Muendelezo wa kuua sekta binafsi, wakandarasi wa umeme kuanza kusoma namba.

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,895
19,069
Katika muendelezo wa kuua sekta binafsi sasa wakandarasi wa umeme wataanza kuisoma namba taratibu.

Kwanza serikali imeamua kuipa idara ya TEMESA kazi zote za umeme zinazohusu majengo ya serikali, electrical contractor katika majengo yote ya serikali ni TEMESA.

Serikali imeenda mbali zaidi kutaka kazi zote za ujenzi wa umeme ambazo watu walikua wanafanya kwa niaba ya Tanesco(ukiacha miradi ua REA) ifanywe na Tanesco wenyewe.

Hapo kabla kama mtu ulikua unahitaji umeme ulikua unaruhusiwa kuipatia kampuni yoyote ya umeme inayotambulika hiyo kazi ikufanyie alafu tanesco wataitoza kampuni hiyo pesa kidogo kama supervision cost katika kazi hiyo ya kukuletea umeme nyumbani kwako/eneo lako.

Kwa mfano unataka kupeleka umeme eneo ambalo halina umeme na haliko katika mipango ya tanesco au tanesco hawana vifaa vya kukufanyia kazi hiyo unaruhusiwa kuipatia kampuni inayotambulika hiyo kazi ya kujenga huo mradi, sasa imeamuriwa kazi hizo zote zitafanywa na Tanesco wenyewe.

Kw kufanya hivyo kampuni zote za umeme ambazo zilikua zinategemea kazi kama hizo zitafte kazi nyingine, serikali inataka kazi zote zinazohusu idara ya serikali zifanywe na taasisi za serikali.

Sijui kama serikali inajua madhara ya kuipuuza sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi. Yetu macho.
 
Ile issue ya nenda uje kesho hapo ndio mahali pake. Kama ukilipa service line tanesco mpaka upate umeme huchukua mwaka mmoja plus itakuwa kupewa miradi mingine??
 
Katika muendelezo wa kuua sekta binafsi sasa wakandarasi wa umeme wataanza kuisoma namba taratibu.

Kwanza serikali imeamua kuipa idara ya TEMESA kazi zote za umeme zinazohusu majengo ya serikali, electrical contractor katika majengo yote ya serikali ni TEMESA.

Serikali imeenda mbali zaidi kutaka kazi zote za ujenzi wa umeme ambazo watu walikua wanafanya kwa niaba ya Tanesco(ukiacha miradi ua REA) ifanywe na Tanesco wenyewe.

Hapo kabla kama mtu ulikua unahitaji umeme ulikua unaruhusiwa kuipatia kampuni yoyote ya umeme inayotambulika hiyo kazi ikufanyie alafu tanesco wataitoza kampuni hiyo pesa kidogo kama supervision cost katika kazi hiyo ya kukuletea umeme nyumbani kwako/eneo lako.

Kwa mfano unataka kupeleka umeme eneo ambalo halina umeme na haliko katika mipango ya tanesco au tanesco hawana vifaa vya kukufanyia kazi hiyo unaruhusiwa kuipatia kampuni inayotambulika hiyo kazi ya kujenga huo mradi, sasa imeamuriwa kazi hizo zote zitafanywa na Tanesco wenyewe.

Kw kufanya hivyo kampuni zote za umeme ambazo zilikua zinategemea kazi kama hizo zitafte kazi nyingine, serikali inataka kazi zote zinazohusu idara ya serikali zifanywe na taasisi za serikali.

Sijui kama serikali inajua madhara ya kuipuuza sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi. Yetu macho.
Kwaiyo mkuu tukatafute majembe tukalime?
 
Hii inasikitisha sana!! Ukicheka na nyani utavuna mabua.... Very soon tutavuna mabua....

Muda ndio hakimu wa yote.
 
Back
Top Bottom