Mtuhumiwa wa mauaji ajaribu kutoroka polisi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) wilayani Kiteto mkoani Manyara, aliyekuwa mikononi kwa polisi amejaribu kutoroka lakini hakufanikiwa.

Mtuhumiwa huyo (jina linahifadhiwa) ambaye yupo kituo cha polisi Kibaya, anatuhumiwa kumuua kwa kumpiga usoni na kitu kinachodhaniwa kuwa ni butu ofisa wa Takukuru, Evanjelina Samson (39) Julai 18 mwaka huu saa 4 usiku.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema kuwa ni kweli mtuhumiwa huyo alitaka kutoroka mikononi mwa polisi jana ila hakufanikiwa na hadi hivi sasa anaendelea kushikiliwa na polisi.

Kamanda Massawe amesema kulikuwa na habari potofu zilizokuwa zinaendelea kwenye viunga vya maeneo ya Kibaya kuwa mtuhumiwa huyo wa mauaji alitoroka jambo ambalo siyo la kweli kwani wanaendelea kumshikilia.
 
Wakimuachia wao ndiyo wataibeba hiyo kesi na hukumu yake, ifike wakati sasa tuwe seriuos na majukumu....
 
Wa Mwangosi ameua bila kukusudia haya ngoja tumsubiri huyo hukumu yake
 
Back
Top Bottom