Mtumishi Sana Freeman Mbowe

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Sikuiti Mh. Mbowe, kwa sababu kwa kauli, matendo na maisha yako kwa ujumla, Mbowe umekuwa mtumishi badala ya Mheshimiwa. Kwa kauli, matendo, moyo na maisha yako, Freeman Mbowe umedhihirisha pasipo shaka kuwa wewe ni mtumishi wa Watanzania.

Ulitengenezewa kesi ya uwongo na akina Kingai, Siro, Swila na Boaz, kwa baraka za Samia, tena yeye Samia akaweka na msisitizo kuwa eti wewe Mbowe ulikimbia nchi. Umewekwa mahabusu, umenyimwa uhuru wako, umekatishiwa nafasi ya kuwa na familia yake, ukaporwa na ushindi wa ubunge wake, ukaharibiwa shamba na biashara zako, lakini hukuyumba, hukutetereka, wala kubabaika, ulisimama wakati wote kwenye nafasi ya kuwa tayari kuteseka, kudhulumiwa, kudharauliwa, na hata kufirisiwa, kwaajili yetu sisi tulio wengi ambao ni waoga, wanafiki, tusio na ujasiri hata kuwa tayari kulala sero japo siku moja, hasa kwa kuutetea ukweli.

Siwezi kukusema mtumishi Mbowe ni mtakatifu wala utumishi wako siwezi kuufananisha na wa Kristo, lakini ndani yako tumeuona upendo wa kweli, ujasiri wa kweli, na kujitoa kwako kikamilifu kwa sisi Watanzajia wote. Mbowe ungeweza kutamka tu kuwa, kuanzia leo naunga mkono juhudi, toka siku hiyo ungeishi maisha raha mstarehe, lakini hujafanya hivyo.

Mbowe, utumishi wako unaweza kudhaulika leo, unaweza usionekane leo, lakini kuna siku utavikwa taji kwa sababu ya sadaka kubwa hizi ulizozitoa kwaajili yetu. Mimi nasema kuwa, nguvu uliyo nayo siyo ya kawaida, ujasiri wako si wa nguvu yako, bali ndani yako kuna yeye akutiaye nguvu, ambaye uendelee kumpa nafasi, uzidi kumsikiliza, maana katika wewe wengi tutapona. Pamoja nawe, wapo wengi, nyote tunawashukuru. Tundu Lisu, Lema, Msigwa, Sugu, Rose Mayemba, Mdee (kamba hukatikia pembamba), na wengine pia, hakika furahini maana ndani mwenu kuna nguvu kubwa.

Mtumishi Mbowe, tunakuomba msamaha, maana pale ulipohitaji nguvu yetu hukuiona, ulipotaka kuuona ujasiri wetu ukakosekana, siyo kwa sababu tunafurahia matendo yasiyo haki, bali roho ya ibilisi, imetujenga katika uoga.

Mtumishi Mbowe nakupongeza sana, siyo kwa sababu umeachiwa huru bali kwa sababu umesimama katika ukweli, haki na dhamira sahihi, toka mwanzo mpaka mwisho. Na mwisho, shetani hakuwa na namna nyingine yoyote, zaidi ya kukiri kuwà waliokutendea uovu na ushetani.

Siku si nyingi, kwa uweza wa Mungu, nitafurahi nikipata nafasi ya kukuona japo najua majukumu yako ni mengi.

Asante Mungu wetu, maana waliodhani watashinda katika uovu wao, badala ya ushindi, wamejidhihirisha kwa uovu wao katika Ulimwengu wote.
 
Picha_ya_pamoja_Mh._Freeman_Mbowe_akiwa_na_wenzake_baada_ya_kutoka_Gerezani_leo_tarehe_4.03.20...jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom