Mwaka 2020 ni miaka 7 kuanzia sasa na pengine sababu iliyokushawishi kudhani hivyo ni ugunduzi wa mafuta ghafi na gesi huko Mtwara.
Nadhani ndoto kama hizo pia walikuwa nazo wananchi wa Mwadui na Shinyanga kwa ujumla wakati tu Almasi ilipogunduliwa huko.
Sio hao tu bali pia wananchi wa Mererani(wakati huo Arusha), Geita na kwingineko kwenye rasilimali madini.
Hivyo kwangu mimi mada hii naiona kama ni ndoto, ukizingatia ya kwamba sio ndoto zote humuitaji muotaji awe amelala.