Facebook ni mtandao wa jamìi mkubwa dunia nzima na ndo una uwezo mkubwa wa kukusanya data ikiifuatia Google...data zinazokusanywa sio za marekani na europe bali hata africa..think about this scenario ya ukweli ya majuzi..nilipewa number ya mtu X simfahamu hanifahamu..number yangu ya tigo yake ya vodacom. Tumetumiana sms 4 za kawaida then saa moja mbele naingia mtandao wa facebook na jina la kwanza naliona kwenye list ya 'People you may know' ni la mtu X.. Nafungua profile yake cha kushangaza hatuna hata mutual friend mmoja...number yangu ya tigo ndio niliyoijaza kwenye facebook verification process na pia naitumia whatsapp..nafahamu mitandao ya simu imeingia ubia na facebook ili wateja waweze kujiunga na kuaccess facebook bure ila wateja wao hatujui mikataba yao wamekubaliana nini kuhusu utunzaji wa taarifa zetu muhimu...Currently nawatafuta tigo kuwauliza kuhusu my customer rights of privacy.. Yaliyonitokea hayawezi kuwa coincidence huwezi jua private information gani hii mitandao ya jamii wanaweza kuzisoma kupitia simu za mkononi so be careful guys.