Mtulia na Godwin mtawaambia nini wananchi wa majimbo haya?

Mtulia badala ya kuwaomba radhi wapigakura na wananchi wa kinondoni yeye ameenda kuwaomba radhi CCM eti kwa kuwashinda kwa kishindo mwaka 2015.
Bora ukose mali lakini upate akili.
 
Kukataliwa hadharani na kwenye box la kura ndio adhabu yao inayowastahili. Hawawezi kutufanya wajinga kiasi hicho!

Najiuliza wataomba kura kwa style gani?

Hiv wananchi wa majimbo haya wanaweza kuwachagua wasaliti hawa tena?

Hiv wananchi wa majimbo haya watakuwa wapumbavu kiasi gan kuwachagua wasaliti hawa tena?

Kama 2015 waliacha kumchagua Aggrey mwanri wakamchagua Mollel(lofa) kwa kuwa n mpinzani ndo waje wamchague kupitia ccm??

Sidhani kama wananchi wa siha watakuwa wapumbavu kiasi hiki hivyo hvyo kwa jimbo la Kinondoni.....
 
Mtulia badala ya kuwaomba radhi wapigakura na wananchi wa kinondoni yeye ameenda kuwaomba radhi CCM eti kwa kuwashinda kwa kishindo mwaka 2015.
Bora ukose mali lakini upate akili.

Maajabu haya,

Ée Mungu naomba uwatembelee wananchi hawa siku ya upigaji kura....majimbo haya yarudi upinzani....
 
Najiuliza wataomba kura kwa style gani?

Hiv wananchi wa majimbo haya wanaweza kuwachagua wasaliti hawa tena?

Hiv wananchi wa majimbo haya watakuwa wapumbavu kiasi gan kuwachagua wasaliti hawa tena?

Kama 2015 waliacha kumchagua Aggrey mwanri wakamchagua Mollel(lofa) kwa kuwa n mpinzani ndo waje wamchague kupitia ccm??

Sidhani kama wananchi wa siha watakuwa wapumbavu kiasi hiki hivyo hvyo kwa jimbo la Kinondoni.....
Huku kwetu Siha tutamnyoosha huyu Dr, (Mollel) anayerubunika kijinga namna ile, ---a PhD holder? Au huo u-Dr wake ni kama ule wa prof. Majimafupi?
 
Cdm ningependa wajipange vizuri pindi watakapokuwa wanapanda jukwaani, wapange watu mahiri wa kuongea. Napendekeza wajipange kwenye mambo manne. tuchukulie mkutano wa wa masaa mawili.
  1. Uchumi: Hapa waelezee hali ya sasa ya uchumi nchini, ikiwemo ajira, kilimo nk Wawe na mchumi mzuri kwa kuelezea hii redundancy inayoitwa vyeti fake bila nafasi hizo kujazwa. Mabenk kufilisika, mikopo ya wanafunzi, ahadi za ccm kutokutekelezeka kama 50m@kijiji/mtaa, Kwanini umeme wa stiegler gorge, wakati awamu iliyopita tuliambiwa gas ndio kila kitu mpaka tukawa tunaimbishwa nchi nzima kama wendawazimu kuhusu uchumi wa gas. Hapa zitumike dakika 20-25.
  2. Hali ya siasa hapa nchini: Hapa izungumziwe demokrasia inavyominywa ikiwemo vyama vya upinzani kunyimwakufanya siasa lakini ccm ikiachiwa kutamba. Kupotea kwa watu kama Ben saa 8, mwandishi wa habari, shambulio la Tundu Lissu na kunyimwa haki za matibabu nk. Nashauri hapa kuwe na vijembe vya kisiasa na sio kejeli na matusi na hasa ikibidi hilo jina la kumuita Magufuli dictator lisitumike sana kwani ndio wanapopata kisingizio cha kusumbua wapinzani. Hapa ielezwe madhara ya kujaza wabunge wa ccm kwani wanaunga mkono hata mikataba mibovu na itolewe mifano kama walivyopitisha sheria ya gas na leo hawazungumzi lolote, Itumike tafsida kuelezea udictator wake. Hapa dakika 20-25.
  3. Cdm watafanya nini: Hapa cdm inabidi wawe wazuri kuonyesha iwapo wao watapewa madaraka watafanya nini kwenye ajira, maendeleo ya watu kama kujenga nyumba bora kwa kupunguza bei za vifaa vya ujenzi, zahanati kila kata, elimu bure mpaka chuo kikuu bure, kurejesha demokrasia, kurejesha uhusiano mwema na wafanya biashara, nk Hapa dk 20-25. Pia wanaweza kuweka dk 10-15 za maswali wangalau matatu na majibu kila mkutano.
  4. Mgombea kuzungumzia jimbo analolipigania matatizo na utekelezaji wake. Ahakikishe anapata taarifa za jimbo lake kupitia madiwani mbalimbali walioko hapo. Yeye ajikite kwenye matatizo ya watu wa jimbo lake tu, na siasa nyingine za kitaifa aachie wengine kama nilivyoainisha hapo juu. hapa atumie dk 30
Cdm wahakikishe wanafanya siasa za kistaarabu bila woga, lakini wawe na watu mahiri kwenye kuongea majukwaani na sio yale mambo ya kusema ilani iko kwenye website. Kisha wawe na watu watakoaratibu kutoa habari kwenye uchaguzi kuanzia vyombo vya habari rasmi na kwenye mitandao ya kijamii. Hapa picha na ujumbe wa kampeni ufike vyema. Tukio lolote ovu liripotiwe kwa nguvu kubwa. Siku ya uchaguzi tatizo lolote lijazwe kwenye makabrasha husika. Kwa mtindo huu tutakuwa tumewabana ccm vyema na sio kampeni za kishabiki tu bila mpangilio mzuri.
 
Sie wabongo bado sana kwenye kujitambua ndio maana ccm hiyo ndiyo njia yao kubwa ya kufanikisha mambo yao
Subiri kampeni utaona jinsi wajinga watakavyojazana kwenye mikutano ya ccm huku wengine wakipewa pilau na kusahau shida zao,vipofu wa fikra nchi hii watazidi kuongezeka kila siku
 
"Wameandaliwa green guards wakutosha kushusha kipigo kwa vijana wa ukawa. Siku ya kupiga kura ndiyo kabisaaa, mawakala watapigwa kipigo cha mbwa mwizi. Mtulia na Mollel lazima washinde"..

Hii imeandikwa kwenye Facebook na mmoja wa wanaccm.

Ukawa mmejipangaje kwa hilo?
 
Back
Top Bottom