Mtulia atema cheche, ateka hisia za wengi

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI KWA TIKETI YA CCM, NDUGU MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA MZIMU JUMAPILI FEBRUARI 4, 2018*

"Mimi nimefanya ubaya kutoka kwenye chama kisicho na kitu kuja kwenye chama chenye dola kinacholeta maendeleo? Huo ndio usaliti" - Mtulia

"Kuna tofauti kubwa kati ya Mtulia yule aliyekuwepo CUF na huyu ambaye amekuja kushirikiana na chama cha Mapinduzi @ccm_tanzania kuleta maendeleo." - Mtulia

"Kwa chama kile ningepata wapi hata uwezo wa kuwaletea maendeleo kwa migogoro isiyokwisha kila siku nimsikilize nani? Katibu au Mwenyekiti?" - Mtulia

"Nilipojiunga chama cha Mapinduzi @ccm_tanzania sikutegemea kama ntakuja kuteuliwa niliingia kwa Moyo mmoja wa kupigania maendeleo, Siingii vikao vya maamuzi mimi ila CCM waliona nafaa kurudi tena hapa kuendeleza mazuri niliyopigania." - Mtulia

"Katika hospital zetu hizi wanatabiwa Watanzania maskini wapo ndugu zetu hushindwa kulipa gharama za matibabu ikitokea bahati mbaya amefariki ameshindwa kulipa gharama za matibabu Mhe. Rais @MagufuliJP nakuomba hawa watu wasamehewe madeni yao." - Mtulia

"Nitahakikisha nasimamia vyema daraja la Madaba linajengwa, Shule ya Mzimuni na Mikumi zinaboreshwa, Madaraja yanajengwa na yanachimbwa, Barabara zinajengwa, Kadi za bima za afya za Wazee zinatolewa mapema iwezekanavyo na mikopo nafuu ya Vijana na Wanawake toka Manispaa inatolewa kabla ya mwezi huu kuisha. Pesa zipo tayari." - Mtulia

"Mie sina ubaguzi wa vyama japokuwa ni CCM, navipenda vyama vyote. Mkinichagua nitawatumikia Watu wote pasipo kujali itikadi" - Mtulia

"Nawaombeni Watu wote hapa mjitume kuhakikisha mnaniombea kura za ndiyo kwa Watu wote wakazi wa Kinondoni waliopo Majumbani wajitokeze Februari 17 wanipigie KURA ZA NDIYO" - Mtulia
IMG-20180204-WA0028.jpg
IMG-20180204-WA0031.jpg
IMG-20180204-WA0026.jpg
IMG-20180204-WA0023.jpg
IMG-20180204-WA0033.jpg
IMG-20180204-WA0033.jpg
IMG-20180204-WA0018.jpg
IMG-20180204-WA0019.jpg
 
CCM MNAFANYA KAMPENI za nini wakati TUME na Mashehe ni wenu?
Kwa kuwa upinzani umerudi kwenye ulingo wa siasa za ushindani, hakuna sababu za kuanza kujenga sababu za kushindwa.

Viongozi wa upinzani agenda yao kubwa ya kampeni ni kwamba mgonlmbea wa CCM ni msaliti. Naamini wakiutumia vizuri ni kete kubwa ya kupata kura.

Lakini wakumbuke kuwa wameshangilia walipowapokea waliohama CCM na mmoja wao kumpa nafasi kubwa ya kugombea Urais, hawakumwita msaliti!!

Mjinga na mwongo kamwe hakumbuki. Ni upumbavu na ulofa
 
Mtulia ni Mbunge mtarajiwa
Kinondoni hawachagui Mamluki toka Mashariki ya mbali!
 
Mtulia atafute kazi nyingine hiyo alishapoteza na uzuri ni kwamba yy mwenyewe anajua
 
Back
Top Bottom