Muda unakimbia, ni kipi cha kujivunia awamu hii ya tano?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Mpaka sasa kwa maisha ya watanzania wa kawaida/Wanyonge hali inazidi kua mbaya, ugumu wa maisha unazidi kuongezeka maradufu, gharama za vitu zinapaa kila Siku, mabenki yanapandisha riba kiholela! Yaani in mafadhaiko kweli kwa kila mtanzania wakati huu.Kwa kiasi kikubwa wananchi nyuso zao zinatia huruma na zenye kukata tamaa haswaa.

Watumishi wa umma hakuna annual increments wala hakuna promotions pamoja na makato makubwa kutoka bodi ya mikopo kwa wale waliwahi kunufaika na mikopo. Mikopo ya elimu ya juu imekua tatizo, wanafunzi wanalia vilio vya kutia huruma pamoja kutoka familia maskini zisizojiweza. Tatizo la ajira sio la kuzungumzia maana hapa hata wenye vyama na wasio na vyama wote hali ni ngumu.

SWALI LA KUJIULIZA,
Pamoja na jitihada zote zinazosemwa kila siku huku tunaelekea kuimaliza nusu ya kwanza ya awamu ya tano, changes chanya zinazomgusa moja kw moja mwananchi wa kawaida ziko wapi? Tulizungumzia viwanda kama motto wetu wa kitaifa awamu ya tano, je, ni product ipi mpya ambayo sasa tunaweza kujivunia tuseme ni jitihada za awamu hii na ni dalili njema kwa tunakoelekea?

Nakumbuka awamu ya nne miaka ya 2006 kulikua na mchaka mchaka wa ujenzi wa shule za kata, tuliona mapori yakifyekwa kila kata kuanzisha ujenzi wa shule za upili. Tuliona vijana waliokua wamemaliza kidato cha sita wakineemeka na ajira za harakaharaka kwenda mafunzo ya ualimu ya mwezi mmoja ambao pia kimsingi tuliona faida zake, tuliona walimu wenye viwango vizuri vya elimu waliokua wakifundisha shule za msingi wakisogezwa kusukuma kurugudumu upande wa sekondari.Lakini hata leo ukitoka mtaani tunaposema vijana wengi wenye shahada wako mtaani hawana ajira tutambue kua ndizo hizo products za miaka ya 2005.

Mimi sio mwanauchumi wala mtunga sera lakini kwa harakaharaka ninaona kunahitajika jitihada za makusudi za kiushauru au kuunyosha msitari unaoonesha dalili za kupinda ikiwa bado ni mapema.

Nchi imo kwenye mfumo wa vyama vingi,huwezi kujiwekea guarantee ya majukumu yako kwa kuzigwa kazi zako kaika mafungu huku ukijumuisha muda ambao bado una kampeni na uchaguzi mbele yake(ni hisia), Kwakweli hali hii inaweza kuwatia wananchi wasiwasi juu ya maisha yao mbeleni.
 
Ni kutokana tu na mitandao kwamba kila mtu ana Uhuru wa kuandika akitakacho..zaidi baadhi wanasukumwa na roho ya upinzani..
Kwanza haijawahi kutokea Tanzania katika wakati wowote ule wa uongozi watu wakasema huu ndio..
Alipoingia Mkapa watu walisema hali ni ngumu mno..bora hata Mwinyi angerudi tena..baada ya Mkapa akaingia Jk..watu wakasema katurudisha nyuma sana..hali ni ngumu..nchi inajiendesha yenyewe.. Mkapa alijificha kwa muda mrefu mara akaanza kujitokeza na kushangiliwa na jk akaonekana hafai..akaitwa Vasco da gama, mzembe na dhaifu..tukataka mabadiliko haya na tukapiga deki hadi lami..hakuna aliyesema tuna maisha mazuri kwa sasa..jk akaondoka.
Ameingia Magufuli kabeba Yale tulikuwa tukiyalilia na kuiaminisha dunia tunayahitaji..
Unaposimama na kuhoji nini kimefanyika inabidi tukufahamu vizuri unavyoongea ili tujue unachofikiria..inawezekana Upo mahali ambapo hupati taarifa, au sio mfuatiliaji au unataka kupoteza muda humu ili mradi uonekane umeandika kitu..
 
Hakuna lolote la maana lililofanyika..

kwangu mimi hata ukijenga mafly-over.kibao, ukajenga chato intern. airpot, na kuhamia Dom...haina maana kama maisha ya watu ni ya hovyo kweli kweli..

Watu hawana furaha, watu wamenyong'onyea mitaani hawajui na hawana uhakika na kesho watakula nini...familia zilizokua zinapata milo mitatu sasa baadhi wanapata milo miwili ama mmoja..

Watumishiwa serikali ndo usiseme kabisaa, ni majanga matupu..hawana amani maofisini...hofu imetanda.hakuna kiongozi anaewajali...ilimradi umefika kazini ukasaini, basi inatosha

Hakuna mwenye uchungu na kazi tena...kwa sabb hakuna anaekuthamini, sasa kwa nini nihangaike na kazi za umma?

yote haya yamesababishwa na FARU YOHANA..Chuki, visasi, roho mbaya, vitisho havijawahi kufanikisha jambo lolote...
 
Ni kutokana tu na mitandao kwamba kila mtu ana Uhuru wa kuandika akitakacho..zaidi baadhi wanasukumwa na roho ya upinzani..
Kwanza haijawahi kutokea Tanzania katika wakati wowote ule wa uongozi watu wakasema huu ndio..
Alipoingia Mkapa watu walisema hali ni ngumu mno..bora hata Mwinyi angerudi tena..baada ya Mkapa akaingia Jk..watu wakasema katurudisha nyuma sana..hali ni ngumu..nchi inajiendesha yenyewe.. Mkapa alijificha kwa muda mrefu mara akaanza kujitokeza na kushangiliwa na jk akaonekana hafai..akaitwa Vasco da gama, mzembe na dhaifu..tukataka mabadiliko haya na tukapiga deki hadi lami..hakuna aliyesema tuna maisha mazuri kwa sasa..jk akaondoka.
Ameingia Magufuli kabeba Yale tulikuwa tukiyalilia na kuiaminisha dunia tunayahitaji..
Unaposimama na kuhoji nini kimefanyika inabidi tukufahamu vizuri unavyoongea ili tujue unachofikiria..inawezekana Upo mahali ambapo hupati taarifa, au sio mfuatiliaji au unataka kupoteza muda humu ili mradi uonekane umeandika kitu..
Jibu hoja wewe acha kuruka ruka na kuleta mipasho kama pombe na bashite , tatizo hapa siyo Mwinyi, Mkapa, Kikwete wala Makomeo tatizo kubwa kuliko yote nchi hii ni ccm, na hakuna siku mabadiliko chanya tutakuja kuyapata kupitia ccm hilo never kabisa vinginevyo itakuwa kila utawala ni afadhali ya jana
 
Usime watu wako hoi nyuso zinatia huruma,! Jisemee mwenyewe, tatizo lako au lenu nyie wachache lisiwe la watanzania wote. Kwanza jiulize mchango wako umekuwa nini nchini humu?. Au ni mafundi wa kushinda kwenye mitandao na kukashifu kila Rais anaekuja? Hivi ni Rais yupi mmewacha hana dosari?na nyie michango yenu imekuwa nini miaka yote hiyo? Mwalimu Nyerere alisema It can be done play your part". Hakuna Rais duniani aliekuwa perfect kwa kila kitu yapo mazuri Yake na mabaya Yake. Sifu panapo stahili, na kosoa panapo stahili na toa maelezo ulivyo toa mchango wako au toa ushauri.
 
Kama mabaya yake yanazidi mazuri tusemeje?
 
Jibu hoja wewe acha kuruka ruka na kuleta mipasho kama pombe na bashite , tatizo hapa siyo Mwinyi, Mkapa, Kikwete wala Makomeo tatizo kubwa kuliko yote nchi hii ni ccm, na hakuna siku mabadiliko chanya tutakuja kuyapata kupitia ccm hilo never kabisa vinginevyo itakuwa kila utawala ni afadhali ya jana
Jk hamjammiss tena??
 
Ni kutokana tu na mitandao kwamba kila mtu ana Uhuru wa kuandika akitakacho..zaidi baadhi wanasukumwa na roho ya upinzani..
Kwanza haijawahi kutokea Tanzania katika wakati wowote ule wa uongozi watu wakasema huu ndio..
Alipoingia Mkapa watu walisema hali ni ngumu mno..bora hata Mwinyi angerudi tena..baada ya Mkapa akaingia Jk..watu wakasema katurudisha nyuma sana..hali ni ngumu..nchi inajiendesha yenyewe.. Mkapa alijificha kwa muda mrefu mara akaanza kujitokeza na kushangiliwa na jk akaonekana hafai..akaitwa Vasco da gama, mzembe na dhaifu..tukataka mabadiliko haya na tukapiga deki hadi lami..hakuna aliyesema tuna maisha mazuri kwa sasa..jk akaondoka.
Ameingia Magufuli kabeba Yale tulikuwa tukiyalilia na kuiaminisha dunia tunayahitaji..
Unaposimama na kuhoji nini kimefanyika inabidi tukufahamu vizuri unavyoongea ili tujue unachofikiria..inawezekana Upo mahali ambapo hupati taarifa, au sio mfuatiliaji au unataka kupoteza muda humu ili mradi uonekane umeandika kitu..
Wakati wa Mkapa pia watu walimtamani mwinyi?
 
Kisukari hakitibiki kwa dakika moja.Au Dodoma haitajengwa kwa siku moja. Watanzania muda wa mmalumbano tunawezajenga viwanda vingi kwa miezi 3
 
Najivunia mkuu wangu wa mkoa anayeniongoza ni mwana zero mwenzangu hata mimi O level nilipiga fafafa
 
Tunajivunia misamiati mipya:
1. I WISH I KUDU BE...
2. SIJARIBIWI
3. KA, TA
4. WATCH IT
5. KUNA MAVYEO MEEENGI
6.........
 
Tunajivunia udhihirisho kuwa kwenye kila watu wanne mmoja ana kichaa.

Hii ilishamiri enzi za Mkapa na Kikwete na ndiyo maana Kikwete alijitahidi kuwaonea huruma watanzania kwa kuwachekea na kuwaalika wasanii kwenda kula maandazi na kunywa chai Ikulu.
 
Back
Top Bottom