Je ni kweli Waziri Mkuu Mh. Pinda hakueleweka na wana-Mtwara?
UMOJA wa vyama tisa vya siasa vya upinzani,
vinavyoongoza hoja ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara
kupinga mradi wa usafirishaji wa gesi kwa njia ya bomba
kwenda Dar es Salaam, umekutana na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda na kumfikishia ujumbe unaoeleza kuwa
wananchi wa Mtwara hawajamwelewa.
Kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa Pinda jijini Dar es
Salaam, Jumamosi ya Februari 2, baada ya umoja huo
kukosa nafasi ya kukutana naye kwa mara ya pili, wakati
Waziri Mkuu huyo alipofanya majumuisho ya ziara yake
mkoani Mtwara katika Ukumbi wa Veta mjini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mtwara jana,
mmoja wa wajumbe wa umoja huo Mustafa Nchia,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mtwara
Mjini, alisema kuwa walilazimika kufunga safari kwenda
kuonana na Waziri Mkuu, ili kumfikishia ujumbe kuwa
wananchi wa Mtwara bado hawajamwelewa.
Tulikutana Jumamosi nyumbani kwake Dar es Salaam,
tukamwambia kuwa wananchi wa Mtwara bado
hawajakuelewa Baada ya kumaliza ziara yake katika
majumuisho hakutuuliza kama tumekubaliana au la,
alisema Nchia na kuongeza:
Alikwenda kwenye vyombo vya habari na kusema
amemaliza mgogoro, sisi tumemwambia bado wananchi
wa Mtwara wana manunguniko moyoni mwao, wanataka
gesi isisafirishwe kwa njia ya bomba.
Alieleza pia kwamba walimfikishia Pinda, kilio cha wana-
Mtwara cha kumkataa Mkuu wa Mkoa, Joseph Simbakali,
kwa maelezo kuwa tayari watu wamekosa imani naye,
hivyo hawawezi kushirikiana vyema katika maendeleo.
Januari 28, mwaka huu katika kikao cha majumuisho cha
ziara ya Waziri Mkuu, Simbakalia aliwaomba radhi wakazi
wa mkoa huo kwa kuwaita wapuuzi na baadaye wahaini,
wakati walipomwalika kupokea maandamano yao
Desemba, 27 mwaka uliopita.
Tulimshauri Waziri Mkuu amhamishe siyo tu kwa sababu
watu wa Mtwara hawamtaki, pia hata kama ataendelea
kuwapo Mtwara, watu hawapo tayari kumpa ushirikiano
ili wananchi wa Mtwara wawe na ari ya kutoa ushirikiano
kwa Serikali yao na kufanya kazi vizuri ni vyema
Simbakalia akahamishwa, alisema Nchia.
Aliongeza: Ametuhakikishia kulifikisha hili kwa Rais
Jakaya Kikwete kwa kuwa yeye ndiye aliyemteua ;
Masuala haya mengine alitujibu kuwa ametusikia.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Uledi Abdallah
aliongeza kuwa katika kikao hicho pia walimwomba
Waziri Mkuu awafungulie kuendesha mikutano ya
hadhara, ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi za
mustakabali wa madai yao.
Mtakumbuka kuwa kanda hii ya Kusini kumezuiliwa
kufanya mikutano ya kisiasa, sisi tumemwambia Pinda
kwamba hapo hatatui tatizo bali anaongeza Tatizo la
watu wa Mtwara hawapati taarifa sahihi kwa wakati na
njia ya kuwapa taarifa hizo ni mikutano ambayo
wameizuia Hapo tunaandaa tatizo lingine, alisema
Abdallah na kuongeza:
Iwapo hatutaruhusiwa kuendesha mikutano, tutaandaa
maandamano makubwa ambayo hata kama hatutapata
kibali, tutayafanya kudai haki yetu ya kueleza hisia na
mawazo yetu, haki ya kupata na kutoa habari.
Naye msemaji wa umoja huo Hamza Masoud Licheta
alisema kuwa siyo kweli kwamba umoja huo umehongwa
fedha ulipokwenda kuonana na Waziri Mkuu, bali
ulikwenda kufikisha ujumbe sahihi wa watu wa Mtwara.
Chanzo: Mwananchi, leo.