Muasisi wa Mapinduzi apinga serikali ya mseto Z`bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muasisi wa Mapinduzi apinga serikali ya mseto Z`bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete.  Wakati Rais Jakaya Kikwete anahimiza kuwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ndilo litakalokuwa suluhisho la mpasuko wa kisiasa, mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya mwaka 1964, amepingana na hatua hiyo.
  Mwanasiasa huyo mkongwe Zanzibar, Said Natepe, amesema wazo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa ni zito utekelezaji wake kutokana na baadhi ya wanasiasa kutokuwa na nia njema ya kuwaunganisha Wazanzibari.
  Akizungumza na Nipashe katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar, Natepe alisema matatizo ya kisiasa yamekuwa yakichelewa kupatiwa ufumbuzi Zanzibar kutokana na viongozi kuweka mbele maslahi binafsi.
  Alisema kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar si wazo jipya kwani jambo hilo liliwahi kufanyika kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964. Alisema mwaka 1963 Zanzibar kuliundwa serikali ya mseto na marehemu Mzee Karume alikuwa Waziri wa Afya, lakini kwa kuwa serikali hiyo haikuwa na nia ya kuwaunganisha Wazanzibari kumaliza matatizo yao ndio maana ilishindwa kudumu.
  Alisema suala la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa linajadiliwa kwa kuangaliwa maslahi ya viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar badala ya wananchi.
  “Suala la kuundwa serikali ya mseto ni vigumu kufikiwa Zanzibar kwa sababu tunaangalia zaidi maslahi ya watu, badala ya maslahi ya nchi,” alisema.
  Natepe alieleza kuwa matatizo ya Zanzibar yataondoka kwa kuzingatia suala la kulinda misingi ya umoja wa kitaifa na kuendeleza sera ya Rais wa kwanza wa Zanzibar ya kupiga vita ubaguzi miongoni mwa Wazanzibari.
  Alisema hivi sasa misingi ya Mapinduzi haienziwi kama inavyostahiki, lakini alisema yawezekana mabadiliko ya wakati au kuweka mbele maslahi binafsi na kusisitiza kuwa bado ipo haja ya kuenzi yale yaliyowekwa na waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.
  Natepe alisema kutokana na kukosekana nia njema ya kuwaunganisha Wazanzibari ndio maana Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume akauawa na wapinga Mapinduzi.
  Rais Kikwete alisema wiki iliyopita kuwa wazo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ndio njia pekee ya kumaliza matatizo ya kisiasa yaliyodumu tangu kurejeshwa mfumo wa vyama vingi.
  Alitoa kauli hiyo Jumanne iliyopita alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Maisara, baada ya kupokea maandamano ya vijana wa CCM ya kumuenzi muasisi wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume.
  Alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshalitafakari suala la serikali ya umoja wa kitaifa na kuamua kulirejesha kwa wananchi, kwa vile mfumo huo utapunguza siasa za chuki.
  Rais Kikwete aliwataka wananchi wa Zanzibar kuunga mkono uamuzi huo kwa vile ndio utakaosaidia kujenga umoja wa kitaifa.
  Aliwataka wana CCM wasiwape nafasi watu wanaopotosha lengo la kufikiwa maamuzi ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwa hatua hiyo inaweza kurejesha nyuma mafanikio yaliyokwishafikiwa.
  Uamuzi wa wananchi kupiga kura ya maoni kuamua juu ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar unatokana na azimio la Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM iliyokutana kijijini Butiama, mkoani Mara mwaka 2008 baada ya kupokea mapendekezo ya mazungumzo kati ya CCM na CUF.
  Uamuzi huo ulipata nguvu zaidi Novemba mwaka jana, baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tatizo la zanzibar ni ubinafsi , dharau dhidi ya jamii nyingine , na wanasiasa kuleta usanii katika kuongoza nchi yao, na yote hii inatokana na kuwa na mifumo legevu ya kisiasa na kiuongozi jambo ambalo linaweza kusababisha mahafa makubwa, tungependa kutoa wito kwa viongozi wa zanzibar wawaachie wananchi wao uhuru wa kuamua na si kuwachochea kuelekea kwenye machafuko
  mungu ibariki zanzibar
   
Loading...