Muda muafaka kwa jk kondoka na wateule wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muda muafaka kwa jk kondoka na wateule wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanyanga, Jul 20, 2011.

 1. k

  kanyanga Senior Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu Wana JF,ushahidi ulio wazi umethibitisha bila kuacha hata chembe ya Shaka kwamba JK aliruka kuingia Ikulu kwa Kutumia EPA Flight No.2005 iliyoongozwa na Rubani Rostam Abdulrasul Aziz kwenye Control Tower ya Kagoda, Wantanzania wameumeza ukweli huo kwa maumivu makubwa sana huku wakijua Binadamu Rostam Aziz asiye raia wa nchi hii (huo ndio ukweli) na ambaye ni Mwizi anaweza kuamua hatima ya uongozi wa nchi hii kwa kumweka mtu madarakani bila huyo anayewekwa madarakani kujiuliza huyu Mnunuzi wa Uraia wa TZ ana nia gani kwake na Nchi kwa ujumla.Mwizi Rostam hakuhitaji hata kuwa Naibu Katibu Mkuu, ili apate fursa nzuri sana ya KUIBA kwa kadri muda utakavyomruhusu.Nina hakika angetaka hata Uwaziri wa Fedha angechukua, lakini kwa kuwa alikuwa na akili ya Wizi Mu-Kichwa akajiweka kando akiwaacha waroho wa kupenda Escort ya Vin'gora vya kwenye Motorcade wachekelee kuingia mjengoni.Sasa yametimia RA amekwapua ameiba na kufanya kila aina ya ubazazi kwa kiwango cha kutisha na hatimaye ametokomea zake huko alikowekeza.Kwa taarifa zilizo rasmi Rostam kamwe HATAREJEA TENA NCHINI.Richmond imebebwa na JK hilo nalo halina ubishi hata chembe ya shaka,sasa Juzi tumeona mteule wake mwingine Jairo aikiibuka na mtindo wa KUWAHONGA WABUNGE ili wapitishe Budget.Hivi kwa kutumia busara na hekima kuna Mtanzania anayeweza kusimama na kusema nchi hii ina Rais mwenye sifa zinazostahili.

  David Cameron aliyekuwa South Africa amerejea London haraka na amewekwa kiti moto na kamati ya Wabunge kuhusu Phone Hacking Scandal, lakini huku Bongo Jairo akifanya vitu vyake Boss wake anazunguka Pretoria kusikiliza Brass Band ikimpigia National Anthem.Prime Minister wake anakiri mbele ya Bunge kwamba Serikali imechemka, JK ndio kwanza hata kwenye Hotline yake hapatikani.Nauliza waungwana hivi nchi hii TZ inaye Kiongozi au jamaa amejishikiza kwenye kipindi cha mpito ? Kubwa kuliko yote imejidhihirisha kwamba hata maamuzi hayawezi kufikiwa na Wateule wake na baadaye akapewa taarifa, sasa nchi inaingia gizani rasmi kwa kuwa maji katika Bwawa la Mtera yameshuka zaidi ya Mita 9.5 za ujazo na uwezekano wa kuzima mitambo ni mkubwa hadi hapo Mvua za mwezi wa 9 zitakapoanza.Hata hilo bado linaonekana kutomfanya Mkuu kushtuka.Je ni kweli kwamba tunatakiwa kusubiri Mkuu apewe ushauri na first family ? au sasa ni wakati muafaka wa kuangalia njia nyingine ya kumpata mtu sahihi wa kusimamia kwa ukamilifu haya yanayoliua Taifa hili ili balaa linalotunyemelea litupite kando ?
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Du!tuliwaamini wanamagamba madaraka tukawapa sasa tuwaache waljimwage,hamna jinsi,jamaaa hawajihudhuru wala kutoka hata kwa maanamano.cha msimngi ni khusubira katiba mpya n a uchaguzi mwingine wa mwaka 2015,kwasasa hamna namna kwani jamaa washika rungu.
   
Loading...