Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa

Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Mabibi na mabwana,

Mtanzania mwenzetu aliyeondoka akiwa "mfu", hatimaye amerejea leo salama salimini nyumbani Tanzania.

Jambo la heshima kubwa sana kwetu sisi sote ambao ni wana halisi wa nchi hii na wazalendo.

Tumeshinda!

Tumeshinda sote tuliofanikisha kurejea kwa mwana huyu wa nchi hii salama na kwa amani. Tafsiri halisi ya kuwa sote tu wajenzi wa nyumba moja. Yaani Tanzania.

Kesho inshallah kwa umoja wetu tena, kama Watanzania na tukamuage kwa pamoja Mzee wetu Rais mstaafu Mkapa (RIP) pale Uhuru, ambaye hakubahatika hata kumwona mwana huyu akirejea nyumbani.

Yaliyopita si ndwele, baada ya mazishi tujipange kuganga yajayo.

Kwako mheshimiwa rais wetu: kwa hakika haupo muda mzuri wa maridhiano na kuponya nchi hii kuliko huu.

Sentensi yako moja tu mkuu, itaifanya Tanzania yote akiwamo Mh. Lissu kuripuka kwa vifijo na vigeregere vya:

"Magufuli tosha!"

Kuyatambua madhila aliyoyapitia mja wake mola huyu, kumkaribisha nyumbani na neno moja la "pole" tu, litabeba uchawi wote unaohitajika.

Eeh mola wetu, hebu ukatujalie kuweza kuyaona yasiyoonekana na hasa kuudhihirisha ushindi wetu huu kwa wote wale wasioitakia mema nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi kuna mtu anaweza kunielewesha ni kwanini watu wanaona Magufuli na Polisi leo wamefanya "jambo la maana"?!

Ni kwamba tunadhani Tundu Lissu alitakiwa kukamatwa pale Airport, au?! Ni kama tunadhani hivyo, kwa sababu zipi?!

Ni kwamba tunasahau hata hiyo safari ya Belgium Lissu hakutakiwa kwenda, kwa sababu sababu zilizompeleka huko ni matunda ya uovu wa utawala, au?!

And guys, let me put this clear... pale alipo Tundu Lissu is a radioactive material lakini wala haimaanishi kwamba yupo salama mbele ya madhalimu tunaodhani leo wamefanya jambo jema sana!!
 
Hivi kuna mtu anaweza kunielewesha ni kwanini watu wanaona Magufuli na Polisi leo wamefanya "jambo la maana"?!

Ni kwamba tunadhani Tundu Lissu alitakiwa kukamatwa pale Airport, au?! Ni kama tunadhani hivyo, kwa sababu zipi?!

Mkuu, pasipo na kupepesa maneno. Ile kukubali busara tu kutamalaki ni jambo jema sana.

Mara ngapi busara imekuwa ikiwekwa pembeni?

Labda kama tunataka kuwa wageni wa hizi ndivyo sivyo za hapa kwetu?
 
Mkuu, pasipo na kupepesa maneno. Ile kukubali busara kutamalaki ni jambo jema sana.

Mara ngapi busara imewekwa pembeni labda kama tunataka kuwa wageni wa ndivyo sivyo za hapa kwetu?
Hata mlevi, akiona nyumbani pamekuja wageni, ataacha au kupunguza kulewa kwa muda!!! Hata mlevi, akiona nyumbani pana msiba, ataacha au kupunguza ulevi kwa muda!

Don't be blinded with these few hours!!
 
Hivi kuna mtu anaweza kunielewesha ni kwanini watu wanaona Magufuli na Polisi leo wamefanya "jambo la maana"?!

Ni kwamba tunadhani Tundu Lissu alitakiwa kukamatwa pale Airport, au?! Ni kama tunadhani hivyo, kwa sababu zipi?!
Sasa hivi mzee anaanza kushaurika na kwa kiwango kikubwa anabadilika mdogo mdogo unajua nguzo muhimu kwake imeondoka ile nguzo ndio ilikuwa inampa nguvu nguzo ilikuwa unazibiti makundi ndani ya chama na yeye huku uraiani anazibiti wapinzani ndio maana alikuwa anajiachia Sana na kauli tata mara mabeberu, mara yeye bora, mara nakutumbua. Sasa nguzo imeondoka atakubari kushaurika na kuwafanyia wapinzani mazuri zaidi ili amalize vizur kutawala
 
Hata mlevi, akiona nyumbani pamekuja wageni, ataacha au kupunguza kulewa kwa muda!!! Hata mlevi, akiona nyumbani pana msiba, ataacha au kupunguza ulevi kwa muda!

Don't be blinded with these few hours!!

Mkuu nakubaliana nawe.

Unampongeza huyo yakhe!

Ndiyo maturity hiyo!
 
Kabisa huu ni mwanzo mzuri sana kwa siasa za ukombozi za nchi yetu, sikuamini macho yangu kwa namna watanzania walivyojitokeza kumpokea shujaa Lissu. Ni pigo kubwa mno kwa waliokuwa na nia ya kumuua.
Makonda alitaman leo angekuwa mkuu wa mkoa wa Dsm
 
Makonda alitaman leo angekuwa mkuu wa mkoa wa Dsm
Huyo sasa ni kama nyani, akija mtaani tu haponi. Tunaambiwa alikuwa anafanya mazoezi Morogoro baada ya jana kutoka kufanya unyama wa kumuua Lissu huko Dodoma. Yaani huyu damu yake iko mikononi mwa watu.
 
Sasa hivi mzee anaanza kushaurika na kwa kiwango kikubwa anabadilika mdogo mdogo unajua nguzo muhimu kwake imeondoka ile nguzo ndio ilikuwa inampa nguvu nguzo ilikuwa unazibiti makundi ndani ya chama na yeye huku uraiani anazibiti wapinzani ndio maana alikuwa anajiachia Sana na kauli tata mara mabeberu, mara yeye bora, mara nakutumbua. Sasa nguzo imeondoka atakubari kushaurika na kuwafanyia wapinzani mazuri zaidi ili amalize vizur kutawala
Yaani hivi sasa anashaurika kwavile Mkapa hatunae?! Man, you can't be serious!!! Magu isn't that stupid to wash his dirt linen in public! Wait and see kama hujasikia imetolewa hati ya kukamatwa Tundu Lissu... sasa hilo likitokea sijui kutakuwa na tofauti gani na endapo angekamatwa leo, zaidi tu ya endapo wangefanya hivyo leo, ingewachafua sana wao wenyewe!

These people walishafahamu in advance kwamba hata international media zingekuwa zinafuatilia kurejea kwa TL to see what would happen!! Matokeo yake, ingekuwa ni breaking news ambayo ingesambaa kama moto wa kifua throughout the world!!
 
Lakini hatuwezi kusema "ameacha ulevi"!! Anachosubiri ni wakti tu aliendeleze!!

Tutangulize nia njema.

Mtanzania mwenzetu karejea kwa amani bila kubugudhiwa, hilo la heri.

Tuupe muda. Tumzike mzee wetu kisha tugange yajayo.

Yaliyopita si ndwele. Tuweke bunduki zetu chini tujenge nchi.

Wanasema ndugu wawili wakigombana chukua jembe ukalime. Siku wakipatana chukua kapu ukavune.

Tuchukue makapu kuvuna, nchi ipone.

Mungu ni muweza wa yote. Hili mbona siyo Corona?

Hili ni utashi tu ambao uko mikononi mwetu?

Yakiwezejana, mbona "Magufuli tosha!"
 
Mkuu, pasipo na kupepesa maneno. Ile kukubali busara tu kutamalaki ni jambo jema sana.

Mara ngapi busara imekuwa ikiwekwa pembeni?

Labda kama tunataka kuwa wageni wa hizi ndivyo sivyo za hapa kwetu?
Chige ana hoja. Hatujui, pengine Magu kapigwa mkwara na mabeberu? Kwamba kama walioandamana leo wangesambaratishwa kama polisi walivyoahidi, mabeberu wageondoa jina la Tanzania kwenye orodha ya nchi za uchumi wa kati? Imajini hiyo tu ingemuacha wapi Magu?
Lakini pengine waliogopa kuaibika, wageni wengi sasa wanakuja hapa nchini sbb ya msiba.
 
Magufuli tosha!"

Kuyatambua madhila aliyoyapitia mja wake mola huyu, kumkaribisha nyumbani na neno moja la "pole" tu, linabeba uchawi wote unaohitajika.
Mmh! Sijui kama anaweza kutoa pole. Huyu jamaa siyo mpatanishi by nature, bali ni mpenda shari na visasi. Akitoa pole jua litakoma kuchomoza.
 
Back
Top Bottom