Muarobaini wa ufisadi ni Katiba ya Wananchi

Muarobaini wa ufisadi ni Katiba ya Wananchi

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
2,441
Reaction score
653
Muarobaini huu si kingine bali KATIBA YA WANANCHI; hiyo ndio pekee yenye dira ya taifa, vipaumbele na maadili ya uongozi. Mtu kudai atakomesha ufisadi huku anaikataa KATIBA YA WANANCHI anapiga porojo za kawaida na kuwafanya watu ni malofa wa kufikiri.

Kansa inayolitafuna Taifa letu ni rushwa na ufisadi. Bila kuliondoa hili hakuna maendeleo yatakayopatikana wala umaskini hautaondoka. Maraisi wote kuanzanzia awamu ya pili, tatu na nne wameshughulika sana na tatizo hili lakini yumkini hawakufika mbali. Rais Kikwete alikuwa amejivika silaha zote na kwa nia ya dhati alikusudia kulimaliza hili lakini kinyume chake tatizo limezidi kukua. Sasa tunajiuliza kikwazo ni nini?

Niseme tu kwmba kikwazo chetu kikubwa ni kukosekana dira ya Taifa, vipaumbele na maadili ya uongozi. Mambo haya yanapatikana ndani ya Katiba ya wanchi walioikataa baadhi yetu; Hiyo ndiyo nyenzo ya kipekee kabisa ya kuweza kudhibiti tatizo la rushwa na ufisadi.

Katiba madhubuti itasaidia kuwabana viongozi wasichafuke wakiingia madarakani hata kama wangependa kufanya hivyo. Bila katiba madhubuti hata aingie Raisi msafi kiasi gani hakutakuwa na uhakika kwamba yeye mwenyewe hatatumbukia kwenye tatizo lilelile na kuanza kuwaonea aibu marafiki zake. Ilani za vyama kuwa na maadili hazisaidii kitu kwa kuwa haitakuwepo nguvu ya kisheria bila katiba.

Haiwezekani kabisa kabisa kuondoa rushwa na ufisadi kwa Ilani za vyama; kwanza sio kila raia yuko kwenye vyama. Chama kinachoikataa katiba ya wananchi na kuikanusha hadharani hakiwezi kuwa na nyenzo muhimu ya kushughulikia ufisadi hata kingefanya nini. Kitakwama tu hata kama mgombea wao ana nia nzuri kiasi gani na ni msafi kama malaika. Inaanza katiba , zinakuja sheria halafu ndipo vinakuja vyama. Nchi inatawaliwa kwa mujibu wa katiba na sio ilani za vyama. Nadhani UKAWA wanayo agenda hii nzuri tu ya KATIBA YA WANANCHI ambayo itang'oa ufisadi na upotevu wa rasilimali za nchi. Wala huwezi kupeperusha agenda ya ufisadi huku unaiweka kando Katiba ya wananchi inayokupa nguvu hiyo.

KATIBA YA WANANCHI ni agenda kubwa kuliko ufisadi. Huo ndio mwanzo mpya wa taifa letu.; tuangalie mbele na sio kufukua makaburi na kulipa visasi. Watu wanajenga madaraja kwenda mbele sio kurudi nyuma. Kansa imekula taifa zima toka juu hadi chini kwa mwananchi wa kawaida kutokana na umasikini wake; utauwa au kufunga wangapi?

Heri tuanze upya, tutafute muafaka wa kitaifa tuijenge nchi yetu upya chini ya KATIBA YA WANANCHI."
 
MMeshaisigina kwa kuwaweka watu wasio na maadili,wapiga dili,kwa sasa hivi hamna uhalali tena wa kuitetea katiba ya wananchi hata Jaji Warioba aliwashitukia akaachana na ninyi.
 
MMeshaisigina kwa kuwaweka watu wasio na maadili,wapiga dili,kwa sasa hivi hamna uhalali tena wa kuitetea katiba ya wananchi hata Jaji Warioba aliwashitukia akaachana na ninyi.

kwani ccm lini waliwahi itetea katiba ya wananchi?
 
Ccm imetoa tutapata wapi sasa Hapa nikupiga chini Ccm ili tupate katiba ya wananchi kukomesha mafisad Wa Ccm
 
Kama mi katiba ya wananchi lazima wanasiasa waisukume?
Je kuna jimsi wananchi wenyewe tutaweza kuipihania hio katiba?
 
Back
Top Bottom