MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Mpaka sasa kwa maisha ya watanzania wa kawaida/Wanyonge hali inazidi kua mbaya, ugumu wa maisha unazidi kuongezeka maradufu, gharama za vitu zinapaa kila Siku, mabenki yanapandisha riba kiholela! Yaani in mafadhaiko kweli kwa kila mtanzania wakati huu.Kwa kiasi kikubwa wananchi nyuso zao zinatia huruma na zenye kukata tamaa haswaa.
Watumishi wa umma hakuna annual increments wala hakuna promotions pamoja na makato makubwa kutoka bodi ya mikopo kwa wale waliwahi kunufaika na mikopo. Mikopo ya elimu ya juu imekua tatizo, wanafunzi wanalia vilio vya kutia huruma pamoja kutoka familia maskini zisizojiweza. Tatizo la ajira sio la kuzungumzia maana hapa hata wenye vyama na wasio na vyama wote hali ni ngumu.
SWALI LA KUJIULIZA,
Pamoja na jitihada zote zinazosemwa kila siku huku tunaelekea kuimaliza nusu ya kwanza ya awamu ya tano, changes chanya zinazomgusa moja kw moja mwananchi wa kawaida ziko wapi? Tulizungumzia viwanda kama motto wetu wa kitaifa awamu ya tano, je, ni product ipi mpya ambayo sasa tunaweza kujivunia tuseme ni jitihada za awamu hii na ni dalili njema kwa tunakoelekea?
Nakumbuka awamu ya nne miaka ya 2006 kulikua na mchaka mchaka wa ujenzi wa shule za kata, tuliona mapori yakifyekwa kila kata kuanzisha ujenzi wa shule za upili. Tuliona vijana waliokua wamemaliza kidato cha sita wakineemeka na ajira za harakaharaka kwenda mafunzo ya ualimu ya mwezi mmoja ambao pia kimsingi tuliona faida zake, tuliona walimu wenye viwango vizuri vya elimu waliokua wakifundisha shule za msingi wakisogezwa kusukuma kurugudumu upande wa sekondari.Lakini hata leo ukitoka mtaani tunaposema vijana wengi wenye shahada wako mtaani hawana ajira tutambue kua ndizo hizo products za miaka ya 2005.
Mimi sio mwanauchumi wala mtunga sera lakini kwa harakaharaka ninaona kunahitajika jitihada za makusudi za kiushauru au kuunyosha msitari unaoonesha dalili za kupinda ikiwa bado ni mapema.
Nchi imo kwenye mfumo wa vyama vingi,huwezi kujiwekea guarantee ya majukumu yako kwa kuzigwa kazi zako kaika mafungu huku ukijumuisha muda ambao bado una kampeni na uchaguzi mbele yake(ni hisia), Kwakweli hali hii inaweza kuwatia wananchi wasiwasi juu ya maisha yao mbeleni.