa kitanzania wanaweza kufanya.
Nadhani uhamiaji wanalojukumu la kufanya uhakiki kujiridhisha kwamba Utaratibu wa kuajiri Raia wa kigeni katika baadhi ya makampuni ulifuatwa.
Zile zama za kubembelezana zimepita. Ni wakati wa kuamka na kulinda vya kwetu.